Gemini Are Forever
JF-Expert Member
- Sep 10, 2019
- 1,508
- 2,619
Za kwenu!
Nipo mkoa fulani kikazi. Na nina ndugu yangu, mtoto wa Shangazi amekuja huku kikazi na nimempokea kama ndugu yangu. Namhifadhi kulala pamoja na kula.
Kinachonikera kwake ni uvivu. Vibarua vipo sio haba endapo ukiwa na bidii, na huko kwenye vibarua anaweza kwenda na akapata chakula huko huko (ukibahatika) na kupunguza gharama za chakula either kwake au kwangu.
Mimi kila siku naenda kazini ila yeye amekuwa mtu wa kulala tu na kuzurura.
Kuna mgahawa nimempeleka awe anaenda kula then nije kulipa ikiwa siku amekosa kibarua lakini imekuwa kigezo cha yeye kutojishughulisha (pengine kwa sababu ana uhakika wa kula na kulala).
Amekuwa analala, akiamka asubuhi anaenda pale mgahawani anakula, anaingia vijiwe vya drafti, vibanda umiza n.k.
Kiukweli wakuu ananipa gharama za chakula sana na ukizingatia kuna vibarua angefanya tu na kujiingizia angalau visenti pamoja na kula.
Je, nimfanyaje huyu wakuu maana ni kama yupo nyumbani kwa Baba yake amesahau kuwa tumekuja kupambana?