Nalinganisha Vyama vya SIASA Nchini Tanzania na Mitandao ya Simu

Nalinganisha Vyama vya SIASA Nchini Tanzania na Mitandao ya Simu

DidYouKnow

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2019
Posts
1,229
Reaction score
1,950
Chama cha Mapinduzi wanafanana sana na Vodacom, wanaweza kukuibia kifurushi chako hivihivi ukiangalia. Hakika wao ni chama kubwa, wenye sera nzuri lakini zilizopo kwenye makaratasi, ambazo hawajaweza zitekeleza hata kwa asilimia 10 toka tupate Uhuru. CCM wamejisahau, ila wajifunze kwa Nokia

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanafanana na Tigo Tanzania na Airtel, kila siku wanafuatia kwa ukubwa, kubadirisha imani za chama chao, wana sera nzuri sana, ila kila siku bado ni wadogo kwa CCM, wajifunze kwa Samsung.

ACT-Wazalendo wana ndoto kubwa sana ambazo ukweli zinapaswa zikue taratibu, mojawapo ya ndoto yao ni kujenga Taifa lenye kujitegemea kiuchumi. Wanajua sana kuandika. Kila siku wanataka waonekane wao ni chama cha upinzani mbadala, hapo ndio shida yao, hawataki kuwa wapinzani, ila wanataka kuonesha ni wapinzani wa mpinzani mkuu. Siwaoni wakikua mioyoni mwa Watanzania. Wanafanana na Zantel ilipotokea Zanzibar - pamoja na huduma nzuri hasa za internet na gharama nafuu za maongezi, hawakuweza kutoboa bara.

Mwanasiasa anayetaka kung'ara kwenye Siasa itamfaa kuwa CCM au CHADEMA lakini ile itakayorudia misingi yake ya awali.
 
Back
Top Bottom