Namna wanahabari wanavyoharibu lugha ya Kiswahili

Namna wanahabari wanavyoharibu lugha ya Kiswahili

Kuna gazeti moja la Mtanzania ndio walikuwa kinara wa kuharibu Kiswahili, wahariri walishindwa kutofautisha wapi watumie 'ha' na wapi watumie 'a'.

Huwa najiuliza hivi hawa waandishi wa habari na wahariri wao walisomea nchi gani, tumefika mahali kizazi hiki Kiswahili hawajui na Kiimgereza nacho ni taabu vilevile. Kiswahili kinatishiwa na uharibifu kuliko wakati mwingine wowote.

Vv
Bado tuna safari ndefu sana na tutafika tukiwa tumechoka sana
 
Wengi ni vilaza waganga njaa tu
 
Utawasikia baadhi yao wakiwa studio nanukuu " Ali Kiba ametoa 'nyimbo' kali sana" mwisho wa kunukuu✍️

Halafu cocastic na kampani yako, acheni mara moja kutumia hili neno "tyuu" !! Kwani ugumu uko wapi kutumia neno hili 'tu'?
kuna wale wamichezo na uchambuz wao wa kule Planet ...shida tupu!
 
Miaka ya hivi karibuni limeibuka wimbi kubwa la uharibifu wa lugha ya kiswahili (nchini Tanzania). Baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha matumizi sahihi ya kiswahili ama kwa kujua au kwa kutokujua kama wanakosea.

Kumeibuka dosari nyingi katika uandishi na utamkaji wa baadhi ya maneno ya kiswahili. Mathalani, baadhi ya watu wanafanya substitution na omission kwenye baadhi ya maneno. Kwa mfano, utasikia/ona mtu ameandika
Hasubuhi badala ya asubuhi,
Hafadhali badala ya afadhali,
Hamka badala ya amka,
Hendelea badala ya endelea,
Humoja badala ya umoja,
Bahadhi badala ya baadhi, yani wana
substitute sound /h/ kwenye sound /a/.

Hali kadhalika wanafanya omission kwenye baadhi ya maneno mfano,
Ela badala ya hela
Alafu badala ya halafu
Angaika badala ya hangaika
Abari badala ya habari, hapa wanafanya complete omission of sound /h/. Makosa ni mengi sana na mbaya zaidi wanaofanya hivyo wengi wao hufanya makusudi wakichukulia kuwa ni swaga kumbe shit.

Sasa turudi kwa wana habari,
Nikiwa kama mfuatiliaji mkubwa wa habari za michezo, kuna baadhi ya wachambuzi hasa kwenye channel yetu pendwa wamekuwa wakinikata mood kutokana na uharibifu wa lugha ya kiswahili wanaoufanya. Inawezekana wanakosea kutokana na haraka wanayokuwanayo wakati wa kuchambua soka, hata hivyo kama baadhi yao watabahatika kupitia uzi huu basi ni vema wajirekebishe.

Sio ajabu kusikia mchambuzi akisema sentensi hizi;
1. Miongoni mwa kitu ambacho kocha amefanikiwa...
2. Jonas Mkude ni miongoni mwa mchezaji ambaye...
3. Moja ya kitu ambacho...

Tukianza na sentensi ya kwanza, neno miongoni linatumika kutaja kitu kimoja kati ya vingi, sentensi ya pili vilevile.

Sentensi ya tatu nayo ina dosari kubwa, unaposema 'moja ya' tunakusudia kuona idadi kubwa ya vitu ambapo hicho kimoja ulichokitaja ni exceptional.

Kwa minajili hiyo basi, sentensi hizo hapo juu usahihi wake ni huu ufuatao;

1. Miongoni mwa vitu ambavyo kocha amefanikiwa...
2. Jonas Mkude ni miongoni mwa wachezaji ambao...
3. Moja ya vitu ambavyo...

Lengo la kusoma ni kuelimika na tunapoelimika hatuna budi kuielimisha jamii.
Mimi nimetimiza wajibu wangu sasa ni zamu yako,
Naomba kuwasilisha.

na wale wamatumizi ya L kwenye R mfano barabara wao watasema balabala habari/ habali wamerudi/ wameludi
 
Unataka kuniambia kuwa katika lugha ya Kiswahili kuna neno "ndio" na "sio?
Ndiyo na nakuandikia na mifano kabisa hapa chini


Ndio= wingi wa ndiye
Mfano "Huyu ndiye aliyekula" (umoja)
"Hawa ndio waliokula" (wingi)

Sio= wingi wa siye (yaani kinyume cha ndio)
Mfano "Huyu siyeninayemtaka" (umoja)
"Hawa sio ninaowataka" (wingi)

Kwahiyo
'Ndiye' wingi wake ni 'ndio' na ukanushi wake kwa ndiye ni 'siye' na kwa ndio ni 'sio'
 
Wengine eti 'hiko' badala ya 'hicho'. Hao wote ni waandishi wa habari waliojiriwa katika radio na TV stations mbalimbali.
 
Umechambua ya ndani sana. Mkuu kuna makosa mengine ya nje sana lakini mtu hajui kama anaharibu lugha yetu. Alipokuwa shule na hata anaposoma maandiko mbalimbali, kitabu kimeandikwa kwa mfano "dharau". Badala ya kusoma kilichoandikwa, atasoma "zarau". Jitu zima na ni msomi huyu. "Thelathini" atatamka "selasini". Jamani tutamke kadri ya maandishi. Kwani hugharimu shilingi ngapi kuzingatia matamshi kwa sahihi?
 
Ndiyo na nakuandikia na mifano kabisa hapa chini


Ndio= wingi wa ndiye
Mfano "Huyu ndiye aliyekula" (umoja)
"Hawa ndio waliokula" (wingi)

Sio= wingi wa siye (yaani kinyume cha ndio)
Mfano "Huyu siyeninayemtaka" (umoja)
"Hawa sio ninaowataka" (wingi)

Kwahiyo
'Ndiye' wingi wake ni 'ndio' na ukanushi wake kwa ndiye ni 'siye' na kwa ndio ni 'sio'
Kama mimi ndiye mwalimu wako hapa nakupa [emoji817]%
 
Wachambuzi wa soka wa redio fulani wananikera wanaposema "timu haikuweza kupata matokeo" wakimaanisha haijashinda.

Matokeo ya mchezo ni aidha kushinda, kushindwa au suluhu. Bure kabisa wachambuzi wa redio hii.
 
Tatizo ni serikali kupenda kufumbia macho masuala ya taaluma ya uandishi kwa kudhani wanalinda ajira kwa vijana kumbe wanabomoa
 
Back
Top Bottom