Namibia yapeta kusafirisha nyama Marekani

Namibia yapeta kusafirisha nyama Marekani

viking

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Posts
2,183
Reaction score
1,322
Nchi ya Namibia imekuwa Nchi ya kwanza kutoka Africa kwa kuweza kusafirisha nyama kwenda USA . Shehena ya kwanza ya nyama tani 25000 inaondoka mwezi huu. Tanzania tunaweza kufanya biashara ya nyama kama tukiamua kwani tuna maeneo mazuri sana ya kufugia ng'ombe .

Botswana pia ni nchi nyingine ya Kiafrika ambayo inajihusisha na usafirishaji wa nyama. Rais Kikwete alikuja na sera ya kilimo kwanza lakini iliishia kwenye makaratasi.

Bado naamini kilimo kinaweza kutupeleka mbele zaidi kuliko viwanda.Morale ya wakulima ipo chini sana hata wachaga siku hizi wana pendelea kulima ndizi zaidi kuliko kahawa
 
Bahati ya mwenzako....???malizia mkuu.
 
Bahati ya mwenzako....???malizia mkuu.
Namibia kuna wazungu wengi wanafuga kisasa sana ngombe wa nyama kwa kiwango cha kimataifa

ngombe wao wa nyama ni ile mingombe mikubwa sana kama kiboko

sisi hapa ufugaji huo wa ngombe wa nyama bado sekta binafsi haijachangamka

tenda za kusafirisa nyama nje ziko kibao tatizo ni upatikanaji wa hiyo nyama

mfano waweza ingia mkataba wa kupekeka nyama uarabuni tani elfu 25 kwa wiki ndege ya kubeba wanaileta wenyewe ukiingia huo mkataba utashindwa na utafilisiwa sababu wafugaji wetu hawafugi kibiashara huuza ngombe siku akijisikia au akiona ana shida .

si kwamba hatuwezi sekta binafsi inapenda tu kufanya umachinga na uchuuzi wa kuuza bidhaa za nje badala ya ufugaji
 
Katika kupanga mipango ya kilimo kwanza ni muhimu kuwahusisha wahadhiri wa vyuo vya kilimo. Waweze kuandaa course ndefu na fupi zitakazo wanufaisha raia katika uwekezeji wa kilimo na ufugaji.

Kutafuta masoko ya bidhaa, soko la ndani peke yake ni kubwa kama kuna usafiri wa kueleweka. Watu wa Bukoba na Kigoma wanaweza kupata samaki barafu kutoka Tanga na nyanya kutoka Lushoto.
 
Waafrica ndio maana hatuendelei kila kitu siasa ndeeeeeefu. Sasa hapo vyuo vinaingiaje Sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesahau kuwa siasa za tz hazina urafiki na taaluma!

Katika kupanga mipango ya kilimo kwanza ni muhimu kuwahusisha wahadhiri wa vyuo vya kilimo. Waweze kuandaa course ndefu na fupi zitakazo wanufaisha raia katika uwekezeji wa kilimo na ufugaji.

Kutafuta masoko ya bidhaa, soko la ndani peke yake ni kubwa kama kuna usafiri wa kueleweka. Watu wa Bukoba na Kigoma wanaweza kupata samaki barafu kutoka Tanga na nyanya kutoka Lushoto.
 
Waafrica ndio maana hatuendelei kila kitu siasa ndeeeeeefu. Sasa hapo vyuo vinaingiaje Sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bila elimu tutaishia kuzalisha mazao hafifu kwa nguvu kubwa. Hivi unafahamu kuwa elimu ni biashara? Course za miezi mitatu kwa vijana kufifunza ukulima bora wa korosho kwa mfano utasaidia vijana na pia uchumi.
 
YEHODAYA, Bwashee unailamu sana sekta binafsi, serikali imefanya nini kuwawezesha?

Na kama mkiingia huo mkataba, ni jukumu lenu kuwaelekeza wafugaji nini wafanye ili huo mkataba uwe na tija kwenu na kwa wafugaji pia, badala ya kuwalaumu wafugaji directly kama unavyofanya.

Tanzania ni nchi ya tatu kwa ufugaji Africa kama sijakosea, sasa kwa n'gombe wote tulionao sioni sababu ya sisi kushindwa kufanya kama Namibia, japo n'gombe wetu hawawezi kuwa na uzito sawa na hao wa Namibia, but atleast, tujitahidi kwenye ubora wa nyama na ngozi tutafanikiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakulima hao, ni waleee .... mabeberu wa enzi zile. Settlers. Jiulize vibarua wao ni kina nani. Matter of fact ile nchi ukiingia humu ni kama "ujerumani flani". Dont compare na Bongo.
Mabeberu ni hatari sana mpaka kuwe na chain ya benefit kwao
 
Kupanga ni kuchagua, bado tuna katiba inayompa Rais nguvu kuzidi hata bunge.Wazo ATCL sawa kwa vibua ndege za kati focus usafiri wa ndani na majirani, hiyo midege mikubwa hiyo pesa tungewekeza kilimo umwagiliaji na mifugo wataalam vijana sua nk tungelisha dunia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila elimu tutaishia kuzalisha mazao hafifu kwa nguvu kubwa. Hivi unafahamu kuwa elimu ni biashara? Course za miezi mitatu kwa vijana kufifunza ukulima bora wa korosho kwa mfano utasaidia vijana na pia uchumi.
Watu wamekuwa wanauza korosho nje miaka na miaka kwa elimu ya kitaa tu, Nyie na elimu zenu za PDF mmekuja maliza na kuharibu soko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soko la maziwa la ndani hatujalitendea haki pia. Fikiria kama tunatengeneza ice cream na milkshake zisambae mpaka huku kwetu Nanjilinji na Kaliua. Yote haya yanafanikiwa kuanzia kwenye ubora wa barabara.
 
Sky Eclat,
TATIZO TANZANIA WAMEANZA KILIMO CHA (GMO) A GENETICALLY MODIFIED ORGANISM. AMBAPO TUTA KUWA NA VYAKULA VIBAYA VYENYE KUKUZWA HARAKA HARAKA KWA HIZO CHEMICALS.

WASINGE RUHUSU HUO UCHAFU KWANZA ARDHI YETU NZURI YENYE RUTUBA ITA HARIBIKA PIA HATU TAKUWA NA VYAKULA VIZURI NATURAL KAMA ZAMANI. EEEH MUNGU KWANINI UKATU LETEA MAGUFULI?
 
Back
Top Bottom