SoC04 Namna Tanzania inavyoweza kuzalisha wataalamu bora katika vyuo vya sayansi na teknolojia nchini

SoC04 Namna Tanzania inavyoweza kuzalisha wataalamu bora katika vyuo vya sayansi na teknolojia nchini

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mwenda Heaven

Member
Joined
May 14, 2024
Posts
6
Reaction score
4
Tanzania tumekuwa na vyuo vikuu mbali mbali lakini bado hatufanyi vizuri kimataifa na kuzalisha wanasayansi ambao wanategemea kusubiri ajira na sio kugundua mambo.

Hivyo serikali inatakiwa kuhakikisha inasimamia kikamilifu namna ambavyo elimu hiyo hutolewa. Mfano. Mwalimu anapotoa assigment kwa nia njema ya kumjenga mwanafunzi, mwanafunzi huyo anaenda kumlipa mtu mwingine amfanyie, hii inamfanya mwanafunzi huyu kuwa na degree ambayo hana maarifa nayo.

vile vile katika Tafiti za kielimu(Academic researches)... Wasomi wanakuwa wakifanyiwa Tafiti kiasi kwamba wanapopewa nafasi serikalini au katika taasisi wanashindwa waanzie wapi.

hivyo ningependa kuishauri mamlaka inayohusika kuhakikisha wanadhibiti vitendo kama hivi ili tupate wasomi wenye maarifa sahihi na wanaoweza kuijenga Tanzania tuitakayo.

HAYA NI BAADHI YA MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA BAADA YA KUZALISHA VIJANA WASIOMAHIRI.

1. Kuwa na utendaji kazi dhaifu katika maeneo watakayo ajiriwa, mfano kama ni Mhandisi (engineer) atakuwa sio mahiri maana yake atashindwa kufanya kazi kwa ufasaha.

2. Kushindwa kutoa maamuzi sahihi katika utatuzi wa jambo. Hii inakuja baada ya huyu mtaalamu kuaminiwa na serikali au taasisi yeyote ile kutatua jambo fulani, na anapokuwa na uelewa wakubabaisha juu ya hilo jambo inaleta shida katika utatuzi wake.

3. Kukwamisha maendeleo kwa taifa. Endapo mtu aliyehitimu mafunzo katika chuo chochote cha sayansi na teknolojia matarajio ni kwamba mtu huyu ana maarifa ya kutosha kufanya jambo fulani lakini kumbe alikuwa ananunua kazi au kulipa watu wamfanyie ndipo afaulu... Hapo mtu asiyesahihi atakabidhiwa mradi na asifanye chochote.

4. Pia katika sekta ya afya tutapata madaktari wasio mahiri na kushindwa kuihudumia jamii.

5. Katika suala zima la kufanyiana/kununua tafiti vyuo vikuu hii itasababisha kutengeneza wataalamu ambao hawalijui tatizo na wala hawawezi kukabiliana nalo

MAPENDEKEZO.
Ninapendekeza kuwa kazi zitolewazo kwa wanafunzi kama assigments, Group discussions zinapokuwa zinawasilishwa mwanafunzi anatakiwa kama ni kufanya afanye pale pale mbele ya msimamizi na atakaposhindwa akafanye tena na sio kupewa maksi ndogo.(Hapa ni katika mlengo wa kujifunza kwa vitendo.)
Vile vile katika kuwasilisha kazi za kuandika mwanafunzi anatakiwa kusimama bila kuwa na kazi yake (awe tu na list note) ya kumwongoza kueleza kipengele hadi kipengele.

Pia ninashauri Kuwepo na rooms maalum kwaajili ya kufanya Individual assigments ili kuweza kumsimamia mwanafunzi afanye vizuri..... na kama ni kuchukua maarifa sehemu mbali mbali ajadiliane na wenzake na afanye na sio kuchukua kazi za watu wengine/kufanyiwa kazi na kujipatia alama.


MWISHO.
Niishukuru serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha mazingira ya vyuo vikuu nchini.
 
Upvote 6
huyo anaenda kumlipa mtu mwingine amfanyie, hii inamfanya mwanafunzi huyu kuwa na degree ambayo hana maarifa nayo.

vile vile katika Tafiti za kielimu(Academic researches)... Wasomi wanakuwa wakifanyiwa Tafiti kiasi kwamba wanapopewa nafasi serikalini au katika taasisi wanashindwa waanzie wapi.
Sasa hivi tunazo na AI, japo kwa upande mwingine ukiangalia, uwezo wa kutambua wenye akili zaidi yao na kuwatumia kufanikisha lengo nayo ni akili broh ujueee....
 
Back
Top Bottom