Nakuwa muwazi. Nashukuru, nilisaidiwa kumpata wa kunioa na rafiki yake mama

Nakuwa muwazi. Nashukuru, nilisaidiwa kumpata wa kunioa na rafiki yake mama

Kwahiyo unatowa ushuhuda, unaweza kuolewa na mwanaume yupo kawaida lakini mkatengeneza pamoja maisha kufikia ndoto zenu? Right?

Today generation wanataka ready made, unawashauri nini?
hili jambo liko wazi na tena hata ukweni utaheshimika....
HATA AKICHEPUKA ataficha sana usijue....hatapenda kukuumiza waziwazi
 
@Arusha,Mama mchagga (Mmaranguu), baba mngoni

Ndege mjanja hunaswa tundu bovu, baada ya kuchemka mwishowe nilisaidiwa kumpata wa kunioa 'Asante'
Mama aliwakataa wachumba zangu wawili, watatu alikuwa Mkibosho very handsome akisoma Uhandisi UDSM baba yake akiwa ni tajiri wa Hardware chains Arusha na Moshi. Mama alimkataa na akawaka kama mbogo na laana akatamka ‘Hata nife sitaki uolewe na mkibosho’

Kuna rafiki yake Mama akiitwa Mama Kavishe (Mchagga wa Rombo)akiwa Tour operator mdogo kipindi kile akanipigia simu, njoo mwanangu kuna zawadi nataka kukupa….Nilipofika akaniambia Marytina usitake kutuua mama zako kabla ya muda…”achana na huyo mkibosho” na tena naomba nikuchagulie mume….

Nikacheka…unichagulie, Ndio niruhusu nikuchagulie na hutajutia….na tunataka uolewe mapema kabla ya 23 years tupate mjukuu wa ndoa.Nakuchagulia mtu ambaye anaweza kuwa bora kwako na kwa familia. Nani huyo….nani huyo mama unataka niolewe naye..akanijibu LOTII, LOTII, LOTII…akaniambia waweza kwenda chukua funguo hamna dereva wa kukupeleka nyumban na hiyo CRUZA haiendi porini wiki ijayo nenda hata mjini (Nairobi) kajitafakari

Baada ya wiki nikarejesha gari na kukutana tena na Mama Kavishe…

Marytina: Mama alikuwa serious?

Mama Kavishe: Ndio na hata ningekuwa na binti wa kumzaa ningemwozesha LOTII,

Marytina :Lakini Mama mbona LOTII ni kama kaka yangu, na sikujua atajakuwa mpenzi wangu so mambo mengi nimemweka wazi tokea utoto? na Hajawahi kunitongoza?

Mama Kavishe : Koma na ukome…wewe Mngoni/Mchagga, LOTII Mmasai/Mmasai huo undugu uko wapi??? Hayo uliyomweka wazi ndio kinga yako kwenye huo uhusiano na tunajua anakupenda anakuheshimu ndio maana hawezi kukutongoza

Marytina: LOTII sasa mara ni mpishi, mara ni mbeba mizigo yupo yupo tu kwenye utalii bila profession sio tour guide, sio dereva, sio mpishi mwenye vyeti….kuna kipindi anakaa bila kazi miezi sita anakuwa kwao kijiweni ILBORU tutaishije mama? Ni form four tu hamna hata ndoto za kazi

Mama Kavishe: Kwa hiyo unampenda ila unakwama hapo….kwenye carrier & professionalism? We will help you to turn him around….step by step ila usimwambie hili. LOTII ana positive comments kwa kila aliyefanya nae kazi hata mimi nimefanya naye kazi kadhaa kwa uaminifu sana hivyo anaelekezeka

Marytina : Kwa hiyo ntamwanzaje wakati namheshimu, mbona kituko??? Na kama ana mtu tayari?

Mama Kavishe : Fanya uwezavyo kufanya ndani ya miezi mitatu nataka kuona ushahidi wa uwepo wa mahusiano …anzia kumpeleka DRIVING kama just rafiki na jirani…akijua nitampa CRUZA kama dereva, MKIFUNGA NDOA tutawapeleka UGANDA & KINSASHA, kisha SOUTH AMERICA, kwa kingereza , kifaransa na spaniola. Kisha German ….wewe nay eye mtakuwa Tour guides….the rest will be history ntajua mtakavyoendelea ila mkikwama tupo..

SASA HUYU LOTII NI NANI….

Utotoni nilipitia historia ngumu kidogo, tukiisha kama vitajiri miaka hiyo Arusha ILBORU, gafla baba, mjomba walitupwa korokoroni, Tukakimbilia Kenya (Mama na wadogo zangu wawili) baadae mama akakamatwa na kurejeshwa Tanzania kuunganishwa kwenye kesi .

Mama akaachiwa baada ya miaka mitatu, ila tayari dunia ilishaanza kunimeza kwan nililazimika kuwalea wadogo zangu mwenyewe (ingawa Mama alikuwa na hela nyingi benki) huku tukiendelea na Chuo na shule .Tulirejea TZ tukanunua nyumba njiro na mama alisema tusipende tembelea ILBORU.

