Uchaguzi 2020 Nalitamani jimbo la Arusha mjini,ni wakati wa vijana wachapa kazi

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
Haja yangu ni kuliona jimbo la Arusha mjini likiwa Geneva ya kweli ya Afrika,kuigeuza na kuifanya Arusha kuwa makao makuu ya utalii Afrika ya mashariki na kati na kuweka mikakati na mipango na wadau wa utalii katika jimbo hili kuhakikisha utalii unatangazwa na vijana wanapata ajira ya uhakika kupitia sekta hii mama katika jimbo hili.

Nitahakikisha haki na usawa unapatikana kwa wafanyakazi wa jimbo hili,nitwaunganisha na kutengeneza vyama vya wafanyakazi vitakavyokuwa na sauti yenye nguvu na itakayosikika na kufanyiwa kazi na serikali,wafanyakazi wa chini nitawahakikishia wanajiona kuwa ni sehemu ya watu wanaostahili kupata haki zao,malipo yao ya zaida,mikataba yenye nguvu katika kazi,nitawatengenezea mazingira ya kuwa sehemu ya jamii inayosikilizwa nchini Tanzania.

Nitaanzisha mpango wa vijana kujiendeleza kielimu na kuanzisha masomo ya jioni kwa ajili yao kwa ajili ya kuwaandaa kuwa wataalamu watakaoendesha maisha yao na kufikia viwango vya juu vya elimu,elimu ya watu wazima itaimarishwa katika misingi rahisi,watoto na wanafunzi wasiokuwa na uwezo wa kupata mahitaji ya shule watapata kupitia mfuko maalumu utakaotengenezwa kwa ajili yao.

Nitahakikisha serikali inaboresha mazingira ya upatikanaji wa matibabu kwa wakazi wa Arusha mjini,madawa yafike kwa wakati na bima maalumu ianzishwe kwa ajili ya watu masikini na wasiokuwa na uwezo.

Kama mbunge wa Arusha mjini,nitaweka mkakati wa kuzungumza na watu wangu kila mwisho wa mwezi,mazungumzo ambayo yatakua ni mazungumzo ya wazi na kila mtu atakua na uhuru wa kuuliza au kutolea maoni chochote katika jimbo langu.

Nitaunganisha taasisi na asasi zote za maendeleo,kina mama,watoto,kina baba na vijana kwa ajili ya kupata fursa mbalimbali zitakazotokea,itakua Arusha ya uwazi,Arusha ya fursa,Arusha ya maendeleo,Arusha ya mfano.

Ni wakati wa mabadiliko katika jimbo la Arusha mjini,ni wakati wa vijana wachapakazi wasio na maneno,ni wakati wa kuileta Arusha pamoja.

Natangaza nia rasmi ya kugombea ubunge jimbo la Arusha mjini.

Asanteni.

Idd Ninga.
Arusha Mjini
04.07.2020
 
Labda ukaongoze ma-abdool wenzio miskitini huko
Usitake kuingiza jambo ambalo halipo,tafadhali tuache tufanye siasa zetu za amani,upendo,umoja na siasa zenye roho na utamaduni wa mtanzania,hizi unazotaka kuzianzisha hatuzihitaji Tanzania.
 
Huna uwezo huo, narudia HUNAA
Sawa,subiri matokeo,kwa sasa hautoamini kwa sababu bado sipo katika nafasi ya kuyafanya yale ambayo wana Arusha mjini wamekua wakiyahitaji kwa miaka mingi.
 
Ulijisahau sana,wakati ukichimba Na wewe ulikuwa unachimbwa vizuri sana bila kujijua, Ndio maana katika mijadala mingi nilikuwa na kuingiza usipotaka na ukaingia kilaini kabisa.
Kumbuka, wana Arusha hawahitaji mijadala ya dini, wanahitaji maendeleo,hawahitaji maneno wanahitaji kusonga mbele.
Unajificha nyuma ya ID fake na bado unajulikana hadi ukucha,unaonaje hilo ?
 
Ndio sababu kubwa ya kulichukua jimbo hili, hatutaki kuwa na watu wanaokubali kila wanachoambiwa eti kwa sababu tu wataonekana wabishi,tunataka kuwa na watu watakaosimamia katika hoja zao hata kama wataonekana viroja, tunataka vijana watakaoibadili Arusha yao na kufikia maendeleo na uchumi imara, hatutaki watu wa ndio mzeee, Ndio mzeee
 
Za uso laivu mchana kweupeeee. JF bana !!!

Ubaya wa mijadala ya kidini huwa ni migumu na kwa kawaida haina mshindi sana sana ni kutukanana tu kama majuha. Miye huiepuka kila inapowezekana !
 
Unataka ugombee ubunge kupitia chama gani?
 
Mwache kamanda Lema wewe tafuta jimbo lingine kwa tiketi ya CDM.
 
Naona unahangaika sana kutaka kuileta mada ya udini,ila hebu kaa pembeni hiyo si hoja yangu kwa sasa, ubishi ni sehemu yangu ya kutetea hoja zangu, kama ungetaka nisiwe mbishi basi ungekubali like ninachokisema,yani unakataa ninachokisema halafu bado unaniona mimi mbishi,kila mtu ana dini yake lakini katika siasa hakuna wapagani wala hakuna upendeleo wa kidini.
unachotaka wewe ni kutaka kuwalazimisha watu waingie katika hoja ya kipumbavu ya UDINI.
kwa hill koma sana,usitake kuingiza ujinga huu, nakwambia tena upuuzia wa udini haupo katika hoja zangu, Kama kweli wewe mwanaume na una uwezo wa kujibizana hoja na mimi, tukutane tu majukwaani live live, siyo unajificha hapa na ID fake yako halafu unapiga kelele za mambo ya dini,katika tangazo langu sijaongelea huo upuuzi wako.
Nasema tena, acha ujinga wa kuhusisha dini katika hili.
 
"Siasa za amani, upendo, umoja na siasa zenye roho na utamaduni wa mtanzania"

Nikisikiaga hizi kauli kwa siasa za Tanzania huwa nacheeeeka.... Kwa dharau
Usitake kuingiza jambo ambalo halipo,tafadhali tuache tufanye siasa zetu za amani,upendo,umoja na siasa zenye roho na utamaduni wa mtanzania,hizi unazotaka kuzianzisha hatuzihitaji Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…