Namkamataje dereva wa lorry la Mohammed Enterprises TanzaniaLimited (METL)aliefanya wizi kukimbia? Msaada

Je niende ofisini kwao nikamshtaki au nitoe taarifa polisi kwa udanganyifu uliofanywa na huyu dereva?? Naomba mwenye kuhusika na hii kampuni aje pm nimuelezee aweze kuchukuliwa hatua dereva mwenye gari namba T 449 DPF
Pole sana ndugu kwa yaliyokukuta. Ushauri wangu, usiishie kumtafuta dereva kupitia mitandao pekee. Kusanya ushahidi wote unaohusiana na tukio hilo—mawasiliano, risiti, picha au taarifa nyingine—kisha toa taarifa rasmi Polisi ili uchunguzi ufanyike.

Pia unaweza kufika ofisi za kampuni husika na kuwasilisha malalamiko yako rasmi, ukiambatanisha taarifa za gari T 449 DPF na maelezo ya tukio. Ni vizuri jambo hili likafuatwa kwa njia za kisheria na kampuni ipewe nafasi ya kufanya uchunguzi wake.

Kama kuna mwenye mawasiliano sahihi ya kampuni au idara inayohusika, anaweza kumsaidia kuyapata kwa njia rasmi. Pole sana na tunatumaini utapata haki yako.
 
Taarifa ya uhalifu (wizi) inatakiwa kutolewa kituo cha Polisi kwanza kwaajili ya taratibu za kufungua shauri la jinai dhidi ya mtuhumiwa.

Baada ya kufanya hayo utapatiwa RB ambayo ndiyo reference utakayotumia kwenda kwa mwajiri wa huyo dereva kaajili ya hatua za kumuwajibisha huyo dereva. Ila kwenda kulalamika kwa mwajiri kabla ya kufungua kesi itaonekana ni majungu tu.
 
Pole sana ndugu kwa yaliyokukuta. Ushauri wangu, usiishie kumtafuta dereva kupitia mitandao pekee. Kusanya ushahidi wote unaohusiana na tukio hilo—mawasiliano, risiti, picha au taarifa nyingine—kisha toa taarifa rasmi Polisi ili uchunguzi ufanyike.

Pia unaweza kufika ofisi za kampuni husika na kuwasilisha malalamiko yako rasmi, ukiambatanisha taarifa za gari T 449 DPF na maelezo ya tukio. Ni vizuri jambo hili likafuatwa kwa njia za kisheria na kampuni ipewe nafasi ya kufanya uchunguzi wake.

Kama kuna mwenye mawasiliano sahihi ya kampuni au idara inayohusika, anaweza kumsaidia kuyapata kwa njia rasmi. Pole sana na tunatumaini utapata haki yako.
Great idea 💡, na akifanikiwa asi sahau kudai fidia ya muda na pesa zake alipoteza kumtafuta🙏
 
Pole sana ndugu kwa yaliyokukuta. Ushauri wangu, usiishie kumtafuta dereva kupitia mitandao pekee. Kusanya ushahidi wote unaohusiana na tukio hilo—mawasiliano, risiti, picha au taarifa nyingine—kisha toa taarifa rasmi Polisi ili uchunguzi ufanyike.

Pia unaweza kufika ofisi za kampuni husika na kuwasilisha malalamiko yako rasmi, ukiambatanisha taarifa za gari T 449 DPF na maelezo ya tukio. Ni vizuri jambo hili likafuatwa kwa njia za kisheria na kampuni ipewe nafasi ya kufanya uchunguzi wake.

Kama kuna mwenye mawasiliano sahihi ya kampuni au idara inayohusika, anaweza kumsaidia kuyapata kwa njia rasmi. Pole sana na tunatumaini utapata haki yako.
Asante kaka nashukuru sana kwa msaada wako kwa hakika dereva nilimuamini ila akavunja uaminifu na nikimpigia hapokei simu
 
Je niende ofisini kwao nikamshtaki au nitoe taarifa polisi kwa udanganyifu uliofanywa na huyu dereva?? Naomba mwenye kuhusika na hii kampuni aje pm nimuelezee aweze kuchukuliwa hatua dereva mwenye gari namba T 449 DPF
Ulimkabidhi mzigo ki-binafsi au kiofisi? Alikuwa anawakilisha kampuni au mlielewana tu kienyeji bila waajiri wake kujua? Na mwisho: Tumbili in town ni nini kilikutoa maporini mpaka ukaja mjini ambako sisi binadamu kumetushinda? Na kumalizia: Mbona huko mashambani mnakimbia na mazao ya binadamu, huoni dereva kalipiza?
 
Hapana sio swala la mzigo, kuna huduma alipewa akavunja uaminifu
 
Back
Top Bottom