Namna nilivyoondoka nyumbani Kwa wazee mpaka kujitegemea

Namna nilivyoondoka nyumbani Kwa wazee mpaka kujitegemea

Doto12

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2023
Posts
787
Reaction score
1,394
Mnamo miaka kadhaa huko nyumba nilisoma sekondari nikiwa naishi Kwa ndgu. Sehemu ya makazi ya ndugu wale ninzaidi ya kilometa tatu. Nilivumilia mwaka mmoja mwaka wa pili nikahamia kwa Mzee ambaye tulikuwa na ukaribu upande wa mama.

Tumuite Mzee Hasan, Mzee wangu huyu alikuwa akiishi peke yake na wapangaji, mke wa mzee Hasan aliishi kijijini alikuwa anakuja mara moja moja. Ni mama angu aliyeongea na Mzee Hasan nikapewa chumba kimoja na kitanda cha kukunja. Nadhani vitanda vya namna Ile ni aidha vya mashirika ya usafirishaji. Maana ni kama unaweza ukasafiri ukakitumia.

Niliishi hapo na kumaliza masomo salama. Nilikiwa mtu wa mungu Ibada haikunipita. Siku moja Kuna mama ntilie mmoja nilikiwa napata mlo maneno hayo, na ucha mungu wangu shetani akaja na tabia zake nikalala na yule mama ntilie. Sasa katika majirani Kuna mama mmoja ana mtoto mmoja mumewe aliishi jijini Arusha. Tuseme tu alimtelekeza. Huyu mama siku moja alinisumbua sana usiku.. doto njoo, doto njoo njoo, nikaona isiwe tabu nikaenda akasema nilale pembeni yake nikamla, sikupenda kitendo kile nikapotezea mazima.

Shule iliisha salama nikarejea home matokeo si haba nikachagukiwa kantalamba. Kufupisha stori shule ya five na six ikaisha. Enzi Ile unakaa muda kabla ya kuingia chuo. Nikapata kishule nikapiga kazi pale mshahara 40k Kwa mwezi...nikiwa geto chafuchafu la kitanda, godoro na stuli. Kuna jamaa angu fundi magari alinipa redio flan nikawa mtu wa BBC na enzi Ile redio mawingu ilikuwa inabamba hadi kuitwa clouds. Hunikosi kipindi cha fina mango na masudi. Hakina redio utaniambia, labda kidooogo RFA.

Maisha yakasonga nikaingia chuo boom! Maisha mazuri ghetto langu likawaka, mademu kama kawa. Baada kumaliza chuo niliuza vitu. Nikahamia ghetto la jamaa angu chamazi. Jamaa alikuwa anafanyakazi Azam pale mfugale.

Tukiwa vinginguti nikapata kashuke nikawa najibanza hapo mshahara chai na lanchi.

Jamaa anasimamia show ya Kodi na sometimes msosi. Mwaka ukakata jamaa akaonesha dalili za kunichoka, kabla hatujalala alikuwa anahesabu hela zake na kabla hajaondoka kazini anahesabu.

Maisha yalikatika nikapata kazi TFDA, ila nje ya mkoa, nilikwenda nikapokelewa ila nikarudi kwanza kujiandaa. Jamaa angu hapo ghetto alishafikia maamuzi. Akahama wakati nikiwa safarini Mkoani.

Nilivyorudi aliniachia box na chandarua na nguo zangu zikining'inia kwenye misumali ya mlango na begi. Sasa si unajua chumba mtu akihama kinakuwa kichafu basi vuta picha.

Ile kitu iliniuma sana. Nikalala kwenye box. Kesho yake nikasafiri kwenda kazini kianza maisha upya mkoani. Nilifanikiwa kununua kila kitu muhimu huko na nikaanza maisha na familia. Ikumbukwe home naenda mara moja moja.

Udhalilishaji alionifanyia jamaa ulinikera sana lkn ndio mshahara wa wapenda kitonga mani nikiwemo.

Hangaika huku na kule nikahamia jijini Mwanza. Mke wangu ni msukuma, tukayajenga tukaamza maisha, yule bwana mkubwa akaanza kujileta leta mara apige simu.

Itaendelea.
 
Back
Top Bottom