Nakusudia kuitisha maadamano makubwa nchi nzima ili kupinga mgao wa umeme ambao ni wa kutengenezwa ili kuumiza wananchi!!

Nakusudia kuitisha maadamano makubwa nchi nzima ili kupinga mgao wa umeme ambao ni wa kutengenezwa ili kuumiza wananchi!!

Attachments

  • IMG-20230927-WA0006.jpg
    IMG-20230927-WA0006.jpg
    40.9 KB · Views: 2
Jamani naomba mniunge mkono biashara yangu inakufa tra wanataka Kodi yao mwenye frem anataka Kodi yake nayaona maisha yangu yanakufa hivihivi.

Kilichonikatisha tamaa ni kuona serikali imerelax kabisa haina hata wasiwasi. Wanakuja na majibu rahisi mno, eti tusubiri miezi 6!!!

Naomba watanzania kwa umoja wetu tuungane bila kujali vyama vyetu maadamu unaumizwa na suala la kukatikakatika Kwa umeme, tuiambie serikali kwa njia ya maandamano makubwa yasiyo na kikomo mpaka iwashe umeme.

Haiwezekani watu tuliowaajiri watutatulie KERO zetu watupuuze namna hii.

Tuungane kusema noooo!!
Tunataka umeme au ondokeni ofisini.
Duh kabla ht hatujaona maandamano ya Mdude wewe unaleta mengine tena
 
Tuishtaki TANESCO. imepewa monopoly kwenye umeme na imeshindwa kazi. Inyang'anywe monopoly na kuvunjwa kabisa.
 
Haiwezekani tuwe na viongozi alafu watuambie hawakufanya service hilo sio jukumu letu sie jukumu letu ni kulipa Kodi serikali itupe umeme
Walipokuwa wanafanya service ikawa inawalazimu kuzima baadhi ya mitambo ili kuifanyia service wananchi tukalalamika sababu ilipelekea umeme kupungua baada ya uzimwaji wa hizo mashine, tukapata kiongozi mmoja anaecheza na jukwaa akaamuru hakuna kufanya service ili umeme usikatike na ikawa hivyo.

Sasa mitambo bila service nadhani hata wewe unajua kinachoenda kutokea. Imeharibika zaidi na inataka service kubwa zaidi bahati mbaya kiongozi wa sasa haamini kwenye kucheza na majukwaa kaamua kuruhusu service kunusuru mitambo ni lazima kuwe na upungufu wa umeme.

Tatizo la kimsingi ni kuwa tunazalisha umeme mdogo kuliko matumizi yetu na bahati mbaya yanaongezeka kila siku. Ingalikuwa tuna vyanzo vingi vya kuzalisha umeme basi hata kuzimwa kwa mtambo mmoja au 2 ili ifanyiwe service kusingekuwa na impact kubwa Sana kwenye upatikanaji wa umeme.

Kwa Hali ilivyo sasa hata umlete Malaika au Nani sijui awe MD wa Tanesco tutaendelea kupata mgao. Subiri masika Ije mabwawa yajae kuwe na umeme mwingi maisha yaendelee
 
Unaweza kuwa na points ila acha kuwa brainwashed kuwa mgao ni wa kutengeneza

Shirikisha akili yako ukiambiwa kitu. Hakuna mtu anaweza tengeneza mgao wa umeme nchi nzima.
Tatizo ni nini haswa?, mitambo imechakaa, maji ya kuendesha hakuna au tatizo ni lipi haswa?.

JPM alihakikisha mgao wa umeme haupo, aliweza vipi yeye na Samia anashindwa vipi?.
 
Walipokuwa wanafanya service ikawa inawalazimu kuzima baadhi ya mitambo ili kuifanyia service wananchi tukalalamika sababu ilipelekea umeme kupungua baada ya uzimwaji wa hizo mashine, tukapata kiongozi mmoja anaecheza na jukwaa akaamuru hakuna kufanya service ili umeme usikatike na ikawa hivyo.

Sasa mitambo bila service nadhani hata wewe unajua kinachoenda kutokea. Imeharibika zaidi na inataka service kubwa zaidi bahati mbaya kiongozi wa sasa haamini kwenye kucheza na majukwaa kaamua kuruhusu service kunusuru mitambo ni lazima kuwe na upungufu wa umeme.

Tatizo la kimsingi ni kuwa tunazalisha umeme mdogo kuliko matumizi yetu na bahati mbaya yanaongezeka kila siku. Ingalikuwa tuna vyanzo vingi vya kuzalisha umeme basi hata kuzimwa kwa mtambo mmoja au 2 ili ifanyiwe service kusingekuwa na impact kubwa Sana kwenye upatikanaji wa umeme.

Kwa Hali ilivyo sasa hata umlete Malaika au Nani sijui awe MD wa Tanesco tutaendelea kupata mgao. Subiri masika Ije mabwawa yajae kuwe na umeme mwingi maisha yaendelee
Masika yakiondoka ukija ukame, tunarudi kule kule kwenye mgao mwingine!. Hatujifunzi chochote kutokana na matatizo ya miaka ya nyuma?.

Ni hatari kuwa na taifa linalotaka usafiri wa kisasa nchi nzima halafu nishati yenyewe ya kulenga na manati.
 
ukikusudia kufanya maandamano hutaamini kuna wanasiasa wakatu wa CCM kama sio wanne watalipa fedha za hayo maandamano mpaka mawe yaandamane. Anafikiri wanampenda kumbe wanamalengo yao
 
Walipokuwa wanafanya service ikawa inawalazimu kuzima baadhi ya mitambo ili kuifanyia service wananchi tukalalamika sababu ilipelekea umeme kupungua baada ya uzimwaji wa hizo mashine, tukapata kiongozi mmoja anaecheza na jukwaa akaamuru hakuna kufanya service ili umeme usikatike na ikawa hivyo.

Sasa mitambo bila service nadhani hata wewe unajua kinachoenda kutokea. Imeharibika zaidi na inataka service kubwa zaidi bahati mbaya kiongozi wa sasa haamini kwenye kucheza na majukwaa kaamua kuruhusu service kunusuru mitambo ni lazima kuwe na upungufu wa umeme.

Tatizo la kimsingi ni kuwa tunazalisha umeme mdogo kuliko matumizi yetu na bahati mbaya yanaongezeka kila siku. Ingalikuwa tuna vyanzo vingi vya kuzalisha umeme basi hata kuzimwa kwa mtambo mmoja au 2 ili ifanyiwe service kusingekuwa na impact kubwa Sana kwenye upatikanaji wa umeme.

Kwa Hali ilivyo sasa hata umlete Malaika au Nani sijui awe MD wa Tanesco tutaendelea kupata mgao. Subiri masika Ije mabwawa yajae kuwe na umeme mwingi maisha yaendelee
We jamaa nyumbani kwako kuna sola?
 
Check comment number 28 hapo juu mkuu
Kuna viwanda vingi vinajengwa, hii biashara ya kupangisha bandari inakuja na wingi wa waanzishaji wa viwanda ambavyo vinatumia umeme.

Nini mkakati wa kiserikali wa kuja na vyanzo vya kisasa ikiwa maono yanayoongoza nchi ni ya kisasa?.
 
Walipokuwa wanafanya service ikawa inawalazimu kuzima baadhi ya mitambo ili kuifanyia service wananchi tukalalamika sababu ilipelekea umeme kupungua baada ya uzimwaji wa hizo mashine, tukapata kiongozi mmoja anaecheza na jukwaa akaamuru hakuna kufanya service ili umeme usikatike na ikawa hivyo.

Sasa mitambo bila service nadhani hata wewe unajua kinachoenda kutokea. Imeharibika zaidi na inataka service kubwa zaidi bahati mbaya kiongozi wa sasa haamini kwenye kucheza na majukwaa kaamua kuruhusu service kunusuru mitambo ni lazima kuwe na upungufu wa umeme.

Tatizo la kimsingi ni kuwa tunazalisha umeme mdogo kuliko matumizi yetu na bahati mbaya yanaongezeka kila siku. Ingalikuwa tuna vyanzo vingi vya kuzalisha umeme basi hata kuzimwa kwa mtambo mmoja au 2 ili ifanyiwe service kusingekuwa na impact kubwa Sana kwenye upatikanaji wa umeme.

Kwa Hali ilivyo sasa hata umlete Malaika au Nani sijui awe MD wa Tanesco tutaendelea kupata mgao. Subiri masika Ije mabwawa yajae kuwe na umeme mwingi maisha yaendelee
We bwana majibu yako Yana mashaka Mashaka pale tanesco wewe ni nani?
Alafu tatizo la umeme ni mitambo kuchakaa au kupungua kwa maji!?

Alipokabidhiwa wizara ndugu January alisema wanafanya service badae kidogo akasema service imekamilika hautakatika tena!
Mara anakuja rais anatoa miezi 6 umeme usikatike tena
Mara anakuja mkurugenzi mpya anatuambia mgawo utaisha mwezi wa 3
 
Maandamano kama haya ndio ya Muhimu sio Yale ya Wanasiasa ya kupigania maslahi Yao Binafsi lakini kinapokuja suala la maslahi ya Wananchi wanakaa pembeni.

Wananchi rasilimali zao zinaporwa.
Bandari imegawiwa Wageni.
Misitu wamepewa Wageni.
Wanyama Wetu ni Mali ya Wageni.
Ardhi inagawiwa Wageni.
Upepo imejaa Kanda ya Kati Yote na joto la kutosha kuzalisha umeme.
Walipewa zaidi ya trion moja Kukarabati miundombinu ya umeme. Wakatuambia watazalisha nguzo za zege Badala yake wanatuletea nguzo za miti kama kawaida.
Nguvu kubwa waliyoweieza kwenye nguzo wangeweza kukamilisha bwawa la Mwalimu Nyerere.

