Nalaani vikali DC MOSHI kukamata mafundi ujenzi site kisa wanajenga nyumba isiyokuwa na kibali cha ujenzi

Heshimu sheria za nchi, kutojua sheria ni upumbavu wako siyo udhuru. Km suala ni njaa kwanini hakwenda kuiba? Hili lilikuwa jukwaa la Great Thinkers limevamiwa na mazuzu. Sintashaanga kuona watakaomwunga mkono mleta uzi, limeshavamiwa km Ukraine
Sababu kubwa ya Tanzania kuwa na squatter nchi nzima ni watu kuwa na mawazo kama yako

Nchi nyingine haujengi tu kiholela ndo maana sehemu kubwa ya makazi ya watu Tanzania ni kubaya sana

ukienda nchi nyingine kama Europe, china, Japan, Korea unajiuliza hawa watu waliwezaje mbona miji Yao mizuri sana Waliwezaje kuwa na miji mizuri ni kwa sababu ya sheria Kali ya ujenzi ambayo huku Tanzania watu akiwemo mleta uzi hawataki kuifuata wanataka watu wajenge wanavyojisikia
 
Viongozi waliokosa exposure ndo matokeo yenyewe haya.

Unaokoteza watu unawapa uongozi wanaishia kukurupuka.
 
Sababu kubwa ya Tanzania kuwa na squatter nchi nzima ni watu kuwa na mawazo kama yako

Nchi nyingine haujengi tu kiholela ndo maana sehemu kubwa ya makazi ya watu Tanzania ni kubaya sana

ukienda nchi nyingine kama Europe, china, Japan, Korea unajiuliza hawa watu waliwezaje mbona miji Yao mizuri sana Waliwezaje kuwa na miji mizuri ni kwa sababu ya sheria Kali ya ujenzi ambayo huku Tanzania watu akiwemo mleta uzi hawataki kuifuata wanataka watu wajenge wanavyojisikia
Mleta uzi hajapinga uwepo wa sheria amehoji kukamatwa kwa watu wasiohusika na pia bei za vibali ambazo kiuhalisia haziko sahihi. Tumia akili yako kuelewa kinachoongelewa badala ya kujifanya kuelewa dunia inavyoendeshwa.

Haya mambo ya kuinflate gharama za kodi, ushuru na tozo yametapakaa kila sekta na malalamiko ni mengi ila hakuna anayechukua hatua.

Na kama wewe ni mpenzi sana wa sheria, mbona hausemi serikali iende kukagua vibali vya ujenzi huko squatters?
 
Pamoja na ukiritimba wa vibali vya ujenzi kuwa bei juu ukiambata na mazingira ya rushwa kuanzia wapimaji katika halimashauri nyingi Tanzania!

Lakini haiondoi haki na wajibu wa kila mtu!

Taratibu za ujenzi katika halmashauri zote zinataka mtu yoyote anayehitaji kufanya ujenzi Tanzania lazima;

1. Awe na michoro iliyoidhinishwa kutoka mchoraji aliyesajiliwa (registered architecture) gharama inaweza kua laki 3 hadi 1mil au zaidi
2. Malipo ya kibali cha ujenzi kila manispaa wana bei zake wanachaji kwa square meter kulingana na ukubwa wa eneo linalojengwa (building area) ambapo square mita moja inaweza kuwa (elf 2~10 au zai) hivyo kwa eneo la sq 400 hivyo unaweza kulipia vibali vya ujenzi laki nane au 1mil ili wakupatie building permit

3. Mbali na pesa hiyo bado kuna pesa ya maombi ambayo huwa fixed inaweza kuwa elfu 50 au zaidi etc

Anyway nisirefushe mada! Yote kwa yote hata kama sheria ni ngumu wamiliki wanalazimika kuzifuata kabla ya kujenga!

Mkuu wa wilaya wakiongozana na polisi wamekamata mafundi waliokuwa wakijenga kwenye nyumba iliyosimamishwa ujenzi kwa kutokuwa na vibali!

Swali! Anaetakiwa kukamatwa ni fundi au mmiliki?

What if kama mmiliki wa jengo aliwadanganya mafundi kwamba kila kitu kipo kashakamilisha?

