Namhifadhi kulala pamoja na chakula lakini ni mvivu kwenda kwenye vibarua. Nifanye nini?

Kaa nae kwa upendo umieleweshe kuwa anavyokaa bila kujishughulisha anapoteza muda na aelewe kuwa maisha ni magumu.Mwambie kuwa hata wewe unatamani kushinda nyumbani ila haiwezekani.Muweke wazi kuwa msaada wa kula na kulala unampa kwa sababu yeye ni ndugu yako na si kwa sababu unajiweza sana na pia ajue leo upo kesho haupo,leo unaweza kumsaidia kesho unaweza ukakwama ukashindwa kumsaidia.Msaidie kwa kutia chachu ya kutamani kufanikiwa na ikishindikana ndio umrudishe nyumbani.
 
Mwambie awe anapika nyumbani kupinguza gharama za kula mgahawani
 
Sio Yale makabila ya mungu ndio anajua. Kufanya kazi mtihani hayo. Sijui tuyasaidie vip walahi. Sio watu wa pwani huyo?
Pwani hamna uvivu usikariri kama unabisha mwambie ataje hilo kabila kama la pwani?
 
Mkuu watu wa pwani, mbona mzee msoga alipiga kazi ya kutukuka? au mandonga mtu kazi yeye atakuwa mtu wa wapi.... 😂
Hao watu wengi wao wakipata hela ya kula ni kutomb*n* mpka iishe ndo wakatafte nyingine
 
Mfukuze
 
Kata kulipa pesa ya msosi hapo mgahawani weka jiko home na mazagazaga ya kupika yasiwe yale ya vinono mdogo mdogo unakua unapunguza mahitaji atazinduka tu
 
Pole sana. Kuna wakati ukweli unasaidia sana kujenga,suala hapo ni kumwambia ukweli tu.
 
Angekuwa wa kike ungenipata assist angekaa kwangu bure [emoji3]ila nikimchoka nakurudishia
 
Mshike mkono mkatafute wote kazi, akikataa au kufukuzwa kazi , chukua funguo za nyumba mpe nauli na hela ya kula njiani arudi alipotoka
 
Huyo ni mvivu na unamlea ndio maana anakuonea na kukutesa. Watu wavivu furaha yao ni kuona wengine wanateseka kwaajiri yao huku wakitumia chochote kinachotafutwa na mwengine bila kuwazia gharama yake.


Sasa huyo ndugu yako kaa nae kitako na umueleze kuwa hapo umempatia hifadhi ya muda si ya kudumu hivyo asijirahisi sana akachukulia maisha ni kujiachia na kufanya anavyojisikia na uvivu wake.

Mtafutie shughuli ya kufanya ili aanze kuwajibika na maisha yake. Ukiendelea kukaa kimya haumsaidii na unamuongezea tatizo.
 
Mtu wa tanga ww
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…