Gesi IPO ya kumwaga kuna mgao Wa umeme .
Bado IPTL wapo kuna mgao Wa umeme.

Tatizo ni kwamba kuna watu na manyani.
Nyani Hawelawezi kuwatawala watu Bali watu wanaotawala manyani .

Nimemwelewa Yule mwimbaji ,Wanatuona Nyani.
Wanasiasa wametuzarau sana .

Leo VYAMA VYA UPINZANI HAWATAKI KUSHIRIKI MAANDAMANO YANAYOGUSA MAISHA YA WATANZANIA WOTE .
Wamesahau kuwa Kesho kwenye uchaguzi wataibiwa kura na Nguvu ya kuwapa ushindi ni maandamano ya Wananchi.

Ni vyema wapinzani wakajitafakari kuwa karibu na Wananchi kupigania maslahi ya Wananchi Ili Kesho wananchi nao waandamane kupigania ushindi Wa wapinzani.

Leo ukasema unaitisha maandamano ya Kudai Katiba Mpya huwezi kupata Watu wakati vijana wanaokosa vipato Kwenye saluni , stationary, vinywaji , nyama zinaoza Kwenye mabucha,Samaki zinaoza Kwenye mabucha , vyakula majumbani vinaoza , Viwanda vidogo vya kuchomea vyuma havifanyi kazi.Uzalishaji umedorora Kwa sababu hakuna umeme. Wajanja walihujumu Kila mbinu ya kuondoa tatizo la umeme Kwa manufaa yao.

Wapinzani jitokezeni kuungana na Wananchi Kwenye matatizo yanayogusa watanzania Wote leo.
Vyama vya Upinzani vimesahau kuwa miaka yote walikua wanashinda na kutangazwa Kwa nguvu ya MAANDAMANO ya Wananchi ?
Leo Chama kama Chadema kimesahau kuwa Wabunge wake wote walikua wanatangazwa Kwa MAANDAMANO ya Wananchi ?? Wananchi Hao Hao wanaotegemewa kuandamana kupigania ushindi Wa wabunge Wa Upinzani leo wanataka kuandamana Kupinga kuuzwa Kwa bandari zetu na rasilimali zetu Zote Kwa Wageni lakini Chadema imekaa pembeni Kwa hasira kuwa Wakati Wa MAGUFULI hawakuandamana .Lakini wanasahau KUWA MAGUFULI alikua ni kipenzi cha wananchi walio wengi. Kwa hiyo Kidemokrasia MAGUFULI alikua anaongoza Watu Kwa ajili ya Watu na Kwa faida ya Watu walio wengi.

Wapinzani mnaua wenyewe moyo Wa wananchi kuandamana matokeo yake Kesho mkihitaji MAANDAMANO yanayohusu siasa hawataandamana mana hayawagusi walio wengi moja Kwa moja.

Wakati Wa Magufuli miaka mitano hakuna tatizo la Umeme. Leo tatizo ni kubwa sana je, Magufuli alikua anazalidha Umeme.????
Jibu ni kwamba Wezi na wahuni hawatakiwi kupewa nafasi ya kupanga bila kusimamiwa.
Hotuba za MAGUFULI zinaonyesha wazi kuwa ni MTU aliyekua anajua michongo Yote iliyokua inafanywa na wahuni ndani ya mashirika ya umma na viongozi Wa Serikali.
Asichogundua Rais Wa Sasa Wa Bangladeshi ni kwamba Wabangladesh wanasimamiwa Kwa mtutu Wa Bunduki muda Wote na anayeharibu anapigwa hapo hapo Ili anayeingia afanye kazi Kwa uaminifu.
Haiwezekani uwape mwanya Wabangladesh wanaowaza kupata pesa za kulewa pombe Kila Siku wanapoingia Kazini. Yaani watumishi wangi wakifika ofisini wanawaza pesa za ziada za pombe na wanawake. Sasa Watu Kama Hao ni Lazima wasimamiwe Kwa Nguvu kubwa sana .
Ukija Mawaziri na wengineo wanawaza pesa za kuhongo Kwenye uchaguzi . Hawa wanatumia mashirika yaliyoko Kwenye wizara zao kama Sehemu ya madili Yao Kwa kufanya Kila hujuma alimradi watengeneze pesa Kwa ajili ya kuhonga Kwenye majimbo Yao na kuoneana Kama wafadhili Wa majimbo ya uchaguzi.

Aliyekuye kuwa Rais Wa Tanzania Hayato Magufuli alifanikiwa Kwa sababu alijua tabia za wahuni Kwa kiwango kikubwa na hakuwa na Rafiki Wa kudumu linapokuja suala la maslahi ya nchi.
 
Wamejivika uwezo, uwezo wa Rabuka,
Hawataki mafunzo, kuwa watashuka,
Shida uzipatazo, wao wanaufaika,
Tafuta kujikwamua, hakuna anayejali.
 
Back
Top Bottom