Namibia yapeta kusafirisha nyama Marekani

Namibia yapeta kusafirisha nyama Marekani

iwawezeshe kufuga ngombe au? kwani masai ngombe wake anaofuga kawezeshwa na serikaki? Asas anayeuza maziiwa ya ngombe hadi nje ya nchi kawezeshwa na serikali?
Huo ufugaji wa mazoea ndiyo haujatuletea tija mpaka sasa. Serikali iandae masomo mafupi kwa vijana na baada ya masomo ndiyo pesa ya vikoba ianzie Hapo. Si kuwakopesha vijana bodaboda na wakipata ajali hawasaidiwi matibabu.
 
Bila elimu tutaishia kuzalisha mazao hafifu kwa nguvu kubwa. Hivi unafahamu kuwa elimu ni biashara? Course za miezi mitatu kwa vijana kufifunza ukulima bora wa korosho kwa mfano utasaidia vijana na pia uchumi.
Tuna chuo kikuu cha kilimo na vyuo kibao vya mifugo vinatoa wataalamu wabobezi wa kilimo na mifugo ila wakimaliza kusoma hawalimi wala kufuga wanazurura mijini wakiwa wamelamba suti wakitembea kifua mbele huku wakiwa wamebeba mabegi yenye laptop migongoni zenye takwimu za kilimo na mifugo wasiyofuga wala kulima
 
iwawezeshe kufuga ngombe au? kwani masai ngombe wake anaofuga kawezeshwa na serikaki? Asas anayeuza maziiwa ya ngombe hadi nje ya nchi kawezeshwa na serikali?
Wawezeshwe kwenye elimu ya ufugaji, hasa kwenye ubora wa nyama na ngozi, na usimlinganishe ASAS na mfugaji wa kisukuma wa kule kijijini, au mmasai, ambao kila siku wanahangaika na n'gombe zao kuwatafutia malisho.

Serikali isikwepe wajibu wake hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TATIZO TANZANIA WAMEANZA KILIMO CHA (GMO) A GENETICALLY MODIFIED ORGANISM. AMBAPO TUTA KUWA NA VYAKULA VIBAYA VYENYE KUKUZWA HARAKA HARAKA KWA HIZO CHEMICALS. WASINGE RUHUSU HUO UCHAFU KWANZA ARDHI YETU NZURI YENYE RUTUBA ITA HARIBIKA PIA HATU TAKUWA NA VYAKULA VIZURI NATURAL KAMA ZAMANI. EEEH MUNGU KWANINI UKATU LETEA MAGUFURI!!!???
Tutashindwa hata kuzalisha organic products
 
Tuna chuo kikuu cha kilimo na vyuo kibao vya mifugo vinatoa wataalamu wabobezi wa kilimo na mifugo ila wakimaliza kusoma hawalimi wala kufuga wanazurura mijini wakiwa wamelamba suti wakitembea kifua mbele huku wakiwa wamebeba mabegi yenye laptop migongoni zenye takwimu za kilimo na mifugo wasiyofuga wala kulima
Sasa ni jukumu la nani kuwaajiri hao na kuwapeleka field wakatoe elimu kwa wahusika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wawezeshwe kwenye elimu ya ufugaji, hasa kwenye ubora wa nyama na ngozi, na usimlinganishe ASAS na mfugaji wa kisukuma wa kule kijijini, au mmasai, ambao kila siku wanahangaika na n'gombe zao kuwatafutia malisho.

Serikali isikwepe wajibu wake hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Vyuo vya kilimo na ufugaji viko kibao kuanzia vidogo hadi vyuo vikuu kwa hiyo serikali iwakamate kwa nguvu iwapeleke kwenye hivyo vyuo au? wakati wanaviona vipo
 
Tuna chuo kikuu cha kilimo na vyuo kibao vya mifugo vinatoa wataalamu wabobezi wa kilimo na mifugo ila wakimaliza hawalimi wala kufuga wanazurura mijini wakiwa wamelamba suti wakiwa wamebeba mabegi yenye laptop migongoni zenye takwimu za kilimo na mifugo wasiyofuga wala kulima
Tatizo ndiyo hilo, vyuo vikuu vinatoa elimu ya juu kwa wachache nao wengine wanaishia kuwa wana taaluma. Unatakiwa kuandaa masomo ya vijana waliomaliza darasa la 12, Ada iwe rafiki na masomo yaweze kutoa elimu ya awaking ya kilimo bora.
 
TATIZO TANZANIA WAMEANZA KILIMO CHA (GMO) A GENETICALLY MODIFIED ORGANISM. AMBAPO TUTA KUWA NA VYAKULA VIBAYA VYENYE KUKUZWA HARAKA HARAKA KWA HIZO CHEMICALS. WASINGE RUHUSU HUO UCHAFU KWANZA ARDHI YETU NZURI YENYE RUTUBA ITA HARIBIKA PIA HATU TAKUWA NA VYAKULA VIZURI NATURAL KAMA ZAMANI. EEEH MUNGU KWANINI UKATU LETEA MAGUFURI!!!???
uko outdated GMO tanzania ilishapigwa marufuku mazao yote vyuo vya majaribio yakaharibiwa na utafiti ukafutiliwa mbali
 
