Namna Watanzania wanavyotapeliwa na Waganga wa Kienyeji nchini Kongo

Hi Ni nzuri nitasoma hii ila ile nyingine no plz utoniona kamwe

Tena harakisha Hadi jmos ikwishe hi[emoji120]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hiy

Hiyo nyingine ni ipi?
 
Haya mambo yakuchokozwa na kutukanwa na baadhi ya members humu halafu mimi nikimjibu nakula BAN sidhani kama imekaa sawa.Haiwezekani mtu anatoka huko anakokujua yeye anaanza kuniporomoshea matusi mazito halafu nimuangalie tu!.

Bado sijafikia kiwango hicho cha Utakatifu,kama ni nginja acha iwe nginja.

Wengine hatujaumbwa kuwa watukanaji,mimi nipo kuwaburudisha na kuwaelimisha hadhira yangu na umma wa watanzania wengi wanaojitambua,sasa anatokea mtu anaanza kukuporomoshea matusi ya nguoni kisa tu alikuja Inbox akaomba jambo fulani ukamnyima,ukimjibu kidogo tu anapelekea na wewe kufungiwa,hii siyo sawa moderators,wengine mnatuonea bila sababu ya msingi.

Kama nyuzi zangu zinakupa kero na huzipendi kwanini usipite ukatazame nyuzi zinazokufurahisha?,Kila mtu hapa anasoma anachoona kwake kina manufaa na anachokipenda,kama unaona hutaki usumbufu una-Block au Una - Ignore unaendelea na mishe zako,waachieni watu wanaotaka kujifunza na kuburudika wasome nyuzi zangu.

Hadhira yangu kwa muda wa siku zisizopungua 5 imeshindwa kupata simulizi nzuri na yenye mafunzo kwasababu tu ya watu fulani wajinga ambao hawataki kuniheshimu na kuanza kuniporomoshea matusi mazito,mimi kuwajibu imekuwa nongwa,hili halikubaliki hata kidogo moderators!.

Kuna muda tunachokozwa na kupandishwa hasira na wajinga kadhaa humu JF,sasa ajabu ni kwamba,mtu anapokutukana mara ya kwanza unamripoti hakuna hatua anayochukuliwa,mara ya pili pia ni vivyo hivyo,akikutukana mara ya tatu uzalendo unakushinda unamjibu,ukisha mjibu tu hapo ndipo Moderators wanakuja kuwaadhibu,wanashindwa kumuadhibu toka awali ulipomripoti wao wanakuja kumuadhibu ulipomjibu ambapo wanawaadhibu wote wanashindwa kumuadhibu mtoa matusi au muanzilishi wa matusi,hili halikubariki na nitaendelea kulipigia kelele.

Nimewahi kutoa mapendekezo kwenye uzi wangu mmoja uko kwenye Jukwaa la COMPLAINTS, APPRECIATION AND ADVICE(TO JF) nikasema tuwekeeni Blocking Button yenye nguvu na siyo hiyo Ignore iliyopo sasa,kwasababu kama nikishaona mtu ananitukana nitampiga Block ili aende akawatukane wazazi wake huko kwasababu wao ndiyo walimfundisha ujinga huo.

Aisee nimesikitishwa sana kupigwa BAN kwakosa ambalo limesabishwa na moja ya wapumbavu hapa JF.Wengine tunakiuka taratibu kwasababu ya kuchokozwa na siyo kwamba taratibu hatuzijui!.


Mimi ni mwema na nitaendelea kuwa mwema ila nikitukanwa lazima nijibu mapigo,kama ni kufungiwa nitafungiwa sana na nipo tayari kwa hilo!.

NIMESHINDWA KUSIMULIA STORI KWA SABABU YA WAJINGA KADHAA HAPA JF,HILI HALIKUBALIKI HATA KIDOGO NA NAUMIA SANA.

Huu ni ujumbe wenu Moderators najua uzi huu mnaupitia.


Ni hayo tu.
 
Mkuu karibu
Sisi kama fans wako tumekusubiria sana
Naomba tuendelee na story
 
SEHEMU YA NNE




Tulipanda kwenye zile bodaboda na safari ya kuelekea makaburini ili kazi ya kuanza kuaga mizimu ya mababu zetu wa kitanzania ichukue nafasi.Tulipofika jirani na lile eneo la makaburi,Jentre aliwaambia Bodaboda wasimame tushuke kisha watusubiri tukakamilishe jambo letu halafu tuondoke.

