SoC01 Namna vijana wanavyoweza kushiriki/kushirikishwa katika shughuli za maendeleo kitaifa

SoC01 Namna vijana wanavyoweza kushiriki/kushirikishwa katika shughuli za maendeleo kitaifa

Stories of Change - 2021 Competition

Saema

New Member
Joined
Jul 18, 2021
Posts
2
Reaction score
0
Hebu fikiria, umepata nafasi ya kuzungumza ana kwa ana na Mh Samia Suluhu (Rais wa JMT) na una dakika tatu tu za kueleza nini ungetamani afanye ambacho kitakufaidi wewe (Kijana) na vijana wengine. Kwa dakika tatu hizo ungemweleza nini?

Bila shaka umepata jibu. Hii inaonesha kuwa kila mtu ana wazo maridadi la kimaendeleo lakini wengi hawaoni namna ya kulifikisha katika meza ya wafanya maamuzi.

Takwimu zinaonesha 66% ya nguvu kazi ya taifa ni vijana kati ya 15-35. Hii ni idadi kubwa kihistoria ambayo ni vigumu kujirudia.

Hivyo ni uamuzi wetu kama taifa kuamua mambo mawili;
1. Tuwekeze katika kizazi hiki na kukiwezesha kufanyika wanamabadiliko chanya kwa Tanzania bora ya baadaye, au
2. Tupuuze kizazi hiki na idadi yake kubwa na kutia giza nene kwa Tanzania ya baadaye.

Uhusishwaji na ushikishwaji wa Vijana katika mipango na utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinazowahusu ndio nguzo pekee inayoweza kusaidia kuvuna nguvu, vipaji na uwezo ulio ndani yao. Changamoto inakuwa kubwa pale Vijana wanapoonekana kama vile ni wapokeaji wa chakula kilichoandaliwa na serikali. Vijana wanatakiwa kushirikiana na serikali kuandaa chakula kwa pamoja. Hii ni pamoja na uundwaji, mapitio, na utekelezaji wa sera zinazohusu maendeleo ya Vijana. Vijana sio wa kusemelewa, wanatakiwa kusikilizwa sauti zao moja kwa moja na kuona zinafanyiwa kazi. Nyenzo hii isipotumika vizuri, ndipo kunaibuka kulaumiana; serikali inasema Vijana ni wavivu hawawezi kujiajiri na Vijana wanasema serikali haiwasaidii. Ili kufanikiwa katika ushirikishwaji huu mambo yafuatayo lazima yazingatiwe;

1. Kuboresha muingiliano wa kisekta: Hebu fikiria mfano Kijana anayelima mchele kijijini Morogoro lakini kiwanda kipo Mwanza mfano. Tunaposema Vijana wajiajiri kupitia kilimo sio suala la kusema tu, lazima tuhakikishe sekta ya viwanda na sekta ya kilimo zimeunganika, miundombinu ya usafirishaji iwe rafiki na bajeti ya serikali iangazie u-kisasa wa pembejeo. Ni ngumu sana Kijana wa Shahada kushika jembe la mkono.

2. Kuimarisha teknolojia ya mawasiliano: Ni ukweli usiopingika kuwa mambo mengi sasa yanaingia kwenye ulimwengu wa kidijitali, COVID-19 imedhihirisha hilo; watu wamegundua kumbe wanaweza kufanyia kazi nyumbani na bado wakafikia malengo ya kampuni, kwa nini tukodi jengo la mamilioni kama ofisi wakati tukiwa nyumbani tunaweza kufikia malengo? Mambo kama haya yanatufanya tuone kuwa muda si mrefu kila kitu kitaenda kimtandao. Biashara, elimu ya afya, usafirishaji, n.k, ni baadhi ya mambo yakayokwenda online kwa kasi. Swali ni je, Vijana hawa mamilioni, wameandaliwa kutumia teknolojia ya habari kwa manufaa? Je STEM zinafika shule zote haswa za kijijini? Je, sheria za mtandao za nchi yetu zinampa mtumiaji uhuru wa kuwa mbunifu? Ifike mahali sasa masomo ya computer shule za msingi na sekondari yawe lazima.

3. Taarifa kwa wakati: Ni Vijana wangapi wanajua kuwa kuna kitu kinaitwa mfuko wa maendeleo wa Vijana katika kila halmashauri ambao hutoa mikopo kwa Vijana? Mwaka wa fedha 2020/2021 mfano serikali ilitoa shilingi Bilioni 9.5 kama mikopo kwa Vijana kupitia halmashauri. Swali ni je, Vijana wote wana taarifa juu ya mfuko huu? namaanisha Vijana waishio vijijini, wenye ulemavu, wasiosoma, wasio na kipato, wasichana, n.k Je Vijana hawa wanatambua namna ya kukidhi masharti mfano ujuzi wa kuandaa katiba ya kikundi? Haya ni baadhi ya maswali ya muhimu ya kujiuliza Mfuko unaweza kuwa upo lakini hauwafikii Vijana wote kwa usawa. Lazima kuwe na mfumo wa ushirikishwaji wa kina haswa maafisa maendeleo wa hamlashauri wasikae tu ofisini, watoke kupeleka elimu hii kwa vijana, maana ni haki yao.

Asanteni.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom