Maandamano kama haya ndio ya Muhimu sio Yale ya Wanasiasa ya kupigania maslahi Yao Binafsi lakini kinapokuja suala la maslahi ya Wananchi wanakaa pembeni.
Wananchi rasilimali zao zinaporwa.
Bandari imegawiwa Wageni.
Misitu wamepewa Wageni.
Wanyama Wetu ni Mali ya Wageni.
Ardhi inagawiwa Wageni.
Upepo imejaa Kanda ya Kati Yote na joto la kutosha kuzalisha umeme.
Walipewa zaidi ya trion moja Kukarabati miundombinu ya umeme. Wakatuambia watazalisha nguzo za zege Badala yake wanatuletea nguzo za miti kama kawaida.
Nguvu kubwa waliyoweieza kwenye nguzo wangeweza kukamilisha bwawa la Mwalimu Nyerere.
Gesi IPO ya kumwaga kuna mgao Wa umeme .
Bado IPTL wapo kuna mgao Wa umeme.
Tatizo ni kwamba kuna watu na manyani.
Nyani Hawelawezi kuwatawala watu Bali watu wanaotawala manyani .
Nimemwelewa Yule mwimbaji ,Wanatuona Nyani.
Wanasiasa wametuzarau sana .
Leo VYAMA VYA UPINZANI HAWATAKI KUSHIRIKI MAANDAMANO YANAYOGUSA MAISHA YA WATANZANIA WOTE .
Wamesahau kuwa Kesho kwenye uchaguzi wataibiwa kura na Nguvu ya kuwapa ushindi ni maandamano ya Wananchi.
Ni vyema wapinzani wakajitafakari kuwa karibu na Wananchi kupigania maslahi ya Wananchi Ili Kesho wananchi nao waandamane kupigania ushindi Wa wapinzani.
Leo ukasema unaitisha maandamano ya Kudai Katiba Mpya huwezi kupata Watu wakati vijana wanaokosa vipato Kwenye saluni , stationary, vinywaji , nyama zinaoza Kwenye mabucha,Samaki zinaoza Kwenye mabucha , vyakula majumbani vinaoza , Viwanda vidogo vya kuchomea vyuma havifanyi kazi.Uzalishaji umedorora Kwa sababu hakuna umeme. Wajanja walihujumu Kila mbinu ya kuondoa tatizo la umeme Kwa manufaa yao.
Wapinzani jitokezeni kuungana na Wananchi Kwenye matatizo yanayogusa watanzania Wote leo.
Vyama vya Upinzani vimesahau kuwa miaka yote walikua wanashinda na kutangazwa Kwa nguvu ya MAANDAMANO ya Wananchi ?
Leo Chama kama Chadema kimesahau kuwa Wabunge wake wote walikua wanatangazwa Kwa MAANDAMANO ya Wananchi ?? Wananchi Hao Hao wanaotegemewa kuandamana kupigania ushindi Wa wabunge Wa Upinzani leo wanataka kuandamana Kupinga kuuzwa Kwa bandari zetu na rasilimali zetu Zote Kwa Wageni lakini Chadema imekaa pembeni Kwa hasira kuwa Wakati Wa MAGUFULI hawakuandamana .Lakini wanasahau KUWA MAGUFULI alikua ni kipenzi cha wananchi walio wengi. Kwa hiyo Kidemokrasia MAGUFULI alikua anaongoza Watu Kwa ajili ya Watu na Kwa faida ya Watu walio wengi.
Wapinzani mnaua wenyewe moyo Wa wananchi kuandamana matokeo yake Kesho mkihitaji MAANDAMANO yanayohusu siasa hawataandamana mana hayawagusi walio wengi moja Kwa moja.
Wakati Wa Magufuli miaka mitano hakuna tatizo la Umeme. Leo tatizo ni kubwa sana je, Magufuli alikua anazalidha Umeme.????
Jibu ni kwamba Wezi na wahuni hawatakiwi kupewa nafasi ya kupanga bila kusimamiwa.
Hotuba za MAGUFULI zinaonyesha wazi kuwa ni MTU aliyekua anajua michongo Yote iliyokua inafanywa na wahuni ndani ya mashirika ya umma na viongozi Wa Serikali.
Asichogundua Rais Wa Sasa Wa Bangladeshi ni kwamba Wabangladesh wanasimamiwa Kwa mtutu Wa Bunduki muda Wote na anayeharibu anapigwa hapo hapo Ili anayeingia afanye kazi Kwa uaminifu.
Haiwezekani uwape mwanya Wabangladesh wanaowaza kupata pesa za kulewa pombe Kila Siku wanapoingia Kazini. Yaani watumishi wangi wakifika ofisini wanawaza pesa za ziada za pombe na wanawake. Sasa Watu Kama Hao ni Lazima wasimamiwe Kwa Nguvu kubwa sana .
Ukija Mawaziri na wengineo wanawaza pesa za kuhongo Kwenye uchaguzi . Hawa wanatumia mashirika yaliyoko Kwenye wizara zao kama Sehemu ya madili Yao Kwa kufanya Kila hujuma alimradi watengeneze pesa Kwa ajili ya kuhonga Kwenye majimbo Yao na kuoneana Kama wafadhili Wa majimbo ya uchaguzi.
Aliyekuye kuwa Rais Wa Tanzania Hayato Magufuli alifanikiwa Kwa sababu alijua tabia za wahuni Kwa kiwango kikubwa na hakuwa na Rafiki Wa kudumu linapokuja suala la maslahi ya nchi.