Nalipenda sana Jeshi langu la JWTZ ila nilichokiona jana pale TPDF Golf Club getini kabisa hakikuwa cha kiungwana

Ilikuwa ni mida ya Saa 5 asubuhi kuelekea Saa 6 mchana ambapo Mzukulu nilikuwa napita zangu ndipo nikashikwa na butwaa hadi Masikitiko makubwa baada ya kuona Kijana (nadhani alikuwa nae ni Askari) akiwa amelazwa chini katika Geti la Kuingilia TPDF Golf Club huku amebebeshwa bonge la chuma na Kuambiwa alinyanyue juu huku anayemwambia hivyo akiwa anafagia zake taratibu Kuzunguka kile Kibanda cha Walinzi.

Sikatai na wala sipingani na utaratibu wa JWTZ (TPDF) katika kuwaadabisha kwa kuwapa Adhabu Maaskari (Wanajeshi) wao kwani najua ni kitu cha kawaida Kwao na kwa Majeshi mengi duniani ila kilichonisikitisha Mimi ni Mazingira husika ya tukio lenyewe ambapo kwa uelewa wangu (na hapa nakaribisha kukosolewa) nadhani halikuwa na uungwana na ni kama vile lilikuwa la kukomoa vile.

Kwanza Mhusika alikuwa akihenyeshwa hivyo Getini kabisa (tena Geti Kuu) la Kuingilia TPDF Golf Club halafu katika Kuonyesha kuwa mtoa hiyo adhabu alikuwa na lake jambo alikuwa kama akiona wanaopita nje (Raia) ni wanaume alikuwa anamwambia ainue lile chuma na atulie nalo tuli lakini akiona tu raia wanaopita nje ni akina dada basi Mtoa adhabu ndiyo alikuwa anapata Morali (Moto) wa kumuamrisha na kumuadabisha yule askari kiasi kwamba nilijisikia vibaya mno.

Hivi huyo mtoa adhabu alishindwa nini kumuadhibu yule Afande sehemu nyingine ambayo wangekuwa wao wawili tu au kule nyuma ambako watu huwa hawapiti ili aweze kumuhenyesha vizuri kuliko kuja kumhenyesha askari pale getini kabisa ambako kila mtu alikuwa akimuona (hasa Sisi Raia) akina Mzukulu kiasi kwamba nahisi yule afande mhenyeshwaji alijisikia vibaya sana?

Na sijui yule askari aliyekuwa akihenyeshwa vile alifanya nini masikini ya Mungu. Kweli cha moto askari kakiona na kakoma!
Kwanza umesema hauna uhakika kama ni askari,lakini ulivoendelea ni kama umethibitisha tayari ni askari,vipi kama ni raia tu? Mimi naona ya Ngoswe tumuachie Ngoswe tu mkuu.
NB; Next time jaribu kumuuliza mtoa adhabu ili uje na story kamili mkuu (joking ).
macson
 
Mwanaharakati wa mitandaoni... We ni keyboard na dole gumba tu.

Umeshindwa kumchana kamanda aache ile tabia, unamuacha unakuja kutuchana sisi.. Sasa si tunafanya vipi mkuu!???

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaaaa angemchana huyo afande sidhani hata angepata nguvu ya kupost huu umbea
 
Ilikuwa ni mida ya Saa 5 asubuhi kuelekea Saa 6 mchana ambapo Mzukulu nilikuwa napita zangu ndipo nikashikwa na butwaa hadi Masikitiko makubwa baada ya kuona Kijana (nadhani alikuwa nae ni Askari) akiwa amelazwa chini katika Geti la Kuingilia TPDF Golf Club huku amebebeshwa bonge la chuma na Kuambiwa alinyanyue juu huku anayemwambia hivyo akiwa anafagia zake taratibu Kuzunguka kile Kibanda cha Walinzi.

Sikatai na wala sipingani na utaratibu wa JWTZ (TPDF) katika kuwaadabisha kwa kuwapa Adhabu Maaskari (Wanajeshi) wao kwani najua ni kitu cha kawaida Kwao na kwa Majeshi mengi duniani ila kilichonisikitisha Mimi ni Mazingira husika ya tukio lenyewe ambapo kwa uelewa wangu (na hapa nakaribisha kukosolewa) nadhani halikuwa na uungwana na ni kama vile lilikuwa la kukomoa vile.

Kwanza Mhusika alikuwa akihenyeshwa hivyo Getini kabisa (tena Geti Kuu) la Kuingilia TPDF Golf Club halafu katika Kuonyesha kuwa mtoa hiyo adhabu alikuwa na lake jambo alikuwa kama akiona wanaopita nje (Raia) ni wanaume alikuwa anamwambia ainue lile chuma na atulie nalo tuli lakini akiona tu raia wanaopita nje ni akina dada basi Mtoa adhabu ndiyo alikuwa anapata Morali (Moto) wa kumuamrisha na kumuadabisha yule askari kiasi kwamba nilijisikia vibaya mno.

Hivi huyo mtoa adhabu alishindwa nini kumuadhibu yule Afande sehemu nyingine ambayo wangekuwa wao wawili tu au kule nyuma ambako watu huwa hawapiti ili aweze kumuhenyesha vizuri kuliko kuja kumhenyesha askari pale getini kabisa ambako kila mtu alikuwa akimuona (hasa Sisi Raia) akina Mzukulu kiasi kwamba nahisi yule afande mhenyeshwaji alijisikia vibaya sana?

Na sijui yule askari aliyekuwa akihenyeshwa vile alifanya nini masikini ya Mungu. Kweli cha moto askari kakiona na kakoma!
Teh teh mtoa mada atakua ni yeye sema amekuja kwa gia ya mpita njia
 
Haa unafrahisha mkuu
Acheni kutufunga kamba hapa unajua raia tunadanganywa sana,,zamani tulikuwa tunaambiwa mwanamke aruhusiwi kuwa mwanajeshi kumbe uongo mtupu,,,Mara ooh wanajeshi 2 wanaweza kubeba gari kumbe ujinga mtupu,,Mara oooh wanajeshi wanajua ngumi wakati wanachapwa kila siku na raia... Mdogo wangu ni askari yuko jeshini huko lkn sioni kama ana dalili za kunimudu hata dk 2 kwenye ngumu,,,wapo wengi tu huko hawana lolote zaidi ya kuvaa baka baka tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kweli ,jeshi ni akili na maarifa,hiyo ya nguvu ni majeshi yale MIAKA YA 47
Afande mbona mnatuoneshaga mabavu sisi RAIA tuwaogope kuliko kutumia akili rejea hoja ya mleta mada au kwenye sherehe za Uhuru mambo ya kuvunja matofari....mbao.
 
Nilishaendaga sana pale Jkt Mgulani,mbona wajeda wa mule ndani wako peace sana ama kwa kuwa ndani mule kuna huduma za kijamii kama shule ya Jitegemee,chuo cha ufundi na shule ya driving school,Nilikuwa naingiaga mule nazurura vile nitakavyo
 
Back
Top Bottom