Namba za simu za Ofisi nyingi za Serikali hazipatikani

Namba za simu za Ofisi nyingi za Serikali hazipatikani

Sijui ni nani anahusika ku huisha namba za Ofisi za Serikali kama za Mawaziri/Wizara, Wakuu wa mikoa, Wilaya, Hospitali za Mikoa, Hospitali kuu za Wilaya na taasisi nyingi za Serikali kwenye mtandao kwani namba nyingi zilizopo zilishafungiwa au zimebadilika.

Naamini kutokuwa na namba za simu sahihi za Idara/mashirika ya Serikali, huchangia Vijana wengi kuishia kuandika malalamiko kwenye mitandao, badala ya kuwasiliana moja kwa moja na ofisi husika.
Kama unawatafuta kwa landline kamwe hutawapata, tumia namba zao za mikononi.
 
Kuna siku kwa mbwembwe kabisa nikaingia website ya Air + Tanzania ili niunge mkono kipaumbele Cha Jiwe, nikachukua namba zao za simu ili nipate maelelezo ya ruti zao. Nilipiga nusu saa mzima simu haipokelewi. Nikajaribu Precision Air. Kugusa tu mhudumu akapokea
 
Ni afadhali ambazo hazipatikani jumla kuliko zile unapiga wee ila hazipokelewi.
Kuna wale ukiwapata kwenye simu hata kama ni issue tuu ya kujua bei, gharama au utaratibu flani utasikia njoo ofisini!! Yaani hajui na wala hajali kwamba uko kijijini, say 100 km or so... Unatamani hata kumtwanga kibao...
 
Back
Top Bottom