Merci
Member
- Feb 6, 2012
- 92
- 138
Kwa kuzingatia yakua machinga na wafanya biashara ndogo ndogo nao huchangia katika pato la Taifa na la kwao moja kwa moja, ni vema kufikiria na kuweka njia nzuri ambayo itawafanya waendelee kutumia maeneo hayo kwa shughuri zao za kiuchumi.
Mfano, unakuta migambo na askari wa jiji wakipambana kuwaondoa na hata kuharibu bidhaa za wananchi wenzetu hawa ambao walipambana sana kupata mitaji kwa kisa tu eti hawako maeneo rasmi?!
Nashauri tutumie mbinu mbadala za kuhakikisha maeneo hayo yaliyo pembezoni mwa barabara na yale yasiyo rasmi yakitumiwa na machinga kwa nyakati za kuanzia jioni hadi usiku kwa kuhakikisha kuna kuwa na vibanda vizuri ambavyo vinahamishika kiurahisi kama inavyojionyesha kwenye video hii.
Jambo hili litafanya machinga waendelea kujumuika katika kukuza uchumi wa nchi na wa familia zao maana "hakuna maendeleo bila sisi wote kwa ujumla". Maendeleo makubwa huletwa na fikra zilizo nje ya hali ya kawaida iliozoeleka.