Nakupongeza sana Maulid Kitenge kwa kumjibu Shaka Hamdu Shaka kuhusu Katiba

Nakupongeza sana Maulid Kitenge kwa kumjibu Shaka Hamdu Shaka kuhusu Katiba

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2019
Posts
9,863
Reaction score
20,806
Watanzania,

Binafsi nampongeza Sana Ndugu yangu Maulidi kitenge kwa nondo zilizoshiba za kumjibu Shaka Hamdu shaka kuhusu Katiba Mpya na ushirikishwaji wake KWA wananchi!

Kitenge amemjibu shaka KWA kusema"wananchi wote walishashirikishwa swala la katiba mpya tena makundi yote kuanzia MAMA ntilie,machinga Hadi wananchi wa kawaida!!kilichobaki ni kumalizia tulipoishia kwani Rasimu ya Warioba ilishapatikana na itumike kupata katiba mpya tu Basi!!!

Ameongeza KWA kusema "labda Ndugu shaka wakati tunashirikishwa wewe ulikuwa mchanga Sana kisiasa KWA hiyo wananchi walishashirikishwa hivyo mchakato uanzie pale tulipoishia na si vinginevyo!!!

Tunawahitaji Sana wanahabari wengi Sana wa aina hii Hapa nchini!
Ni dhahiri chama tawala kina Mpango maksudi KABISA wa kuchelewesha mchakato huu Ili uchaguzi 2025 ufanyike KWA katiba ya zamani Ili washinde KWA kumtumia polisi kama 2020.

Shaka anapaswa kujua kuwa mchakato huu kikwete aliuanzisha na Samiah akawa Mwenyekiti wa Binge lile la katiba na wananchi walishirikishwa KWA hiyo watanzania hawatokua ngonjera Muda umefika wajiandae tu kisaikolojia KWA uchaguzi huru na haki wa katiba mpya na sio vinginevyo.

Kumbuka katiba mpya Sio takwa la CCM wala CHADEMA bali la wananchi wenye nchi na hatuhitaji hisani ya Mwenyekiti wa CHAMA chochote cha siasa ili tuipate!hivyo haizuliki unakuja kama mafuriko.

Niwaombe waandishi wa habari na watangazaji muanze rasmi KWENYE vituo vyenu vya redio na Television kutangaza takwa la katiba bila uoga wala Soni!!!

Moderators naomba mpachike ile clip ya kitenge kama mnayo! Mimi sijapata nimeisikia redioni tu!

Asanteni kwa muda
 
Hivi Maza alimuokota wapi huyu Shaka .... sidhani kama anajua majukumu yake na mipaka ya kazi yake. Yaani naona anakuja na mawazo yake binafsi na kuyatoa kama vile ni ya chama. Chama chake kilishakaa na wakaamua na akatupa taarifa ya nini walikiaamua .... sasa anakuja upya na kujifanya ni Spinning Master ...... Seriously!!
 
Hivi Maza alimuokota wapi huyu Shaka .... sidhani kama anajua majukumu yake na mipaka ya kazi yake. Yaani naona anakuja na mawazo yake binafsi na kuyatoa kama vile ni ya chama. Chama chake kilishakaa na wakaamua na akatupa taarifa ya nini walikiaamua, sasa anakuja upya na kujifanya ni Spinning Master. Seriously!!
Mkuu nasikia Eti ni Mtoto wa Dada SIJUI!!!

Mama aliongozwa na hofu ZAIDI KWENYE uteuzi huu!

Aliogopa matamko fualni yatakayo kinzana na wizi Wake wa kalamu kupitia mikopo ya wahisani!
Ilikuwa lazima amweke msemaji wa mazuri yake na sio mabaya!!
 
Hivi Maza alimuokota wapi huyu Shaka .... sidhani kama anajua majukumu yake na mipaka ya kazi yake. Yaani naona anakuja na mawazo yake binafsi na kuyatoa kama vile ni ya chama. Chama chake kilishakaa na wakaamua na akatupa taarifa ya nini walikiaamua .... sasa anakuja upya na kujifanya ni Spinning Master ...... Seriously!!
Alimtoa kwenye uchunguzi akiwa chini ya ulinzi kwa tuhuma za Rushwa mkoani Morogoro.
 
Hivi Maza alimuokota wapi huyu Shaka .... sidhani kama anajua majukumu yake na mipaka ya kazi yake. Yaani naona anakuja na mawazo yake binafsi na kuyatoa kama vile ni ya chama. Chama chake kilishakaa na wakaamua na akatupa taarifa ya nini walikiaamua .... sasa anakuja upya na kujifanya ni Spinning Master ...... Seriously!!
Tatizo la Shaka ni ile 'jinsia' yake.
 
Mauldi Kitenge ni mchumia tumbo tu, kipindi cha dikteta mbona alikuwa kimya kuhusu katiba mpya?
 
Ulichosikiw redioni ndicho ulipaswa kukiandika hapa siyo lazima hicho kipamde cha sinema.

Attach maneno uliyosikia.
 
Back
Top Bottom