Nalalamikiwa, nimfanyie nini mpenzi wangu zaidi ya haya?

Nalalamikiwa, nimfanyie nini mpenzi wangu zaidi ya haya?

Sisi waislamu katika dini yetu inasema kazi ya mwanamke ni moja tu,mengine ni mume, lakini mtume wetu muhammad (s.a.w) amewaasa Wanawake kuwafanyia ihsani kama yako,na malipo mbele ya mungu ni makubwa mno, m/ ke unapo kuwa kwa wazee pepo yako iko chini yao, na unapo kuwa kwa mume ipo chini ya nyayo za mume.
Kila unapo mfanyia mazuri mume barka huwa ni kubwa na always munakuwa watu wenye furaha na mafanikio, katika maisha ya ndoa kuna mambo mawili ambayo yanaweza kuwabadilisha kimaisha.
Mwanamke anaweza kumfanya mume awe tajiri au uwezo mzuri tu au kutoka hali alio nayo na ku improve zaidi.
La pili mwanamke anaweza kumfanya mume kuwa fukara na maskini.
Na hivi ni vitu vya ukweli kabisa, tumeamrishwa kuowa wake wazuri wenye dini,huruma na mapenzi, tumeamrishwa tuzae na tusiogope umasikini, kwani Allah subhana Wataala ndio mtowaji rizki. I believe in God.
Tufanyie mazuri zaidi mupate malipo na sisi tupate mafanikio na malipo.
 
Na mimi nimewaza pia,nikasema anyway,acha nisimtie kihoro bibie ES,shem anataka kutumia ile kanuni"ukitaka kumuua mbwa wako mpe jina baya" nimewaza tu.

Hayo ya michepuko enzi hizi mbona ni kawaida ndugu, kuna cha kihoro basi...
 
Kwakweli kwa mtazamo wangu, naona roles zako km mama unazitekeleza vizuri tu tena unaenda extra extra miles; hongera sana sana kwa hilo km ni kweli. kitu ninachokushauri, endelea hivyo hivyo. Km mmeo ataendelea na vijimalalamiko vyake despite all the efforts unazomfanyie mi nafukiri uignore. Kwa mtazamo wangu; sioni sababu umfulie mwanaume boxer, umwekee maji, umpigie nguo pasi...?!!!, hell no.., i m doing it my self. Mambo mengine ni mambo ya kiswahili jamani hayana tija...mwanaume unanawishwa mikono!!!? Hou ni zaidi ya umwinyi enzi zile za 18 Centuary.
Wala sio umwinyi ni wajibu, mapenzi na heshima
 
Mbwa mzee kujifunza mbinu mpya hili nalo tatizo tena tatizo kubwa.

Huwa naona real men The Boss akiwa among wanasema mwanaume anahitaji mambo matatu: food, sex and space.

Katika hayo mambo kwakweli am doing the best inawezekana kabisa nina mapungufu yangu ila am doing the best kwakweli, food, napika japo sio bonge moja la mpishi kama farkhina but I cook tena delicious ones, sex hii si kuwa tu ni wajibu ila ni hobby yangu kitu ikiwa hobby kifuatacho itv ni known kabisa, space hapa kidogo pananishinda japo najitahidi ila sio kwa fungulia doggy, anaechungwa ni mbuzi kwa binadamu tunafanya kukaba tu japo kukaba kwenyewe ni kulinda bahari ila hivo hivo tu almradi kuna kibao "Punguza mwendo kazi inaendelea mbele" tunapunguziana speed natoa space kwa kiasi Chake may be majukumu yakinizidi itakua zaidi ya hapo.

Apart from hivo vitatu nafanya na mengineyo mengi napika mwenyewe simuachii dada wa kazi, mezani naweka mwenyewe kumake sure kila kitu kipo sawa, nguo nasaidiwa kufua ila boxa nafua mwenyewe, nanyoosha mwenyewe, asubuhi naanda maji ya moto napeleka bafuni (bafu halina heater) muda huo nshaweka nguo za kazini standby na viatu nimebrush kabisa mara chache naandaa Chai sio kila siku kwasababu ni mvivu kula BADILI TABIA bila shaka unanishangaa sana make haya mambo hautajagi ha ha ha nishangae tu ukinishangaa nami na kushangaa.

Swala la heshima na kujali nikijifanyia assessment najiona nina 99%,i do respect him much, much kwakweli nikijilinganisha na ndugu, jamaa na rafiki am the best, naweza kuwavisit katikati ya maongezi mara wachambane na waume zao mara wawafokee kitu ambacho mi huwa nashangaa unawezaje kumchamba mmeo au kumfokea mbele za watu mmh sijawahi na sitakaa nithubutu nikikereka nangoja tukiwa wawili nikiona nachelewa kutoa dukuduku naandika meseji.

Kuna shost angu alishawahi kunitembelea akaishia kunishangaa inakuaje nanyoosha nguo za baby dady yeye wanaishi wote ila hajawahi kumfulia wala kumnyooshea nikamshangaa pia na kuzidi kujiona am the best mie ni "mwanamke" hizi huduma nazionaga kwa wamana watu wazima ndo wanawalea waume zao ila mie kwa age yangu tu hii najiona nipo kama mama lowasa ha ha .

Point yangu what else should I do? Pamoja na kujiona mwanamke, najiona kama mama Lowassa ila bado nalalamikiwa jamani wanaume zaidi ya haya kunakuna yapi tena?au ni human nature tu kwamba hatunaga kuridhika? Au kunanii?

HIVI FORM FOUR M'SHAMALIZA PEPA Au BADO??
 
Dhaaaa!! Kwakweli uko vzr kwa yote hayo unayomfanyia nataman nimpate mwanamke km ww
 
Dhaaaa!! Kwakweli uko vzr kwa yote hayo unayomfanyia nataman nimpate mwanamke km ww
Teh Teh mapenzi sasa sio tanga tuu...hata kwa kina bukwimba yapo...tanga ni mbwembwe tuu...
 
Hahaha Sishangai hawa viumbe hata ufanye nini bado hautakuwa perfect. Your doing your best mengineyo akilalamika we sema am sorry then fanya
 
Hebu jaribu kumshirikisha Mungu ktk hilo kama ni wa kwako kweli, naamini atanadilika tu.
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1447940419.991869.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1447940419.991869.jpg
    24.4 KB · Views: 121
Nshaandaa nondo za kutosha, tight ya kuvaa kesho nshaiandika majibu.... Vipi we umejiandaaje?

Mnapanga ratiba za kukutana au ndo kama kuku mkicharuka tu hata wkt mnakula tayari? haahaahaaa!! ni muhm sana wee *evelyn salt* kupanga ratiba ili hata mwili unakua na maandalizi mazr
 
Alishawahi kukueleza kuwa hayo ndiyo anayoyataka?

You might be pressing a wrong button, halafu unajiona unajituuuma kama Mess...lol!

mada imepita muda lakini ndo nimepata leo muda wa kurudi. Swali lako limenikumbusha kitu nilichojifunza kwenye mahusiano yangu na mtoto. Katika kuwa mama kuna wakati nilikuwa nikiona kitu kizuri kwangu nakinunua wakati mwingine kwa gharama kubwa nampeleka mtoto nikitarajia naye atakiona ni kizuri na atafurahi sana. Mara nyingi alikuwa hafurahi kiasi cha kuweza kutuliza kiherehere cha moyo wangu. Anasema asante, anaipeleka chumbani anaendelea na mambo yake. Basi napata huzuni au nanung'unika kwamba hajali jinsi nilivyojinyima ili kumpatia kile kitu. Unamnunulia nguo bei kubwa unakuta yeye anapenda kuivaa anapoenda kucheza, na ile uliyomnunulia elfu 3 kwa ajili ya kuchezea yeye ndo anaipenda sana na anataka aivae karibia kwenye kila tukio analolithamini.

Mtoto huyo huyo ninayenung'unika kuwa hathamini mahangaiko yangu nikimnunulia pipi, popcorn, rangi za kuchorea au kumpeleka matembezi anafurahi sana na anashukuru sana . Kuna wakati nikajiuliza hivi huyu ana kichaa au? With time nikajifunza kuna mambo tunawafanyia wapendwa wetu kwa ajili yetu, na kuna tunayowafanyia kwa ajili yao. Kumnunulia nguo laki 1 badala ya elfu 20 ni mapenzi yangu na kiherehere changu binafsi - nataka apendeze, najiskia fahari mimi mwenyewe kuona bidii yangu kwenye mwili wake lakini hawajibiki kuninyenyekea na kunishukuru saaana. Ile "tenda wema uende zako" inaingia hapa. Nitende wema kwa ajili ya wema. Nikitaka kumfurahisha, nasema leo nataka nimfurahishe mtoto basi nachagua nimfanyie nini katika yale mambo ambayo with time nimegundua yanamfurahisha, mfano, kumpikia chakula anachopenda sana, kumnunulia tu pipi au choklet anayopenda au kumpeleka kwenye maeneo ya mitoko ya watoto anayoyapenda. Kama hii kanuni inafanya kazi kwa mtoto basi hata kwa watu wazima inafanya kazi hivyo hivyo kwani mtoto ndo picha halisi ya binadamu.
 
Sifanyi kwa kujihami, kufata kanuni wala nini naona hayo ni majukumu yangu na ni wajibu wangu kuyatekeleza that's all
Sasa dada kauli kama hii ndo inanichanganya. Sasa kama unajua ni majukumu na wajibu wako unalalamika nini? Umesahau kawaida hujenga sheria na hakuna excuse ya kuvunja sheria? Just be you. We shukuru tu kuwa hata unapika, unaweka mezani na kinaliwa. Wapo wenzio humu wameenda mpaka shule za mapishi lakini waume hawakamatiki. Vyakula vinawekwa mezani, mume anaingia home saa 7 usiku au harudi kabisa na siku akiwahi anakitoa kasoro halafu anaenda kulala. Jifunze kuhesabu baraka, hayo mengine potezea. Malaika utampata wapi?
 