Kuna siku nikaenda ILBORU….nikakutana na LOTII (mmasai, mvulana, jirani yetu, akisoma Lyamungo, akitumia muda mwingi tokea namfaham kushinda kwetu nyumbani ILBORU na nilimchukulia kama KAKA)…Akanikumbatia akalia akaniambia kwa nin tuliondoka bila kuaga hata kwa wazazi wake? Nilijaribu kumweleza akanielewa…

YAAN LEO MIMI NA LOTII NI MKE NA MUME NA WATOTO...TUKIZURURA KUSINI MWA JANGWA LOTE LA SAHARA TUTAKAVYO..asante mama KAVISHE,
Hongera kwa mama zako kwakuona mbele,na kukuelekeza Binti Yao.

Hongera kwa kupata mume mwema
 
Hongera kwa kumpata mume mwema katika maisha yako
Ilikuwa uamuzi mgumu sana ikifikiriwa bado nilikuwa mdogo na mashoshi wote walikuwa hawakubaliani na huo uamuzi wangu,
Namshukuru mama mzazi na mama kavishe....kwa kweli tulikuwa kundi la wasichana kama wanane na ni mimi tu niliye na ndoa tulivu, hao wengine single maza , wameachika na mmoja wanaishi ili mradi siku zisonge....
Sasa ingekuwaje mim na historia yangu ilivyo mbaya?
 
Ilikuwa uamuzi mgumu sana ikifikiriwa bado nilikuwa mdogo na mashoshi wote walikuwa hawakubaliani na huo uamuzi wangu,
Namshukuru mama mzazi na mama kavishe....kwa kweli tulikuwa kundi la wasichana kama wanane na ni mimi tu niliye na ndoa tulivu, hao wengine single maza , wameachika na mmoja wanaishi ili mradi siku zisonge....
Sasa ingekuwaje mim na historia yangu ilivyo mbaya?
Safi sana mama kavishe , kavishe ukoo mkubwa sana
 
Kuna kitu ni very serious kuhusu watu wa kibosho hasa kuoa na kuolewa, sana sana kuolewa.

Nimewahi kuwa nae binti mkibosho na wazazi wangu pamoja na watu wa karibu wakakataa kabisa kuingia kwny ndoa na huyo mkibosho.

Baada ya siku nyiingi mbele ikabidi nimshukuru Mungu kwa kutoingia kwenye ndoa na yule mkibosho.

Nilichogundua ni kwamba, watu wako wa karibu wale wanaokujua hasa wazazi, ndugu n.k sana sana watu wazima wenye ndoa zao na maisha yao, wakikwambia kitu huwa kwa 90% wapo sahihi.

Mungu atusaidie kwenye maamuzi ya kuoa wanaume na kwa wanawake pia.
yaan ni ujana tu ulitaka kuniponza....yule mkibosho mwanaume yupo Arusha na ni mlevi mlevi tu, sijui hata anakumbuka aliyosoma UDSM, yaan MUNGU alisema tuwasikilize wazazi hakukosea
 
Kuna fumbo kubwa pale wazazi wetu wa kwanza Adam na Hawa walipokosea kwa tamaa.

Mpaka leo hii tunateseka ktk maisha kutokana na tamaa, mambo mazuri yalojificha Mungu kuna namna ameyaweka ili umtafute ujue.

Shetani ili kutupoteza huwa analeta mazingira ya tamaa, ataleta watu, mali n.k ili utamani kisha akupige pingu.
TAMAA TAMAAA mbaya....kesho ya mtu aijuaye MUUMBA
 
.
Nakubaliana na wewe 100%, baada ya mambo yangu kuanza kwenda kombo, nikaanza kuzama zaidi kutafuta ukweli juu ya hawa watu, mpaka huku JF nikazama ndo nikagundua mengi zaidi zaidi.

Nilimpenda sana mkuu, sikuwahi kuwa serious ktk mahusiano kama ambavyo nilikuwa na yule binti, hakuna kitu ambacho alikosa ila ndo hivyo mkuu.
Ni bora kuvunja mahusiano mapema kila mtu Mungu atampa wa kufanana naye kuliko kuingia kwenye ndoa ambayo ni sawa na Jehenamu.

Sasa hapa naanza kuelewa kunawachaga wameowa wanawake wachaga wanaume wana pesa lakini hawawapi kipaumbele wake zao.

Kuna mmoja alianza kumuamini mke wake kariakoo ikatokea safari wakati anasafiri akapata dharura kurudi dukani akamkuta mke wake na kaka yake, wakati yeye akiwepo kaka mtu huwa haendi dukani kwao.

Yule jamaa sasa hivi ameamuwa mke wake akae nyumbani alee watoto swala kupanga kumuibia na ndugu zake hataki.
 
Bora wewe
Wenzio ni maskini lakini anataka mume tajiri badala atafute maskini mwenzie waishi
Inahitaji moyo sana....ukifikiria nilikuwa natongozwa na vijana wenye vihela vyao, ila nilikaa nikawaza mimi elimu sina, historia mbaya, uzuri utachuja....natakiwa nipate mwanaume atakayesimama na mimi kwelikweli
 
yaan ni ujana tu ulitaka kuniponza....yule mkibosho mwanaume yupo Arusha na ni mlevi mlevi tu, sijui hata anakumbuka aliyosoma UDSM, yaan MUNGU alisema tuwasikilize wazazi hakukosea
Ungesikiliza wazazi ungejuta, mabinti wengi ktk umri huo wana tabia ya kuchagua wanaume, ukifika umri wa 27 au 28 ndo wanaanza kushtuka. Hapo sasa wanaingia ndani ya ndoa ili wawe ndani ya ndoa.
 
Back
Top Bottom