Tulipofika pale makaburini Jentre alituambia kila mtu atafute kaburi ambalo lilikuwa bado halijasakafiwa na ambalo bado lilikuwa halina siku nyingi tangu shughuli ya mazishi ifanyike.Baada ya kuwa kila mtu amepata kaburi lake,ndipo Jentre akatupa ishara ya kwamba tuvue nguo na tubaki kama tulivyozaliwa.

Jentre "Kamata hii"

Aliendelea "Naomba uniambie ndugu zako waolikwisha kufa"

Mimi "Babu,Baba wakubwa kadhaa,Bibi mzaa mama,mama wadogo pamoja na wajomba ikiwemo watoto na ndugu kadhaa"

Jentre "Sasa chukua hicho kijiti nilichokupatia kisha utahesabu kutoka miguuni mwa hili kaburi hatua kumi,kisha utachukua hicho kijiti utachimba hapohapo ulipofikia kuhesabu hatua zako hizo kumi"


Aliendelea "Hakikisha shimo utakalo chimba liwe saizi ya kiganja cha mkono wako"


Baada ya kutamka maneno hayo aliondoka kwangu akaelekea kwa Kamugisha ambaye alikuwa mbali kidogo na mimi,sasa mkononi Jentre alinipatia Pemba nyeupe pamoja na kijiti kidogo chenye makadirio kama Centimeter 15.Sasa kwenye Kaburi lolote lile huwa kuna ile sehemu ambayo misalaba huwekwa na kuandikwa majina,hapo mara zote huwa tunaita kichwani na kule ambako hakuna kibao cha majina wala msalaba huwa tunaita miguuni,sasa jamaa akawa ameniambia nichukue kile kijiti cha senitimita 15 alichokuwa amenipatia nikipime kuanzia sehemu ya miguu ya lile kaburi kwa hatua ya vijiti kumi,yaani Sentimita 150 kisha hapo katikati zitakapofikia hizo hatua za vijiti ndipo nichimbe kishimo kidogo ambacho nikizamisha kiganja cha mkono wangu kiishilie chote.

Hivyo ndivyo nilivyofanya na baada ya kumaliza niliendelea kuchuchumaa pale chini nikimsubiri aje anipe maelekezo ya kufanya;Alipomalizana na Kamugisha alinirudia ndipo akaanza kuniambia nitamke maneno kadhaa atakayonielekeza yeye.

Jentre "Naomba unifuatishe maneno haya,Babu zangu,Bibi zangu,wajomba zangu,ndugu zangu wote mliofikwa na mauti,kijana wenu ninarudi kwenu naombeni baraka zenu,nimekuja kuwaaga mimi nasafiri kuelekea Congo,hivyo ninaomba baraka zenu ili nivuke salama na nikafanikishe mambo yangu"

Baada ya kuyatamka maneno hayo na mimi niliyarudia kama alivyokuwa ameniambia,nilipomaliza kuyatamka maneno hayo alichukua ile pemba nyeupe aliyokuwa nayo mkononi akanipatia akaniambia niitupe kwenye kile kishimo nilichokuwa nimekichimba pamoja na kile kijiti kisha nifukie.

Jentre "Haya lizunguke hilo kaburi mara kumi ukirudi kinyumenyume"

Nilifanya kama alivyoniambia na baada ya kumaliza aliniambia nisimame niende nikavae nguo kisha nimsubiri akamlizane na Kamugisha kisha tuondoke zetu.Baada ya lile zoezi kuwa limekamilika kwa wote wawili,jamaa alitushika mikono kwa pamoja kisha akaanza kuongea maneno aliyokuwa akiyafahamu yeye kwa lugha ya Lingala na French.

Tulipomaliza huo mchakato tuliondoka zetu kurudi hotelini na jamaa yeye aliondoka kwenda kwake.

Asubuhi kulivyopambazuka Seif alimpigia simu Kamugisha na kumwambia inabidi tufanye harakati za kuvuka kwasababu ile Boti ambayo tulipaswa kuondoka nayo ilikuwa inaondoka baada ya kukamilisha zoezi la upakiaji wa mizigo.Tuliondoka tukaelekea zilipo ofisi za uhamiaji na kuacha documenti zetu pale tukaambiwa tutaletewa kwenye boti ambayo tulikuwa tukisafiri nayo.

