Kuchagia!! Nakutania mkuu usijali.Naogopa kuchagia. Nikikosea hapa mtaanza na mimi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuchagia!! Nakutania mkuu usijali.Naogopa kuchagia. Nikikosea hapa mtaanza na mimi.
hauko sahihi=you are wrongTuliza akili ndugu utaelewa tu,
Uko sahihi= you're right
Huko sahihi= you're not
Bila kuanzia kwa viongozi wa CCM Baraza la Kiswahili litatuzibia masikio, kiswahili lazima kianzie kwa viongozi wa juu wa CCM.Sahihi! Karibu tuungane kuiokoa lugha yetu adhimu
Wanaonikera zaidi ni wanaotumia "ga" "ge" "gi" mfano "alikwendaga" badala ya "alikwenda" "sielewagi" badala ya "sielewi"Tena utakuta mwingine kasoma kiswahili mpaka ngazi ya shahada lakini uandishi wake ndio huo
Watu wa kigoma,Bukoba na Mara wana lafudhi za hovyo sana wanatupa kazi ngumu sisi Wanapwani/wajuvi wa kiswahili kuwarekebisha.nakura kwanza nikishiba naenda kupiga kula
Daah
Mzaramo akikosea kuongea kisambaa sio tatizo. Tatizo ni msambaa akikosea kisambaa.Nadhani kwa ukanda wa Afrika ya Mashariki, Kenya wanaongoza kwa kuongea kiswahili kibovu!
Ahueni Watanzania tuna unafuu! Ingawa ni kweli, tuna changamoto.
UkiPOOZA koo si ni paralysis hii???Wengine wanashindwa kutofautisha neno POZA na POOZA, utasikia "nataka kupooza koo"
Zote ni sahihi.Madawa ya kulevya badala ya Dawa za kulevya.
Dawa haina wingi,huwezi kusema Madawa,Zote ni sahihi.
Neno "madawa" hutumika kutia msisitizo wa jinsi gani hizo dawa ni mbaya na zisizofaa.
"Dawa za kulevya" ni neno ambalo si kali sana. Na linaweza kutumika pia kulingana na muktadha au namna ambavyo muwasilishaji anataka kutia uzito ujumbe wake.
Nyambafu!!xafi xana mleta mada
Wengi sana wanafanya hivo, fuatilia wachambuzi wa mpiraSentensi 2 hivi kuna mtu anayejua kiswahili anaweza andika hivi kuchanganya ngeli kiasi hiki
Ndiyo ila wachambuzi wa mpira wamekuwa wakitumia neno POOZA wakimaanisha freezingUkiPOOZA koo si ni paralysis hii???
Hahahaaa
Inasikitisha ndio maana naanza kukumbuka walimu wa kiswahili walivyokuwa wanatilia maanani ngeliWengi sana wanafanya hivo, fuatilia wachambuzi wa mpira
Watu wa pwani mnanikera sana pale mnaposhindwa kutofautisha matumizi ya BAADA na BADALA, utasikia mzaramo anasema " baada atoe pasi anajivuta tu"Watu wa kigoma,Bukoba na Mara wana lafudhi za hovyo sana wanatupa kazi ngumu sisi Wanapwani/wajuvi wa kiswahili kuwarekebisha.
Karibu tuungane kuiokoa lugha yetu adhimuHili jambo nadhani usiishie kuwaangazia tu hao wachambuzi ila tuliweke Kitaifa. Kuna kaumbumbumbu ka kijinga sana kanaendelea ndani ya Taifa lwtu hili halafu wao wanajiona wako sahihi muda wote!
Mfano mtu anakwambia Mbaka badala ya Mpaka au anakuambia Ndakwambia badala ya Nitakuambia. Au wale wanaoweka x badala ya s.
Nazidi kumuelewa mzee Mkapa aliposema kuna haja ya kuangalia mustakabali wa elimu yetu. Tena hawa wanafunzi wa vyuoni wengi wao ndio Wapumbavu wahed kabisa katika kuzungumza na kuandika kiswahili. Unakuta hawezi kukiongea kiswahili wala hawezi kuongea kiingereza wanachotambia na maneno yao mawili mawili.