Uzoefu wangu kama Mtanzania anayeishi ughaibuni. Watanzania na Wakenya wapo karibu sana, Waganda wamejitenga (nadhani sababu ya Kiswahili). Wakenya kwa Wakenya kuwa marafiki baina yao hadi wawe wanatokea kabila moja, Watanzania huwa 'buffer zone' kati ya makabila tofauti ya Kenya. Karamu ya Watanzania utakuta Wakenya wengi na karamu ya Wakenya utakuta Watanzania wengi.Wanyarwanda wanaojua Kiswahili wapo karibu zaidi na Wakenya na Watanzania.
Kuhusu uchapakazi, sote ni wachapakazi kwa kuwa tupo nje ya nyumbani na hakuna mjomba wa kukusaidia. Kuhusu hili la uchapakazi, wageni popote duniani huwa wachapakazi kuliko wenyeji kutokana na 'do or die factor'.
Tabia zingine kama kufuatiliana sana, unafiki wa hapa na pale na umbea hizi zipo kwa jamii zote nilizokutana nazo, kuanzia Waafrika, Wazungu na Waasia.
Wasichana/ wanawake wa Kenya wanapenda Wabongo sababu ya ukarimu wetu (nadhani na udadisi wa kawaida wa binadamu).
Warundi siwajui vizuri kutokana na kutokuwa na mwingiliano sana na wao.