Nalazimishwa kumuoa binti niliyemzalisha lakini nimegoma. Sheria za nchi zinasemaje?

Nalazimishwa kumuoa binti niliyemzalisha lakini nimegoma. Sheria za nchi zinasemaje?

Imetokea kuna binti 21 yrs, nilikuwa napunguza naye upwiru (siyo mchumba), akapata mimba na kujifungua mtoto. Wazazi wake hawanijui hata chembe maana miji (, hometowns) yetu ni tofauti na iko mbalimbali lkn binti kanitaja kwao kuwa mimi ndiye mhusika.

Sasa Jana jioni, baada tu ya mtoto kutimiza miezi 2 baba wa binti kamtimua na kumtaka binti yake aje aishi nami niliyempachika mimba.

Baada ya tafakuri pana na mshikaji wangu wa karibu tukaukwepa mtego huo. Maswali yalikuwa haya:-

1. Kwao hatupajui na ndugu zake hatuwajui, huyu binti akifa je?
2. Itakuwa vipi endapo wazazi wake watatóa taarifa polisi kuwa binti yao kapotea? Nani atatuelewa?

Tukaamua kuwa " kwa kuwa kurudi kwao haiwezekani kutokana na umbali, tutoe taarifa kwa mjumbe na alale kwa mjumbe, halafu kesho yake ageuze kurudi kwao. Tukafanya hivyo na asubuhi akapewa nauli na hela ya kula kisha akapandishwa gari.

Je, wadau mpk hapa niko salama? Sheria zinasemaje kuhusu kuzaa na mtu vs kumuoa? Mzazi huyu (baba wa binti) siwezi kumshitaki kwa kitendo alichofanya na kunisababishia usumbufu?
Watu kama nyie ni wa kutupa tu hamna faida yoyote kwa taifa.
 
Kisheria hautafungwa ila utaamliwa ku-provide makazi na matunzo ya mama na mtoto. Kiubinadamu kama una uhakika mtoto ni wako na uyo binti hana dosari za kitabia yaani anafaa kuwa mke we mpokee anzisha nae kaya yako. N8mejaribu kuvaa viatu vya uyo binti nimepatwa na huzuni sana. Kwao kafukuzwa aliemtia mimba kamlaza kwa mjumbe dah.! Uyo binti angekua mdogo angu kwa kweli nisingekuacha salama ungetujua vizuri wajaluo ni watu wa aina gani.
Huyu ni wewe uliyeandika au kuna mtu kakupokonya simu anatumia? Tangu lini umeanza kuwaonea huruma wanawake?
 
Back
Top Bottom