Nakupongeza RC Chalamila kurudisha mabasi ya mkoani Mbezi Magufuli, bado hili la malori!

Nakupongeza RC Chalamila kurudisha mabasi ya mkoani Mbezi Magufuli, bado hili la malori!

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,308
Reaction score
12,812
1. Nianze hii sledi pendwa kwa kukupongeza RC Chalamila kwa hatua ya kurejesha mabasi ya mikoani katika eneo la Mbezi Magufuli. Ni hatua nzuri katika kupunguza msongamano na usumbufu kwa wakazi wa Dar es Salaam.

2. Sasa tuangalie tatizo jingine kubwa: malori na ICDs zilizo ndani ya jiji.

3. Dar es Salaam ina ICDs nyingi zinazohifadhi mizigo inayokwenda mikoani na nchi jirani. Mizigo hii inapofika bandarini, badala ya kuingia moja kwa moja kwenye maeneo ya nje ya jiji, malori yanaingia katikati ya Dar es Salaam kwenda kupakia, kushusha au kusubiri.

4. Hii inachangia sana foleni, hasa kwenye barabara kuu zinazoingia na kutoka jijini.

5. ICDs zote zinazohudumia mizigo ya transit na mizigo inayokwenda mikoani zipunguzwe au ziondolewe katikati ya jiji. Ziwekwe maeneo ya pembezoni ambako malori yanaweza kufanya shughuli zao bila kuathiri usafiri wa wananchi katikati ya jiji la Dar na viunga vyake.

6. Maeneo kama Kibaha, Mlandizi, Bagamoyo na maeneo mengine ya nje ya jiji yanaweza kuendelezwa kuwa vituo vikubwa vya logistics/ICDs vikisaidiana na ICD ya Kwala.

7. Hata kwa ICDs za magari ya IT (In Transit), kama wawekezaji wana nia ya kuendelea na biashara hiyo, serikali inaweza kuwaelekeza kuanzisha vituo vyao nje ya jiji, badala ya magari makubwa kwa madogo kuingia katikati ya Dar es Salaam.

8. Hii siyo kuzuia biashara. Ni kupanga matumizi ya ardhi na shughuli za logistics kwa namna inayolingana na ukubwa wa Dar es Salaam.

9. Pia, faini ya maegesho mabaya iwe kubwa zaidi, hasa kwa magari yanayozuia njia za zinazotumika, barabara na maeneo yaliyotengwa kwa usafiri.

10. Daladala zinazopakia na kushusha abiria nje ya vituo(hii imekuwa tabia sugu, madereva wa daladala kupakia mwanzo wa kituo hawataki kuingia kituoni kabisa), pamoja na bajaji zinazopaki au kusimama kiholela(hasa hii Morogoro road), nazo ziwekwe kwenye mfumo mkali wa utekelezaji wa sheria na faini ziwe nzito. Kama wanavyoshughulikiwa bodaboda mjini hawa daladala nao msiwachekee wanasababisha sana foleni hasa njia ya Morogoro.

11. Sheria ikiwa ipo lakini faini ni ndogo kiasi kwamba mtu anaona ni gharama ya kawaida ya biashara, nidhamu ya barabarani haitajengeka. Faini igongwe nzito hasa, Manispaa na Majiji huko duniani kwingine huwa hawacheki na uholela mjini, hata Rwanda tu hapo ujinga mjini marufuku!

12. Tukiunganisha uhamishaji wa ICDs na vituo vya malori nje ya jiji + udhibiti mkali wa maegesho + matumizi sahihi ya vituo vya daladala + nidhamu ya bajaji, tunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa foleni za Dar es Salaam na tukagudundua kwamba sio kweli barabara zetu ni finyu sana bali tatizo uholela.

13. Dar es Salaam ni jiji la biashara na lango la nchi nyingi za Afrika Mashariki na Kati. Tunahitaji logistics zinazofanya kazi vizuri na kwa wakati, lakini zisifanyike kwa gharama ya muda wa mamilioni ya wasafiri kila siku na kupoteza mapato mengi ya nchi.

Hongera RC Chalamila kwa hatua ya Mbezi Magufuli. Sasa tuende hatua inayofuata: MALORI NA ICDs. Hapa wanasiasa msiogopane ambianeni ukweli na lobbyists muwadhibiti wasitangulize rushwa kufanya hii mikakati kuwa haiwezekani!

Dar es Salaam tunaweza kuifanya iwe safi, yenye mpangilio na yenye usafiri unaotabirika na ikawa na sura halisi ya "Jiji la Kibiashara"

Tuache uholela.

In the memory of Afande wa Trafiki Mwaibula.
 
Back
Top Bottom