Nakuwa muwazi. Nashukuru, nilisaidiwa kumpata wa kunioa na rafiki yake mama

Kwahiyo unatowa ushuhuda, unaweza kuolewa na mwanaume yupo kawaida lakini mkatengeneza pamoja maisha kufikia ndoto zenu? Right?

Today generation wanataka ready made, unawashauri nini?
hili jambo liko wazi na tena hata ukweni utaheshimika....
HATA AKICHEPUKA ataficha sana usijue....hatapenda kukuumiza waziwazi
 
Hongera kwa mama zako kwakuona mbele,na kukuelekeza Binti Yao.

Hongera kwa kupata mume mwema
 
Hongera kwa kumpata mume mwema katika maisha yako
Ilikuwa uamuzi mgumu sana ikifikiriwa bado nilikuwa mdogo na mashoshi wote walikuwa hawakubaliani na huo uamuzi wangu,
Namshukuru mama mzazi na mama kavishe....kwa kweli tulikuwa kundi la wasichana kama wanane na ni mimi tu niliye na ndoa tulivu, hao wengine single maza , wameachika na mmoja wanaishi ili mradi siku zisonge....
Sasa ingekuwaje mim na historia yangu ilivyo mbaya?
 
Safi sana mama kavishe , kavishe ukoo mkubwa sana
 
yaan ni ujana tu ulitaka kuniponza....yule mkibosho mwanaume yupo Arusha na ni mlevi mlevi tu, sijui hata anakumbuka aliyosoma UDSM, yaan MUNGU alisema tuwasikilize wazazi hakukosea
 
TAMAA TAMAAA mbaya....kesho ya mtu aijuaye MUUMBA
 
.
Ni bora kuvunja mahusiano mapema kila mtu Mungu atampa wa kufanana naye kuliko kuingia kwenye ndoa ambayo ni sawa na Jehenamu.

Sasa hapa naanza kuelewa kunawachaga wameowa wanawake wachaga wanaume wana pesa lakini hawawapi kipaumbele wake zao.

Kuna mmoja alianza kumuamini mke wake kariakoo ikatokea safari wakati anasafiri akapata dharura kurudi dukani akamkuta mke wake na kaka yake, wakati yeye akiwepo kaka mtu huwa haendi dukani kwao.

Yule jamaa sasa hivi ameamuwa mke wake akae nyumbani alee watoto swala kupanga kumuibia na ndugu zake hataki.
 
Bora wewe
Wenzio ni maskini lakini anataka mume tajiri badala atafute maskini mwenzie waishi
Inahitaji moyo sana....ukifikiria nilikuwa natongozwa na vijana wenye vihela vyao, ila nilikaa nikawaza mimi elimu sina, historia mbaya, uzuri utachuja....natakiwa nipate mwanaume atakayesimama na mimi kwelikweli
 
yaan ni ujana tu ulitaka kuniponza....yule mkibosho mwanaume yupo Arusha na ni mlevi mlevi tu, sijui hata anakumbuka aliyosoma UDSM, yaan MUNGU alisema tuwasikilize wazazi hakukosea
Ungesikiliza wazazi ungejuta, mabinti wengi ktk umri huo wana tabia ya kuchagua wanaume, ukifika umri wa 27 au 28 ndo wanaanza kushtuka. Hapo sasa wanaingia ndani ya ndoa ili wawe ndani ya ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…