Namhifadhi kulala pamoja na chakula lakini ni mvivu kwenda kwenye vibarua. Nifanye nini?

Namhifadhi kulala pamoja na chakula lakini ni mvivu kwenda kwenye vibarua. Nifanye nini?

Amekuja kwa ajili ya kazi,sawa

Sometimes ni ngumu kwa baadhi ya watu kuendana na mazingira ikiwa unafahamu ajira/vibarua ni changamoto ila kwakuwa wewe mwenyeji na umesema fursa hizo zinapatikana kwa wingi basi Kaa chini uongee naye
Sometimes, vibarua ni changamoto ila mara nyingi vikitokea anasema kazi ngumu, mazingira magumu n.k..

Pamoja na hayo, ameshindwa kutafuta namna ya kufanya mfano aende nyumbani kama mazingira yamemshinda. Nimejaribu kumwambia aende nyumbani napo hataki anasema "ngoja nisikilizie labda nitazoea mazingira"
 
Maisha ya sasahv sio ya kuogopana especially kama mtu anakuumiza. We muambie ukweli, kama hawezi kufanya kazi arudi alipokuwa.
 
Mkuu, unaweza kumtafutia kibarua lakini amekuwa akikwepa, mara aseme hajisikii vizuri, mara kachelewa...! yaan atafanya kila analoweza ili mradi tu asiende kibaruani halafu baadae unamkuta vijiweni.
Ongea nae usimpe chakula afanye kazi
 
Sometimes, vibarua ni changamoto ila mara nyingi vikitokea anasema kazi ngumu, mazingira magumu n.k..

Pamoja na hayo, ameshindwa kutafuta namna ya kufanya mfano aende nyumbani kama mazingira yamemshinda. Nimejaribu kumwambia aende nyumbani napo hataki anasema "ngoja nisikilizie labda nitazoea mazingira"
Mm nmemaliza chuo soon tu. Nauza maembe na kupaka rangi majumban na kazi kwenye mashirika naomba. Nimeshangaa San kuona baadhi ya ndugu zangu wananilaumu Kwa nini nauza maembe. Sasa waliotaka niwaombe hela za vocha?. Mkuu rudisha kwenu hiyo mutu
 
Kama ana miaka zaidi ya 18 hapo unalea tatizo na haumsaidii. Unamuwekeaje bill mtu kwenye mgahawa. Huyo mpeleke dry dry ikibidi kula huko huko ukirudi mwambie mambo magumu leo. Fanya hivyo siku tatu utakuwa umemtibu huo ugonjwa wa uvivu. Mjini mtu unampa pa kulala tu.
 
Kumpa mtu chakula na sehemu ya kulala sio msaada hayo ni mahitaji ya msingi ya mwanadamu na hata yeye hawezi kukukumbuka kwa sababu ulimpa chakula na malazi.

Msaada ni lile jambo utakalolifanya juu yake ili aweze kupata mwenyewe mahitaji ya msingi.

Msaidie ndugu yako hukohuko alipo kama yupo nyumbani kwa wazazi wenu msaidie hapohapo ili atoke kama ulivyotoka wewe.
 
Genius bro [emoji120][emoji120][emoji1666]
 
Kumpa mtu chakula na sehemu ya kulala sio msaada hayo ni mahitaji ya msingi ya mwanadamu na hata yeye hawezi kukukumbuka kwa sababu ulimpa chakula na malazi.

Msaada ni lile jambo utakalolifanya juu yake ili aweze kupata mwenyewe mahitaji ya msingi.

Msaidie ndugu yako hukohuko alipo kama yupo nyumbani kwa wazazi wenu msaidie hapohapo ili atoke kama ulivyotoka wewe.
Kumpa mtu chakula sio msaada ni mahitaji ya msingi boss upo serious? Maandiko yenyewe yanasema asiefanya kazi na asile..sasa hufanyi kazi ila unakula bure useme hujasaidiwa ni haki yako, kweli?
 
Kwani uwezo wako ukoje unapompa tafu kwenye kula na kulala inakuelemea kiasi gani mpaka unahisi unaumia. Endapo una uwezo kiasi kwamba hyo kula yake sio issues sana we mpige tafu tu hata kama miezi 6/12 huwezi jua bro kitu gani utatengeneza kwenye akili yake juu yako na mtazamo wake kwenye kusaidia wengine

Itakua faraja sana endapo umemsaidia ata kama mda mrefu akaja kupata channel ya ndoto yake na kutusua maisha huko mbeleni kutakua na history yako kwenye maisha yake na inabidi tu uheshimu tu mana ameshakwambia kazi hizo si rafiki kwake huna haja ya kumlazimisha ila kama uwezo wako ni mdogo umeelemewa mwambie ukweli tu ili arudi nyumbani kwa uzuri si kwa ubaya kuna kitu pia utakuwa umekijenga.

