Namna wanahabari wanavyoharibu lugha ya Kiswahili

Haya mambo tumeyasoma shule, tena primary. Lakini watu wakimaliza mtihani basi wanasahau. Kizazi cha sasa ni bure kabisa. Lugha za makabila ziro, Kiingereza ziro, Kiswahili ziro!!!
Kiswahili ni kipana sana na kitamu. Niliwahi kusoma mahala matumizi na tofauti ya maneno 'ndio' na 'ndiyo' pia 'sio' na 'siyo'. Maneno ambayo tunayatumia tu bila kujali usahihi wa matumizi yake
 
Hatuna lugha, hatuna utamaduni...tumekuwa Taifa lisilojua kwao.
 
Kwan matumizi ya lugha n nn?si kufanikisha mawasiliano baina ya watu..sasa kama alichodhamiria mtu kukisema mm nimekielewa hayo mengine yananisaidia nn..namrekebisha tu mambo mengine yaende

Na hakuna ambaye ni mkamilifu ktk lugha..tuvumiliane tu
 
Ingekuwa simplistic hivyo, kungekuwa na haja gani ya kwenda shule na kujifunza lugha? Utakuwa chinga wewe!!
Kwan matumizi ya lugha n nn?si kufanikisha mawasiliano baina ya watu..sasa kama alichodhamiria mtu kukisema mm nimekielewa hayo mengine yananisaidia nn..namrekebisha tu mambo mengine yaende

Na hakuna ambaye ni mkamilifu ktk lugha..tuvumiliane tu
 
Haya mambo tumeyasoma shule, tena primary. Lakini watu wakimaliza mtihani basi wanasahau. Kizazi cha sasa ni bure kabisa. Lugha za makabila ziro, Kiingereza ziro, Kiswahili ziro!!!
Karibu tuungane kuiokoa lugha yetu adhimu
 
Baadhi yao hutangaza.... "mtu mmoja ameweza kufariki na wengine... kujeruhiwa"!!!
 
Mbaka..... Mpaka
Nimemdhibiti.... Nimemzibiti
 
Alusi badala ya Harusi.

Mwingine ana andika ela badala ya hela huku akiamini kua, kuandika hivyo ndio kwenda na wakati,mimi hua najiuliza,hivi na huko ofisini au Shuleni hua wana andika hivyo?
 
Kiswahili ni kipana sana na kitamu. Niliwahi kusoma mahala matumizi na tofauti ya maneno 'ndio' na 'ndiyo' pia 'sio' na 'siyo'. Maneno ambayo tunayatumia tu bila kujali usahihi wa matumizi yake

Unataka kuniambia kuwa katika lugha ya Kiswahili kuna neno "ndio" na "sio?
 
Baadhi yao hutangaza.... "mtu mmoja ameweza kufariki na wengine... kujeruhiwa"!!!
Huwa nashangaa sana kiswahili hicho utadhani alikuwa anashindana au alikuwa ana nia ya kufa hivyo amefanikiwa alichokuwa anakitaka!!!!
 
Watanzania hatuko makini na vitu vya msingi.

Halafu watu wamekuwa ni wabishi hawataki kukosolewa.
 
Na waimbaji wa bongoflava nao ni majanga, hasa kubadili penye l kuweka r na kinyume chake.
 
Kuna gazeti moja la Mtanzania ndio walikuwa kinara wa kuharibu Kiswahili, wahariri walishindwa kutofautisha wapi watumie 'ha' na wapi watumie 'a'.

Huwa najiuliza hivi hawa waandishi wa habari na wahariri wao walisomea nchi gani, tumefika mahali kizazi hiki Kiswahili hawajui na Kiimgereza nacho ni taabu vilevile. Kiswahili kinatishiwa na uharibifu kuliko wakati mwingine wowote.

Vv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…