Namanga: Madereva 23 toka Tanzania wazuiliwa kuingia Kenya baada ya kukutwa na COVID-19

Namanga: Madereva 23 toka Tanzania wazuiliwa kuingia Kenya baada ya kukutwa na COVID-19

Serikali ya CCM pamoja na Rais, waitishe kikao cha dharura kulinusuru taifa. Hili swala halina chama wala kabila, ni swala la dharura la kitaifa. Mambo yanaelekea kubaya...
Acha taharuki hata huko kenya kuna COVID19 kedekede kila mahali huo ugonjwa upo usichanganyikiwe changanyikiwe kua mtulivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mama angejiuzulu tu lakini ndo hivyo tena! Hata akiondoka, anakuwa replaced hapo hapo na kazi inaendelea.
Ili iweje kwani yeye ndiye kawapa hao madereva hiyo COVID19?au yeye ndiye kaficha dawa ya COVID19?na kama a akijiuzulu ndiyo huo ugonjwa utaisha sekunde hiyo hiyo?mbona unachanganyikiwa sana kupita kawaida?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi maabara za kuhama zina usahihi wa kiasi gani. Nilichosikia ni kuwa siyo sahihi sana katika matokeo.

Pia kwa mujibu wa taratibu za WHO hao wagonjwa wanatakiwa watibiwe nchi waliyopimwa na kukutwa wagonjwa. Inakuwaje Kenya wawazuie kuingia ili watibiwe?
 
EX4YD-gX0AAvQ1r (1).jpeg
 
Niliandika siku kadhaa kuwa mbinu sahihi ni test, test, test test na anayepatikana unam-isolate kumpatia tiba ya dalili alizonazo; lakini waziri akasema tuna test wale tu wenye dalili au waliokuwa karibu na wenye dalili!
Haya sasa tunaadhirika mpakani na madreva wanarundikana na kuambukizana! Je wanaporudishwa Tanzania, tunachukua tahadhari gani maana sisi vipimo vyetu vinaonyesha hata papai lina corona!
Too late to do that now. It seems the damn virus is alll over the country. We still want to know the extent of the infection, so dear our govt be transparent here please
 
Nikiwa kama ni mtu ninayeweza kushughurisha akili zangu ninaona habari nyingi ni upuuzi tu, tunaishi wote mitaani na tunasafiri sana tu na tuna ndugu jamaa na marafiki huko mikoani kote,hakuna vifo kama mnavyosema..swala la madereva kukutwa na Covid-19 yamkini ni uongo wa 95%..kuna watu wanasafiri na mabasi,

kuna vijiwe vya kahawa na masoko yanaendelea na hakuna Covid kwa kiwango msemacho,leo ije iwe kwa dereva wa roli anayesafiri peke yake au yuko na tingo wake tu?kwanza hata kumuona tu mtu hatumuoni,wala ndugu,wala jamaa,wala jirani na rafiki wa jirani,sasa hiyo Covid iko wapi?

Hii naamini ni kweli ni vita ya kiuchumi na inapiganwa na washenzi walioamua kunyenyekea kwa mabeberu,kuna nchi jirani zetu na mataifa mengi tu inaonyesha kuna mkono wa mzungu wameshibishwa kidogo ili kumsaidia beberu/mkaburu..kufifisha uchumi wa mataifa na waje kwa sura za kutoa misaada ili wakirudi tena kesho wapate kufunguliwa mlango kibiashara dhuluma.

Rais wetu atashinda ktk hili kwa uwezo mkubwa wa MUNGU.Asikiaye na afahamu.

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Acha uongo
Mbona update za Ukimwi na malaria huwa hatupewi na hamlalamiki?

mie naona waendelee kupiga kimya tu as long as tunajua Covid 19 ipo mtaani so tuendelee kujifukiza na kujikinga
 
Wazee wa vyama wanaweza kufanya nini?
WHO walianza kutoa alert ya kutokupewa ushirikiano wa kutosha

Zambia wamefunga mpaka kwa ajili ya madereva malori 18...
 
Mbona update za Ukimwi na malaria huwa hatupewi na hamlalamiki?

Mie naona waendelee kupiga kimya tu as long as tunajua Covid 19 ipo mtaani so tuendelee kujifukiza na kujikinga
Ikitokea outbreak ya Colera mbona huwa hawatangazi? na watu hawalalamiki?
Kule spain nilisikia wahudumu wa afya wakilalamika kuwa figure serikali inatoa ni za uongo kwa sababu wao waliacha kuhesabu kwa sabau ya wingi wa maiti. Sasa bora lipi tunyamaziwe au tupewe figure za uongo.

Then tukipewa kinafuata nini? Tuipe serikali uhuru, watangaze wanapoona ni muafaka kwa sababu ya uhamasishaji, wakiona sio salama wasituambie ni kuogopesha raia bure
 
Wewe elewa tu kua Corona imegonga mwamba huku Africa,it's ok kua ni ugonjwa upo na tunapaswa kabisa kuchukua kila tunaloelekezwa na Serikali maana wao ndo wanafanya jitihada za kuhakikisha tuko salama.

Lakini this mdudu unaitwa Corona..imeshindwa na ni kwa sababu ni vita, ni ugonjwa biashara, MUNGU atatutetea sana na Rais wetu atachukua taji hata kama hawatasema tutasema sisi wananchi wake.
[emoji23][emoji23] Kwa namna hii!!! Kama ni kweli! Natilia mashaka afya zetu, huenda tumeathirika karibu wote Ila cha ajabu, Watanzania wako Imara licha ya kutembea na virusi mwilini mwao, hii Nayo ni ajabu duniani.

Mimi nishauri, ikiwezekana, kuchukuliwe vipimo, virusi wale wapimwe utendaji wao wa kazi kwenye miili yetu Watanzania ili ibainike kama virusi hao hawawezi kutuathiri tuendelee kujichanganya zaidi.

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Mbona update za Ukimwi na malaria huwa hatupewi na hamlalamiki?

Mie naona waendelee kupiga kimya tu as long as tunajua Covid 19 ipo mtaani so tuendelee kujifukiza na kujikinga
Ukimwi na malaria zina dawa angalau za kupunguza lkn corona bado haijapata dawa wala chanjo.
 
Back
Top Bottom