Mkuu upande wangu niko sahihi kabisa na upande wako uko sahihi kabisa.
Kufupisha tu wewe umeme wa buku unauona mwingi sana kulinganisha na maisha ya watanzania tunayoishi.
Mimi naendesha maisha kwa umeme.
Kwa siku natumia umeme wa 15,000 mpaka 20,000 na nitaongeza matumizi itafika mpaka umeme wa 45, 000 kwa siku.
So hiyo umeme wa buku sijui wa mia tisa unajilipa humo humo.
Na nilishasema mimi sipiki maharage kila siku.
Itokee kwa wiki au baada ya wiki 2.
Pressure cooker nitanunua hii nikiichoka au ikiharibika.
Kwa sasa ni mkombozi wangu.
Ningekuwa napipaka makande ningepikia pia.