Teh gelofriend bila shaka hata ye ukimuuliza anaweza kua hajui may be nikupe kamfano kadunchu jana mchana mida ya kula nimemnawisha mikono nikampakulia akaanza kula mara kidume cha mbegu kinazunguka pale (our son) nikamchukua kumlisha daddy kamaliza kula mie namlisha mtoto akaanza kunawa mwenyewe eeh nkashangaa analalamika kuwa anajinawisha mwenyewe simhudumii au nlitakiwa nimuache kidume cha mbegu nimnawishe? Maisha ni magumu mweh.... Kuna vitu vidunchu ila vinaumizaga kichwa unaweza hata usilale unakiwaza tu japo kidogo

Hongeraaaa.. Jembe la wife...May be human nature
 
mada imepita muda lakini ndo nimepata leo muda wa kurudi. Swali lako limenikumbusha kitu nilichojifunza kwenye mahusiano yangu na mtoto. Katika kuwa mama kuna wakati nilikuwa nikiona kitu kizuri kwangu nakinunua wakati mwingine kwa gharama kubwa nampeleka mtoto nikitarajia naye atakiona ni kizuri na atafurahi sana. Mara nyingi alikuwa hafurahi kiasi cha kuweza kutuliza kiherehere cha moyo wangu. Anasema asante, anaipeleka chumbani anaendelea na mambo yake. Basi napata huzuni au nanung'unika kwamba hajali jinsi nilivyojinyima ili kumpatia kile kitu. Unamnunulia nguo bei kubwa unakuta yeye anapenda kuivaa anapoenda kucheza, na ile uliyomnunulia elfu 3 kwa ajili ya kuchezea yeye ndo anaipenda sana na anataka aivae karibia kwenye kila tukio analolithamini.

Mtoto huyo huyo ninayenung'unika kuwa hathamini mahangaiko yangu nikimnunulia pipi, popcorn, rangi za kuchorea au kumpeleka matembezi anafurahi sana na anashukuru sana . Kuna wakati nikajiuliza hivi huyu ana kichaa au? With time nikajifunza kuna mambo tunawafanyia wapendwa wetu kwa ajili yetu, na kuna tunayowafanyia kwa ajili yao. Kumnunulia nguo laki 1 badala ya elfu 20 ni mapenzi yangu na kiherehere changu binafsi - nataka apendeze, najiskia fahari mimi mwenyewe kuona bidii yangu kwenye mwili wake lakini hawajibiki kuninyenyekea na kunishukuru saaana. Ile "tenda wema uende zako" inaingia hapa. Nitende wema kwa ajili ya wema. Nikitaka kumfurahisha, nasema leo nataka nimfurahishe mtoto basi nachagua nimfanyie nini katika yale mambo ambayo with time nimegundua yanamfurahisha, mfano, kumpikia chakula anachopenda sana, kumnunulia tu pipi au choklet anayopenda au kumpeleka kwenye maeneo ya mitoko ya watoto anayoyapenda. Kama hii kanuni inafanya kazi kwa mtoto basi hata kwa watu wazima inafanya kazi hivyo hivyo kwani mtoto ndo picha halisi ya binadamu.

Nimejitahid kukuelewa my sis, but mwisho wa siku hakuna kitu kizuri kama mtu kuwa na moyo wa shukrani. Sawa kuna Vitu tunavyovifanya kwa ajili ya wenzi wetu na wenyewe wala wasivifurahie. Na kuna Vitu unajua kabisa nikikifanya hiki mwenzangu atafurahi. Angalau tu Ukiona Tabasamu lake inakupa furaha hata kama Hajasema Ahsante. Sasa mtu ambaye haoni hata jema moja akashukuru ni mtu wa aina gani? Ndo maana tunaambiwa mtoto mfundishe haya maneno tangu akiwa mdogo " Ahsante, samahani, pole". Kuna muda mtoto ukimpa Pipi anasema Ahsante, sembuse mtu mzima bana. Maisha yenyewe yalivyo busy haya ukimpata mke wa hivi si unashukuru

Sasa dada kauli kama hii ndo inanichanganya. Sasa kama unajua ni majukumu na wajibu wako unalalamika nini? Umesahau kawaida hujenga sheria na hakuna excuse ya kuvunja sheria? Just be you. We shukuru tu kuwa hata unapika, unaweka mezani na kinaliwa. Wapo wenzio humu wameenda mpaka shule za mapishi lakini waume hawakamatiki. Vyakula vinawekwa mezani, mume anaingia home saa 7 usiku au harudi kabisa na siku akiwahi anakitoa kasoro halafu anaenda kulala. Jifunze kuhesabu baraka, hayo mengine potezea. Malaika utampata wapi?

Tatizo naloliona si kwamba anamlazimisha kumshukuru, tatizo ni kwamba kwa nini analalamika na kipi haswa anachokilalamikia wakati mtu anajitahidi kutimiza majukumu yake yote na zaidi? It's better hata kama angekuwa hasemi Ahsante ila tu asilalamike pasipo sababu. Analalamikia kitu gani kisichojulikana? Ndo swali hapo
 
Back
Top Bottom