Namna nilivyofunga ndoa kwa harusi nzuri na kubwa (ya ndoto yangu) bila kuchangisha wala kukopa

Ujinga tuu...rudini katk asili zenu, achen kuiga uzungu, mwishoe mnaarbu mambo kwa kuendekeza udunia na uzungu...simply harusi ilitakiwa imalizikie uko ibadani ambapo mkishafunganishana mapete, bas kila mtu atawanyike arudi kwake huku ninyi mliooana mnaenda magetoni/nyumban kuifaid ndoa, hizo habar za maukumbi na mapicha picha hotelin ni mbwembwe zakijinga ambazo lengo lake ni kuwafuraisha watu kwa siku moja, uku wew ukipukutika pesa na kubaki mtupu zaid ya kumilik picha zisizo na maana.....

Kuna umuhimu wa sie african kuachana na hizi mbwembwe za masherehe yasiyo na maana, hasa ukiwa na akili timamu na mwenye uchungu wa pesa, ni lazma ujue kusave money kwa kupuuza na kuachana na mambo yasiyo ya msingi il kupata furaha ya siku moja, mimi hata nikichangiwa pesa ya kufanya shughuri ya harusi, nitaandaa kamati alafu itakuja na majibu kiwa pesa zote nikafanye mtaji, na wote mliotoa.

Asanteni kwa Moyo wenu muendelee hivo hivo, but siku ya harusi tukutane kanisan/msikitini mapema sana saa3 asubuh alafu saa4 kila mtu aendelee na mishe zake za muhimu, hakuna hata kupoteza muda, siku hiyo hata mm nktoka kumvisha pete mtoto wa watu mchana wake nitaenda shamba kuandaa mavuno...hakuna kuendekeza ujinga[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Aah, hayo ni makubaliano na babe wako. Huku kwetu wazazi hawaelewagi hilo. Kwanza utasikia fulan mchoyo ametuonaje asitushirikishe kwenye shughuli ya mwanaye.
Wakati wa kulipa madeni watawasaidia?
 
Kwa jinsi nisivyopenda kuchangishwa na mtu ambaye unakuta hatukuwa hata na mawasiliano miaka, mimi pia sichangishi.. unless to my very close circle nao watakuwa huru ili wasione nimejitenga kwak
 
Hahahah daah sawa
 
Hiyo harusi yako ilikua ya gharama sana asieee
 
hiyo harusi yako ilikua ya gharama sana asieee
Jumla haikuzidi milioni 2.5 nimesema haikuwa ya gharama sababu nililinganisha na zile za bajeti ya milioni 15-40. Ila ukilinganisha na harusi za laki tano ni sahihi yangu ilikuwa ya juu
 
Mimi ktk harusi yangu sikuwa na Deni.
1. Nililipia ukumbi 2,000,000
2. Nililipia Mc na Mziki 1,000,000
3. Nililipia Picha na Video 700,000
4. Nililipia Usafiri kwa ujumla 1,000,000

Wazazi na familia walideal na mapambo 1800,000 na vinywaji 4,000,000.

Mchango wa kadi single na double 30,000 tu. Pesa za waalikwa ni kwaajili ya msosi.

Nilipata zawad nyingi Sana na pesa nyingi za zawadi. Ilibidi kukodi fuso kubeba.

NB: JIPANGENI MNAOTARAJIA KUOA. MSITEGEMEE MICHANGO. MWISHO HARUSI SI MSIBA
 
Umemaliza kabisa kaka, hongera mno
 
Wasalaam,

Kuna wadau wanaumizwa sana na madeni ya harusi baada ya kufunga ndoa, inampelekea mtu mpaka muda wa miaka minne akilipa tu deni la harusi ya ndoa yake.
Kwa hizo gharama zote huwezi kusema ulifanya harusi ya bei rahisi! Sijajumlisha gharama zote ila kwa haraka hazipungui 5M hizo hela.

So still ni harusi ya gharama endapo ukijumlisha na hela ya mahari!
 
Hiki ndicho kinawakwamisha watoto wa sikuhizi mnaozea makwenu😂 yani unakuta kufanya majukumu ya mke mtu hawezi ila anataka harusi ya 40M
 
Mie pia ndoto zangu ni kuoa bila kuomba michango! Nataka nikakodi sehemu tu ambayo ni setup ya venue yenye mapambo tayari na ma buffet! Kiongezeke mpiga picha na MC tu
 
Kama hujui mkuu hao jamaa ndiyo wanaongoza kwa kufanya harusi za gharama kubwa, fuatilia vizuri. Mimi hapo sijatumia hata zaidi ya milioni 2.5
Itakuwa una shida ya hesabu mkuu malaki yote hayo useme harusi ni 2M
 
Halafu boda anakuja kujilia bure
 
Hii kama Lulu na majizzo 😂 sema kwa mtu wa kawaida utaonekana bahili na wana ndugu watakupondea sana ila kwa watu wenye pesa inaonekana uzungu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…