Ni mtazamo wangu tu huu na ushauri tu sio lazima mkuu [emoji120]
 
Dah umenikumbusha stori za huko kwetu br.
Ndugu yangu mmoja yeye ana 40 watoto 5 but hajui kujitegemea. Maisha yake yote alizoeshwa kutokujitegemea. Sijui hii ilitokea kwa bahati mbaya ama vipi.
Hadi 200 ya shule kwa wanae hawezi. Watoto wanamcheki Bibi yao na Ni wengi ( bi mkubwa wangu) yaani Ni mtihani.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Watu wa hivi wapo mkuu, nafikri ni hulka yao ya kutowajibika hata kwa maisha yanayowahusu wao wenyewe au wamejikuta kwenye mazingira ya kukata tamaa, ama wana ndugu na jamaa wengine wanaowazunguka ambao wanaweza kuwasaidia majukumu yao hivyo wanaamua kujiendekeza.....
 
Mtafutie mume aolewe ale na kulala bure kazi yake ni kukata viuno usiku wa manane.
 
Sio Yale makabila ya mungu ndio anajua. Kufanya kazi mtihani hayo. Sijui tuyasaidie vip walahi. Sio watu wa pwani huyo?
Mkuu watu wa pwani, mbona mzee msoga alipiga kazi ya kutukuka? au mandonga mtu kazi yeye atakuwa mtu wa wapi.... 😂
 
Un
Za kwenu!

Nipo mkoa fulani kikazi. Na nina ndugu yangu, mtoto wa Shangazi amekuja huku kikazi na nimempokea kama ndugu yangu. Namhifadhi kulala pamoja na kula.

Kinachonikera kwake ni uvivu. Vibarua vipo sio haba endapo ukiwa na bidii, na huko kwenye vibarua anaweza kwenda na akapata chakula huko huko (ukibahatika) na kupunguza gharama za chakula either kwake au kwangu.

Mimi kila siku naenda kazini ila yeye amekuwa mtu wa kulala tu na kuzurura.

Kuna mgahawa nimempeleka awe anaenda kula then nije kulipa ikiwa siku amekosa kibarua lakini imekuwa kigezo cha yeye kutojishughulisha (pengine kwa sababu ana uhakika wa kula na kulala).

Amekuwa analala, akiamka asubuhi anaenda pale mgahawani anakula, anaingia vijiwe vya drafti, vibanda umiza n.k.

Kiukweli wakuu ananipa gharama za chakula sana na ukizingatia kuna vibarua angefanya tu na kujiingizia angalau visenti pamoja na kula.

Je, nimfanyaje huyu wakuu maana ni kama yupo nyumbani kwa Baba yake amesahau kuwa tumekuja kupambana?
afugaje mtu mvivu!? Mpangie kazi mpaka apaone pachungu hapo
 
Watu wa hivi wapo mkuu, nafikri ni hulka yao ya kutowajibika hata kwa maisha yanayowahusu wao wenyewe au wamejikuta kwenye mazingira ya kukata tamaa, ama wana ndugu na jamaa wengine wanaowazunguka ambao wanaweza kuwasaidia majukumu yao hivyo wanaamua kujiendekeza.....
Asee inaskitisha. Na unajiuliza bi mkubwa 60+ anawezaje kuwalisha wao? Na si wao wamlishe bi mkubwa.
Chaajabu utaskia maza anawapelekea hata vihela kidogo ulivyotuma eti nao watumie.
Huwa najiuliza hivi maza asipokuwepo maisha yake na familia yatakuwaje

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Asee inaskitisha. Na unajiuliza bi mkubwa 60+ anawezaje kuwalisha wao? Na si wao wamlishe bi mkubwa.
Chaajabu utaskia maza anawapelekea hata vihela kidogo ulivyotuma eti nao watumie.
Huwa najiuliza hivi maza asipokuwepo maisha yake na familia yatakuwaje

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Mtu anaishi passively ili mwisho wa siku yeye na familia yake wawe mzigo kwa wengine, na unakuta watu wa hivyo wana lawama kishenzi...
 
Back
Top Bottom