Namna bora ya kumsaidia Bwana Mdogo mtaji wa Biashara

Ukifanya yote hayo utakosana na mdogo wako sababu mtu mzima ana hulka ya kujiongoza mwenyewe huwa hapangiwi, mimi nashauri mkatieni mirija mtelekezeni kwa mwaka mmoja tu apigike achakae ajifunze then mkikutana mwakani ukimpa mtaji kidogo atakua na adabu na hatarudia huo ujinga wa kuendekeza mademu
 
Noma sana dogo kajaziwa Million 10 kachomoa 8 kaacha 2 hizo 8 ni Bata TU kidimbwi Juliana Samaki Samaki Kitambaa Cheupe,
Kama ulikuwepo Mkuu. Dogo (Mwanangu) nilimwachia duka limejaa mitungi ya gesi midogo kwa mikubwa, maji ya kunywa ya kila aina, soda na juice. Nilikuwa mbali kidogo, nilivyorudi Dar nikaambiwa alikuwa anashinda Kitambaa Cheupe. Namuuliza salio hana hata sh 100. Dukani yamebaki makreti tupu na mitungi ya gesi tupu. Kwa kweli ni balaa!
 
Watu wote tuna Strengthes and Weaknesses. Unaweza kuta mwingine ni mchapakazi sana, ila utanzaji wa fedha ni zero na mwingine ni mtunzaji sana wa fedha, lakini kwenye kazi, ni mzembe sana. Hii ni suala la uwezo wa kuwatambua watu wako na kujua wana fit wapi. Unaweza kuta huyo bwana mdogo ungemuwekea mtu wa kuwa yeye jukumi lake ni kudeal na mauzo tu, usingekuta shida hii.
 
Bandiko zuri sanaa mheshimiwa... umetisha sanaa
 
Moja kati ya tatizo kubwa sana kwa vijana ni kuamini kuwa biashara ni mtaji na sehemu nzuri pa kuifanyia,....wanasahau sana juu ya NIDHAMU ya biashara.....hongera sana mkuu
 
Moja kati ya tatizo kubwa sana kwa vijana ni kuamini kuwa biashara ni mtaji na sehemu nzuri pa kuifanyia,....wanasahau sana juu ya NIDHAMU ya biashara.....hongera sana mkuu
Kabisa mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…