Ilipofika muda wa saa 8 mchana,Seif alitubeba kwenye mtumbwi wake uliokuwa umefungwa injini kutuvusha kuelekea kisiwani ambako ndiko ile boti kubwa tuliyokuwa tunaondoka nayo ingetukuta hapo,kwenye ule mtumbwi wa Seif kulikuwa pia na abiria wengine ukiacha sisi.

Seif "Nawapeleka kwenye kile kisiwa pale,jamaa wanaenda kupakia mizigo mingine kwenye bandari ya Kipili,wakimaliza watawachukulia pale muondoke zenu!"

Kamugisha "Hakuna tatizo"


Kulikuwa kuna kisiwa kikubwa sana kinaitwa Mandakerege ambacho ndicho bwana Seif alituacha hapo akatuambia wale jamaa wa ile Boti wangemaliza kupakia mizigo pale bandari ya Kirando walikuwa wanaelekea bandari ya Kipili iliyokuwa kushoto mwa Kirando wakapakie mzigo mwingine kisha ndiyo tusepe zetu Congo.

Kwakuwa tuliambiwa ziwani tungekaa siku zaidi ya moja kulingana na hali ya hewa,tulichukua soda za kopo pamoja na maandazi ya kutosha kama dharura endapo kungetokea jambo lolote.Kiukweli ndugu zangu kwakuwa ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika ziwa Tanganyika na kuliona,asikwambie mtu si ziwa la kawaida hata kidogo,kwa wale waliofanikiwa kuliona hata kulipita watakubaliana nami!.

Ingawa wajuvi wa mambo ya majini wanasema ziwa lile lina unafuu mkubwa kuliko ziwa Victoria lakini mimi kwakuwa maziwa yote mawili nimeshayashuhudia kwa macho;kwa upande wangu ziwa Tanganyika ni hatari kuliko ziwa Victoria,nina maana yangu kusema hivyo.

Basi bhana,tulikaa pale Mandakerege hadi mida ya saa 11 jioni,baada ya ile boti kumaliza kupakia shehena ya mzigo pale Kipili ilikuja kutuchukua pale.Kiukweli sikuwahi kuona Boti limebeba shehena ya mzigo kama lile,nilipoliona kwanza nikaingiwa na hofu nikajikuta tu nauliza wenzangu!.

Mimi "Sasa lilivyojaza mzigo hivyo tutakaa wapi?,au kwachini kuna nafasi ya abiria kukaa?"

Jamaa mmoja "Ndiyo mara yako ya kwanza kusafiri nini!"

Mimi "Yes,hii ndiyo mara ya kwanza"

Jamaa "Abiria wote wanakaa juu ya huo mzigo"

Baada ya jamaa kuniambia vile nilitaka kabisa kugoma kupanda lile boti,roho yangu ilijaa hofu sana na kiukweli nilivyokuwa nikidhani ndivyo ilivyokuwa.Basi nilipiga moyo konde na nikajikaza kisabuni kijana wa Kikurya kisha baada ya kuitwa majina nikazama kwenye chombo.Ile boti ilikuwa imekula mzigo hadi ule mstari wa ujazo ukawa umepitwa na maji,ilikuwa ukiinama kidogo unayashika maji na mkono.Kiukweli mimi ni jasiri lakini hofu kuu ilitanda ndani ya moyo wangu,nilikuwa nikimuangalia Kamugisha yeye hakuwa na hofu yeyote kana kwamba alikuwa akiifurahia ile safari.

Jamaa wa Boti "Jamani nadhani muanze kunipatia nauli"

Kila mmoja alimpatia nauli ambayo ilikuwa shilingi elfu 30 kwa mtu mmoja.Baada ya kukamilisha mambo yao Boti iling'oa nanga mida ya saa 12 jioni kuelekea upande wa Congo.

Kadiri tulivyokuwa tukiyakata maji ndivyo hali ya hewa nayo ilianza kubadirika na kusababisha mawimbi makubwa yaliyokuwa yakiyumbisha ile boti kwa kiasi kikubwa;Upande wangu kiukweli nilikuwa napata taabu sana kwa hofu hadi upumuaji ukawa ni changamoto,sikuwahi kushuhudia hali kama ile tangu nimezaliwa.

Muendeshaji wa ile Boti alipoona hali imeanza kuwa mbaya aliipelekea kando ya kile kisiwa cha Mandakerege kwa upande wa nyuma kwasababu tulikuwa tushaviacha vijiji kadhaa nyuma,alipofika hapo alianza kuwasiliana na watu wa upande wa Congo kuwauliza kama kwa upande ule hali ya hewa inaweza kuwa nzuri tuondoke mdogo mdogo,sasa nadhani wale jamaa wa Moba walimwambia aende mdogo mdogo hali ya hewa si nzuri kwasababu kulikuwa kuna kitu wanakiita wao "KUSI".

Sasa hiyo KUSI ilikuwa ni aina ya upepo mbaya sana ambao ulikuwa unapiga kutokea Kusini kuelekea Kaskazini na Mashariki,Upepo huu ni mbaya zaidi kwa mujibu wao na wajuvi walikuwa wanasema ni heri ukutwe na Upepo utokao KASKAZ kuliko kukutwa na hiyo kitu iitwayo KUSI,ilikuwa ni hatari sana.

Basi baada ya jamaa muendesha chombo kujiridhisha aliamua kuondoa chombo mdogo mdogo,kadiri tulivyokuwa tunaviacha visiwa vya Tanzania giza totoro na upepo mkali vilikuwa vikitusumbua kwa sana tu.

Tuliyakata maji kwa shida sana usiku huo kwa kuwa kulikuwa na mawimbi makali mno,ilipofika mida ya saa 6 usiku tukafika sehemu ambayo wao wanaiita GEZI,hiyo GEZI ni katikati ya TANZANIA na CONGO na ndipo kwenye mkondo mkali mno wa maji,huwa mkivuka salama eneo hilo mnapaswa kumshukuru Mungu kwa kuwavusha salama na kama wewe ni muabudu mizimu basi inapaswa uishukuru Mizimu ya kwenu.

Haikuchukua muda hali ikabadirika sana na kupitia mawimbi yale makali yaliyokuwa yakiipiga ile boti,nahodha wa chombo aliamua kuzima injini kwasababu hali ilikuwa mbaya,sasa kumbe kuzima injini jamaa ni kama alifanya makosa makubwa mno,Kuna Wimbi lilikuja likatuchota likatuzungusha ile boti ikaangalia ilipotokea,kiukweli kila mtu alikuwa anamuomba Mungu kwa namna alivyokuwa anajua yeye,jamaa muendesha chombo alipoona boti imegeuzwa na mawimbi alikiwasha chombo tukawa tunarudi tena Tanzania,sasa kumbe yale mawimbi yalitikisa ubao ukawa unapitisha maji kwa chini kwa kasi ya ajabu.Wale wasaidizi wake wakaanza kupiga kelele kwa nguvu sana.

Wasaidizi "Mwambieni Ustaadhi maji yanaingia ndaniiiiii !"

Waliendelea "Mwambie ustadhi maji yanaingia ndaniiiiiiii !"

Kwakuwa wao walikuwa mbele kabisa walitaka tupaze sauti kumwambia muendesha chombo aliyekuwa akiitwa Ustadhi,ya kwamba ajaribu kuwa makini kwasababu maji yanaingia ndani.Watu waliokuwa nyuma kwenye injini walijaribu kumwambia jamaa na yeye akawaambia wawashe majenereta ya kuvuta maji na kuyatoa nje.

Wasaidizi " Maji ni mengi mno na mashine zinazidiwa"

Baada ya kuona hali inakuwa mbaya,kuna jamaa ambao walikuwa na mizigo yao kwenye ile boti walianza kuvua nguo wakabaki na kaptura pekee kisha wakaanza kupiga kelele ya kwamba wanaume wote tuingie chini tukasaidie kutoa maji kwa nguvu zote kupitia ndoo zilizokuwa huko kwasababu ile mashine iliilemewa.


Inaendelea......................
 
Daaah, poleni sana mkuu, utafutaji ndivyo ulivyo.
 
Tupe burudani mkuu, tupo tumeketi hapa na mfungo huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…