Ni fundi gani na njaa hii atathubutu kumuuliza bosi vibali wakati kazi zenyewe za kusotea?

Unaanzaje kukamata mafundi wabangaizaji innocent na kuwasondeka kwenye difenda wakati jengo linamwenyewe, jengo lipo, mwenyekiti wa mtaa yupo, mjumbe yupo etc!

Cha ajabu kila fundi kaambiwa alipe laki nne ili aachiwe, wapo 15!

Kosa lao kwenda kujenga nyumba pasipo kumhoji bosi wao kibali cha ujenzi!

Waziri Tamisemi mh Bashungwa, na Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu,kazi, Ajira vijana wazee na wenye ulemavu shughulikieni mapema jambo hilo, DC na mkurugenzi hawana hekima!

Rais ikimpendeza fukuza hao ili nao watoke ofisini waone maisha yalivyo magumu kwa wabeba zege

AJIRA ngumu
Kiburi chako ndo kikekuponza,
Kopi za Vibali wanakuaga navyo mafundi
Hilo jengo lishaonyeshwa Hadi na Mwewe wa Clouds kuhusiana na ukaidi huohuo lakin bado,
Upigwe tu namie nasema mpigwe tu maana hakuna namna
 
Huu ujinga niliwahi kumshikia panga Mtu wa ardhi na hakurudi tena. Nimejichanga nimenunua kiwanja Kwa kudunduliza, nimetafuta ramani Kwa wachoraji wanaotaka Kwa 3.5k, nakwenda ardhi kuomba kibali napigiwa hesabu zaidi ya laki 4, nikaona huu Sasa ni ujinga, nikaenda kujenga ili kama ni hasara nipate tu wakivunja. Nimeinua ukuta usawa wa madirisha anakuja kiherehere toka ardhi eti simamisha ujenzi nionyeshe kibali. Sikutoka Musoma kama Mtalii. Namshukuru alinifundisha kuwa Msimamizi wa Muda wote wa ujenzi. Maana wengine walioniletea ujinga ni Watu wa misitu àmbao baada ya kupiga kenchi naelekea kuezeka wananiambia mbao nilizotumia hazijagongwa mhuri. Aisee Acha niishie hapa.
Nakumbuka nilikwambia shusha hzo mbao zote uzilete ofisin Kwa galama zako,,[emoji1787]
 
Kiburi chako ndo kikekuponza,
Kopi za Vibali wanakuaga navyo mafundi
Hilo jengo lishaonyeshwa Hadi na Mwewe wa Clouds kuhusiana na ukaidi huohuo lakin bado,
Upigwe tu namie nasema mpigwe tu maana hakuna namna
Sasa fundi kibarua anahusikaje wewe!? Kwani mwenyewe hayupo?
 
Heshimu sheria za nchi, kutojua sheria ni upumbavu wako siyo udhuru. Km suala ni njaa kwanini hakwenda kuiba? Hili lilikuwa jukwaa la Great Thinkers limevamiwa na mazuzu. Sintashaanga kuona watakaomwunga mkono mleta uzi, limeshavamiwa km Ukraine
Anaemkamata mwenyewe aliiba kura ili apate uongozi! Hiyo sheria gan ya kuumiza wasiokuwa na hatia!
Wapunguze gharama za vibali vya ujenzi ili kila mtanzania atamani kuwa na kibali!

Kuna kodi ya ardhi, kodi ya jengo, n.k vibali havitakiwi hata kuzidi elfu hamsini.

Yote Tisa, sasa kwanini wasimkamate mmiliki, wanakimbilia kukamata vibarua ambao hawajui hata mbambambamba yoyote?
 
Employee Liability,,,
 
Mafundi wanajua utaratibu huo

Dereva kapakie Mzigo usioujua usafirishe wakati ni bangi uone
Gari inaendeshwa na dereva mwenye leseni!
Mfano wako hauna tija!.
Kibarua na mbeba zege hana leseni ! Yeye anaitwa tu ili apate ugali,
Anawajibishwaje kwa wajibu wa mmiliki wa jengo?
Kama mwenye jengo alikaidi wanashindwaje kupiga greda nyumba?
 
Sababu kubwa ya Tanzania kuwa na squatter nchi nzima ni watu kuwa na mawazo kama yako

Nchi nyingine haujengi tu kiholela ndo maana sehemu kubwa ya makazi ya watu Tanzania ni kubaya sana

ukienda nchi nyingine kama Europe, china, Japan, Korea unajiuliza hawa watu waliwezaje mbona miji Yao mizuri sana Waliwezaje kuwa na miji mizuri ni kwa sababu ya sheria Kali ya ujenzi ambayo huku Tanzania watu akiwemo mleta uzi hawataki kuifuata wanataka watu wajenge wanavyojisikia
Kama viwanja vimepimwa na michoro ipo serikali ya kijiji na copy ziko ardhi hio squatter inatoka wapi??? Tatizo la Tanzania ni kugeuza sheria Kama chanzo cha mapato na ndo maana rushwa haiishi nchi hii!
 
Kabisa mkuu! Sheria zinakuwa hazitekelezeki kwasababu ni za kukomoana!
Kuna sababu gani vibali kuwa bei juu namna hiyo!
 
Pamoja na ukiritimba wa vibali vya ujenzi kuwa bei juu ukiambata na mazingira ya rushwa kuanzia wapimaji katika halimashauri nyingi Tanzania!

Lakini haiondoi haki na wajibu wa kila mtu!

Taratibu za ujenzi katika halmashauri zote zinataka mtu yoyote anayehitaji kufanya ujenzi Tanzania lazima;

1. Awe na michoro iliyoidhinishwa kutoka mchoraji aliyesajiliwa (registered architecture) gharama inaweza kua laki 3 hadi 1mil au zaidi
2. Malipo ya kibali cha ujenzi kila manispaa wana bei zake wanachaji kwa square meter kulingana na ukubwa wa eneo linalojengwa (building area) ambapo square mita moja inaweza kuwa (elf 2~10 au zai) hivyo kwa eneo la sq 400 hivyo unaweza kulipia vibali vya ujenzi laki nane au 1mil ili wakupatie building permit

3. Mbali na pesa hiyo bado kuna pesa ya maombi ambayo huwa fixed inaweza kuwa elfu 50 au zaidi etc

Anyway nisirefushe mada! Yote kwa yote hata kama sheria ni ngumu wamiliki wanalazimika kuzifuata kabla ya kujenga!

Mkuu wa wilaya wakiongozana na polisi wamekamata mafundi waliokuwa wakijenga kwenye nyumba iliyosimamishwa ujenzi kwa kutokuwa na vibali!

Swali! Anaetakiwa kukamatwa ni fundi au mmiliki?

What if kama mmiliki wa jengo aliwadanganya mafundi kwamba kila kitu kipo kashakamilisha?

Ni fundi gani na njaa hii atathubutu kumuuliza bosi vibali wakati kazi zenyewe za kusotea?

Unaanzaje kukamata mafundi wabangaizaji innocent na kuwasondeka kwenye difenda wakati jengo linamwenyewe, jengo lipo, mwenyekiti wa mtaa yupo, mjumbe yupo etc!

Cha ajabu kila fundi kaambiwa alipe laki nne ili aachiwe, wapo 15!

Kosa lao kwenda kujenga nyumba pasipo kumhoji bosi wao kibali cha ujenzi!

Waziri Tamisemi mh Bashungwa, na Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu,kazi, Ajira vijana wazee na wenye ulemavu shughulikieni mapema jambo hilo, DC na mkurugenzi hawana hekima!

Rais ikimpendeza fukuza hao ili nao watoke ofisini waone maisha yalivyo magumu kwa wabeba zege

AJIRA ngumu
mambo haya ya vibali,ramani yangefutwa tu ili watu wawe huru kujenga kwa ramani waitakayo.Mlolongo wote huo ukikamilika nadhani masikini mwenye m2 yakujenga hela yote inaishia kwenye vibali hawezi kujenga.
 
Msingi wa vibali ilikuwa na lengo la kuupanga mji lakini utekelezaji wake umegeuzwa chanzo cha mapato
 
Back
Top Bottom