Namna nilivyofunga ndoa kwa harusi nzuri na kubwa (ya ndoto yangu) bila kuchangisha wala kukopa

Tutafute hela jamani ....mambo ya kufanya sherehe ya harusi kama birthday haikubaliki kwetu..... tunaishi mara moja tu
 
Mimi sina ela na katika harusi yangu nimepanga nitumie laki 5 Tu Kwa watu 20 nguo zote zitakodishwa Mimi na mke wangu wasaidizi nao ivyoivyo Kama ikiwa lazima Ila japo sioni ulazima siowi kumfurahisha mama wala Baba wala mjomba wala Bibi naowa kwaajili ya maisha yangu mwenyewe kama uyo. Mwanamke akikataa wala sitalazimaisha mapema snaa naachana naye
 
Shela unakodi ila suti zenu nunua tu za elfu 80, ni sawa na kukodi.
 
Kwa hizo gharama zote huwezi kusema ulifanya harusi ya bei rahisi! Sijajumlisha gharama zote ila kwa haraka hazipungui 5M hizo hela.

So still ni harusi ya gharama endapo ukijumlisha na hela ya mahari!
Nilishajumlisha ni milioni 2 na laki 3
 
Gharama zote Hizo..? Ngoja Waje Watani zetu Wapare wakupe dondoo Muhimu Kwenye Kubana Bajeti Ya harusi..!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji16]wapareee.
Lengo la jamaa ni kutochangisha watu wala kuachiwa madeni, amefaulu sana
 
Wasalaam,

Kuna wadau wanaumizwa sana na madeni ya harusi baada ya kufunga ndoa, inampelekea mtu mpaka muda wa miaka minne akilipa tu deni la harusi ya ndo
Hiyo gharama ni kubwa sana
kama wewe ni msabato unafunga ndoa siku ya ibada, mkimaliza hapo nyie wanne mnakutana sehemu mnakula wali na soda shughuli imeisha
 
Hapo nakuunga mkono kijana mwenzangu,tena ukimuona mwenye kutaka makubwa zaidi ya kipato chako ujue huyo ni pasua kichwa kwako,mke mzuri ni yule ambae unapanga nae jambo lililo ndani ya uwezo wenu,Safi sana kwa huo msimamo wako
 
Hiyo gharama ni kubwa sana
kama wewe ni msabato unafunga ndoa siku ya ibada, mkimaliza hapo nyie wanne mnakutana sehemu mnakula wali na soda shughuli imeisha
Kweli kabisa,lazima twende na hali halisi ya uchumi ilivyo
 
Nitafanya sherehe nikiwa na doo tuu, kama sivyo sintofanya huo ujuha wa kufurahisha mijitu afu mi nibaki na maumivu.
 
Naomba msaada wako wa kuniunga nae mpiga picha na video.....mwisho wa mwaka nina jambo langu nalifanya
 
Kila nikimuambia twende kwa DC hataki.

Sasa mishe zenyewe hazisomi ananiambia atanisubiri mpaka zinyooke. Mimi siamini kwakua recently nimeanza kuota anachepuka
Kuna jambo la kukushauri hapa kama unaweza kufanya ni bora ukajua hatima yako kuliko kupotezeana nae muda,kama demu uwezo anao basi akuwezeshe kipesa ufanye hata biashara ama kama anauchungu na wewe basi ajiongeze kipindi iki ili baadae mishe zako zikikaa vizuri basi fresh tu,mpaka hapo kama yupo kiupendo kweli kwako basi utamuona tu
 
Madai yake ni kwamba kufunga ndoa kwa DC siyo sahihi Mungu haitambui
 
Naomba msaada wako wa kuniunga nae mpiga picha na video.....mwisho wa mwaka nina jambo langu nalifanya
Ni watu wawili tofauti, ukiwa tayari nicheki inbox nikuelekeze kwao.
 
Plus mahari pengine umetumia zaidi ya 10M.

Mbona maisha magumu jamani? Kuoa pesa. Kujenga ndiyo usiguse.

Corolla kwa 1M unapata. Dah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…