Na Tanzania tutafika maana tayari kuna kiwanda cha Tan Choice na kingine kinajengwa Longido pia kuna kiwanda cha Mzindakaya kipo kinapiga kazi kimyakimya bila kelele, pia machinjio ya Dodoma yamefufuliwa. Tatizo ni malisho na mbegu za ng'ombe tulizo nazo. Ng'ombe wa asili wa kitanzania kwa miaka mitatu na nusu mpaka miaka mitano anakuwa na kilo 200 tu inakuwa hasara. Hao ng'ombe wa Namibia ni mbegu ya boran na mbegu nyingine za kisasa pia wanafugwa na wajerumani wa namibia na wana malisho ya hadhi ya kimataifa hata hivyo namibia ni jangwa pia wanapata madawa kwa wakati na chanjo zote kwa wakati, huku kwetu bongo 90% ya dawa na chanjo ni feki na wanachakachua paranex (dawa za josho) wanaweka maji mengiiiiiiiiiiii dawa kiduchu. Hatuwezi kuwafikia hao wajerumani wa namibia ni watu wenye akili kubwa mno wana mitaji mikubwa pia kumbuka nchi ya namibia ni jangwa ila ng'ombe anafikisha kilo 350-450 ndani ya miezi 18 mpaka 24.

Maoni.
1. Tuwe na ranch za kisasa kila wilaya angalau kuanzia hekta 100000.
2. Tupate mbegu nzuri za ng'ombe zinazokomaa haraka na kufikisha uzito haraka.
3. Tupate dawa na chanjo halisi.
4. Makodi ya hovyohovyo kwa wawekezaji wa sekta ya nyama yapunguzwe hasa kuingiza mitambo bandarini.
5. Tupambanie soko la uarabuni la nyama litatupa pesa nyingi za haraka.
6. Wafugaji wapewe mikopo ya kueleweka angalau kuanzia 50m na kuendelea.

Picha za boran. Pia kuna picha za ng'ombe wa asili (mifupa tupu)
 
Attachments

  • 14479550_716279698524231_4690008499451653350_n.jpg
    14479550_716279698524231_4690008499451653350_n.jpg
    112 KB · Views: 3
  • 58902321_2408236099406702_6827668162801041408_n.jpg
    58902321_2408236099406702_6827668162801041408_n.jpg
    122.8 KB · Views: 3
  • 86368967_3449156518492930_8761594036705296384_n.jpg
    86368967_3449156518492930_8761594036705296384_n.jpg
    39.3 KB · Views: 3
  • 52426855_1947957611981870_7320211052346474496_o.jpg
    52426855_1947957611981870_7320211052346474496_o.jpg
    107.7 KB · Views: 3
Tuna chuo kikuu cha kilimo na vyuo kibao vya mifugo vinatoa wataalamu wabobezi wa kilimo na mifugo ila wakimaliza kusoma hawalimi wala kufuga wanazurura mijini wakiwa wamelamba suti wakitembea kifua mbele huku wakiwa wamebeba mabegi yenye laptop migongoni zenye takwimu za kilimo na mifugo wasiyofuga wala kulima

Tena wanabeba mabegi meusi hivi na unakuta wanasema ni wataalamu wa kilimo na mifugo kutoka uyole au ukiriguru au zamani mubondo au wengine watasema SUA,

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwakifupi wanye taaluma ya kilimo na ufugaji wafikirie jinsi watakavyouza elimu yao kwa vijana wengi wa Tanzania. Elimu ya muda mfupi yenye basic contents zinazojitosheleza.
 
Hiyo biashara inamilikiwa na wamarekani wenyewe,jaribu wewe mswahili uone vikwazo,ooh! Nyama inaugonjwa
Nchi ya Namibia imekuwa Nchi ya kwanza kutoka Africa kwa kuweza kusafirisha nyama kwenda USA . Shehena ya kwanza ya nyama tani 25000 inaondoka mwezi huu. Tanzania tunaweza kufanya biashara ya nyama kama tukiamua kwani tuna maeneo mazuri sana ya kufugia ng'ombe .

Botswana pia ni nchi nyingine ya Kiafrika ambayo inajihusisha na usafirishaji wa nyama. Rais Kikwete alikuja na sera ya kilimo kwanza lakini iliishia kwenye makaratasi.

Bado naamini kilimo kinaweza kutupeleka mbele zaidi kuliko viwanda.Morale ya wakulima ipo chini sana hata wachaga siku hizi wana pendelea kulima ndizi zaidi kuliko kahawa
 
Soko la maziwa la ndani hatujalitendea haki pia. Fikiria kama tunatengeneza ice cream na milkshake zisambae mpaka huku kwetu Nanjilinji na Kaliua. Yote haya yanafanikiwa kuanzia kwenye ubora wa barabara.
Kuna kitu kinaitwa consumer behaviour kwenye uuzaji na ununuzi Wa bidhaa, watanzania wengi kunywa maziwa mpaka waandikiwe na daktari ,vivyo hivyo nyama huliwa kwa wingi baadhi ya mikoa plus matukio muhimu ndio familia hupata kitoweo

Sasa ukilitegemea zaidi soko la ndani kW nyama na maziwa bila kuliboost utazeeka na bidhaa zako kwenye jokofu.
Achilia mbali hizi elimu za mitandaoni ulaji Wa nyama na maziwa unaleta kansa ndio kabisaaa wabongo wanapata loophole teh teh!
Wazalishaji Wa ndani tupo tunazalisha mazao ya maziwa tena home based factories na tunasambaza nchini na Africa Mashariki ambapo nchi kama Kenya Rwanda na Sudan kusini wanakunywa sana diary products za Tanzania.
Tuendelee kufuga na kuboresha viwanda vya ndani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom