Namna Watanzania wanavyotapeliwa na Waganga wa Kienyeji nchini Kongo

SEHEMU YA TANO

Hali ilizidi kuwa mbaya sana kwasababu maji yaliendelea kujaa kwa wingi,Baada ya yule Ustadhi aliyekuwa akiendesha kile chombo kuona mambo yanazidi kwenda mlama,alijaribu kuwasiliana na watu wa nchi kavu kule bandari ya Kirando kuona kama tutapata msaada,Mungu alisaidia mpaka wakati huo mawasiliano kwa hiyo sehemu ya katikati ya ziwa yenye mkondo mkali mawasiliano yalikuwa yakipatikana.

Alimpigia yule Seif usiku huo na bahati nzuri akapatikana,sasa ishu ikawa ni kutufikia kwasababu tulikuwa mbali mno,sasa kumbe Seif alimwambia Ustadhi tuanze kutupa mizigo ziwani.

Utaratibu huwa ni kwamba,mnapopata matatizo ya msukosuko mkiwa ziwani huwa hakuna namna,mnaambiwa muanze kutupa mizigo kwenye maji,hapa huwa kuna imani za aina mbili.

1.Huamini mkitupa mizigo ziwani basi hali ya hewa itakuwa shwari.

2.Ni kupunguza uzito kwenye boti angalau kuweka uwiano sawa ili mpone.

Ustadhi "Anzeni kutupa mizigooooooo!"

Aliendelea "Tupeni mizigoooooo hiyoooo!"

Kila mtu aliyekuwa kwenye ile boti alianza kushika mzigo anaohumudu na kuurusha kwenye maji,mimi wakati huo kwakweli sikujua nifanyeje kwasababu hali yangu ilikuwa mbaya sana na nilidhani uenda siku hiyo ndiyo ilikuwa mwisho wa maisha yangu hapa duniani.Nilikuwa nawaza itakuwaje kwasababu niliondoka bila mtu yeyote kufahamu naenda wapi.

Pamoja na kutupa mizigo kwenye maji,bado hali ikazidi kuwa mbaya sana,Yule ustadhi niliona amechua boya akavaa akachukua na kamba akakamata dumu akaifunga kwenye dumu akawa tayari kwa lolote.

Wasaidizi wake nao nikaona kila mmoja amejiandaa kisaikolojia;Sisi ambao tulikuwa abiria kila mtu alikuwa akilia na kusali kivyake,wakati wenzangu kila mtu alikumbatia dumu lake,mimi kuna dumu lilikuwa na mafuta ambalo lilikuwa kando yangu,nikalichukua nikamwaga yale mafuta ziwani kisha nikafunga mfuniko nikaliweka chini ya miguu yangu.

Ustadhi na wasaidizi wake kumbe wao wote walikuwa wamejifunga kamba kiunoni kisha wakazifunga kwenye yale madumu, baadae nilipokuja kuuliza nikaambiwa madumu huwa yanakawaida ya kuponyoka mkononi ukiwa kwenye maji,hivyo ukifunga kamba itakusaidia katika purukushani za mawimbi ya maji lisikimbie kwenda mbali ukafa maji.

Nakumbuka ilibidi nimuombe Mungu anisamehe dhambi zangu kwakuwa nilikuwa nimekosea sana.

Mimi "Eeeh Mungu wangu nimekutenda dhambi kwa kujua au kutokujua,naomba unisamehe,ikikupendeza leo ndiyo ikawa mwisho wa maisha yangu naomba unikumbuke katika ufalme wako utakaokuja"

Hayo ndiyo maombi nilimuomba Mungu wangu kwa wakati huo,kiukweli nilikuwa nimeshakata tamaa na nilijua sitoiona tena nchi kavu.

Sasa kumbe Seif aliwapigia simu kikosi cha uokoaji cha JWTZ ambao wapo jirani na Kirando kwenye mji wa Kipili,baada ya kikosi kazi cha Uokoaji cha JWTZ kupewa taarifa ile waliwasha Boti zao aina ya Fiber ambazo zinakimbia hatari,sasa kwakuwa Seif aliwaambia tupo Gezini jamaa waliondoka hadi Kirando kumchukua Seif waje nae maeneo ambayo tulikuwepo,walipofika Kirando Seif aliwapa mashine 2 za kuvuta maji kwenye boti kisha wao wakaondoka kutufuatilia tulipokuwa na Seif yeye akawasha boti yake akawa anakuja na watu wengine kwa ajili ya ukoaji.

Zile Boti za Jeshi zilifika eneo tulilokuwepo mida ya 8 usiku,walivyofika wakaanza kutuokoa kutoka kwenye ile Boti iliyokuwa inazama taratibu kwa kuzidiwa na maji,baada kuhakikisha watu wote tumeokolewa,walichukua zile mashine za kuvuta maji wakazihamishia kwenye ile boti kisha wanajeshi wengine wakabaki pale na ile fiber yao wakawa wanasaidia.Sisi tuliondolewa pale na kurudishwa hadi Kipili zilipo Kambi ya jeshi pamoja na kituo cha polisi.

Pamoja na zile Fiber kukimbia kwa spidi kali lakini tulitumia masaa 3 hadi kufika Kipili,kumbuka walifika kutuokoa ilikuwa saa 8 usiku,sasa kuondoka hapo Gezini hadi kufika Kipili ilikuwa saa 11 Afajiri.

Aisee sitokaa nisahau lile dhoruba na hata Wanajeshi walituambia Mungu alikuwa upande wetu siku hiyo kwasababu walidai huwa ni nadra kufika sehemu ya tukio wakakuta watu bado wapo hai,walisema ajali nyingi za hapo Gezini huwa wanafika kuokoa wanakuta watu walishakufa kitambo.

Bado hadi leo namshukuru Mungu sana kwasababu naamini bado anamakusudi na mimi,sema mimi ndiye muda mwingine najizima data na kuendelea kufanya maovu.

Baada ya kufika Bandarini nakumbuka simu zilipigwa sana siku hiyo kutoka kwa wakubwa,baada ya kuhesabiwa idadi yetu tulikabidhiwa kwa jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano wakitaka kufahamu ni kitu gani kilitokea.

Kamanda wa Jeshi "Poleni sana ndugu zetu,Mungu amewasaidia na mmenusurika,msiwe na hofu hapa ni sehemu salama na mtahudumiwa hadi pale mtakapopata usafiri mwingine au hadi dhoruba zitakapotulia"

Aliendelea "Sisi kama Jeshi lenu tumeshakamilisha kazi yetu,tunawakabidhi sasa kwa Jeshi la polisi nao waendelee na utaratibu wao,ila muwe na amani kabisa hapa mtaishi kama mpo kwenu vile"

Sasa kumbe kesho yake mkuu wa Mkoa alimwambia mkuu wa wilaya aje atuone na kutupatia Pole,kiukweli Polisi na Jeshi la wananchi(JWTZ) Kwa upande wa kule wanajali sana wananchi wa Tanzania kuliko nilivyokuwa nikidhani,nadhani ni kwasababu ya mipakani na mavurugu vurugu ya waasi wa Kongo.

Mtanzania upande ule wa Sumbawanga hadi Kigoma wanathaminiwa sana majeshi yao.

Basi,baada ya kuwa kila kitu kimekamilika,tulitafutiwa boti nyingine ambayo ilikuwa ikielekea Congo siku iliyokuwa ikifuatia na tukaombewa nafasi na kiongozi wa pale bandari ya kipili,boti ile ilikuwa inaelekea Congo sehemu moja inaitwa Fungo,sasa tukifika hapo kuna mizigo ishushwe kisha ndiyo turudishwe Moba.Ile safari kiukweli kutokea Kirando hadi Moba ilituchukua siku 5 kwasababu kadhaa wa kadhaa.

Sasa tukafanikiwa kufika Moba,tulipokamilisha taratibu zote za uhamiaji upande wa Congo tukaondoka zetu kuelekea mji mmoja ambao haukuwa mbali na hapo Moba unaitwa Kirungu.Sasa hapo Moba ni Jimbo au Mkoa na makao makuu yake ndiyo hapo Kirungu.

Naendelea...................
 
Picha kadhaa za Moba
 
Attachments

  • IMG-20230405-WA0005.jpg
    IMG-20230405-WA0005.jpg
    209.2 KB · Views: 168
SEHEMU YA TANO

Hali ilizidi kuwa mbaya sana kwasababu maji yaliendelea kujaa kwa wingi,Baada ya yule Ustadhi aliyekuwa akiendesha kile chombo kuona mambo yanazidi kwenda mlama,alijaribu kuwasiliana na watu wa nchi kavu kule bandari ya Kirando kuona kama tutapata msaada,Mungu alisaidia mpaka wakati huo mawasiliano kwa hiyo sehemu ya katikati ya ziwa yenye mkondo mkali mawasiliano yalikuwa yakipatikana.

Alimpigia yule Seif usiku huo na bahati nzuri akapatikana,sasa ishu ikawa na kutufikia kwasababu tulikuwa mbali mno,sasa kumbe Seif alimwambia Ustadhi tuanze kutupa mizigo ziwani.

Utaratibu huwa ni kwamba,mnapopata matatizo ya msukosuko mkiwa ziwani huwa hakuna namna,mnaambiwa muanze kutupa mizigo kwenye maji,hapa huwa kuna imani za aina mbili.

1.Huamini mkitupa mizigo ziwani basi hali ya hewa itakuwa shwari.

2.Ni kupunguza uzito kwenye boti angalau kuweka uwiano sawa ili mpone.

Ustadhi "Anzeni kutupa mizigooooooo!"

Aliendelea "Tupeni mizigoooooo hiyoooo!"

Kila mtu aliyekuwa kwenye ile boti alianza kushika mzigo anaohumudu na kuurusha kwenye maji,mimi wakati huo kwakweli sikujua nifanyeje kwasababu hali yangu ilikuwa mbaya sana na nilidhani uenda siku hiyo ndiyo ilikuwa mwisho wa maisha yangu hapa duniani.Nilikuwa nawaza itakuwaje kwasababu niliondoka bila mtu yeyote kufahamu naenda wapi.

Pamoja na kutupa mizigo kwenye maji,bado hali ikazidi kuwa mbaya sana,Yule ustadhi niliona amechua boya akavaa akachukua na kamba akakamata dumu akaifunga kwenye dumu akawa tayari kwa lolote.

Wasaidizi wake nao nikaona kila mmoja amejiandaa kisaikolojia;Sisi ambao tulikuwa abiria kila mtu alikuwa akilia na kusali kivyake,wakati wenzangu kila mtu alikumbatia dumu lake,mimi kuna dumu lilikuwa na mafuta ambalo lilikuwa kando yangu,nikalichukua nikamwaga yale mafuta ziwani kisha nikafunga mfuniko nikaliweka chini ya miguu yangu.

Ustadhi na wasaidizi wake kumbe wao wote walikuwa wamejifunga kamba kiunoni kisha wakazifunga kwenye yale madumu, baadae nilipokuja kuuliza nikaambiwa madumu huwa yanakawaida ya kuponyoka mkononi ukiwa kwenye maji,hivyo ukifunga kama itakusaidia katika purukushani za mawimbi ya maji lisikimbie kwenda mbali ukafa maji.

Nakumbuka ilibidi nimuombe Mungu anisamehe dhambi zangu kwakuwa nilikuwa nimekosea sana.

Mimi "Eeeh Mungu nimekutenda dhambi,naomba unisamehe,Ikikupendeza nikalala mauti naomba unikumbuke katika ufalme wako utakaokuja"

Hayo ndiyo maombi nilimuomba Mungu wangu kwa wakati huo,kiukweli nilikuwa nimeshakata tamaa na nilijua sitoiona tena nchi kavu.

Sasa kumbe Seif aliwapigia simu kikosi cha uokoaji cha JWTZ ambao wapo jirani na Kirando kwenye mji wa Kipili,baada ya kikosi kazi cha Uokoaji cha JWTZ kupewa taarifa ile waliwasha Boti zao aina ya Fiber ambazo zinakimbia hatari,sasa kwakuwa Seif aliwaambia tupo Gezini jamaa waliondoka hadi Kirando kumchukua Seif waje nae maeneo ambayo tulikuwepo,walipofika Kirando Seif aliwapa mashine 2 za kuvuta maji kwenye boti kisha wao wakaondoka kutufuatilia tulipokuwa na Seif yeye akawasha boti yake akawa anakuja na watu wengine kwa ajili ya ukoaji.

Zile Boti za Jeshi zilifika eneo tulilokuwepo mida ya 8 usiku,walivyofika wakaanza kutuokoa kutoka kwenye ile Boti iliyokuwa inazama taratibu kwa kuzidiwa na maji,baada kuhakikisha watu wote tumeokolewa,walichukua zile mashine za kuvuta maji wakazihamishia kwenye ile boti kisha wanajeshi wengine wakabaki pale na ile fiber yao wakawa wanasaidia.Sisi tuliondolewa pale na kurudishwa hadi Kipili zilipo Kambi ya jeshi pamoja na kituo cha polisi.

Pamoja na zile Fiber kukimbia kwa spidi kali lakini tulitumia masaa 3 hadi kufika Kipili,kumbuka walifika kutuokoa ilikuwa saa 8 usiku,sasa kuondoka hapo Gezini hadi kufika Kipili ilikuwa saa 11 Afajiri.

Aisee sitokaa nisahau lile dhoruba na hata Wanajeshi walituambia Mungu alikuwa upande wetu siku hiyo kwasababu walidai huwa ni nadra kufika sehemu ya tukio wakakuta watu bado wapo hai,walisema ajali nyingi za hapo Gezini huwa wanafika kuokoa wanakuta watu walishakufa kitambo.

Bado hadi leo namshukuru Mungu sana kwasababu naamini bado anamakusudi na mimi,sema mimi ndiye muda mwingine najizima data na kuendelea kufanya maovu.

Baada ya kufika Bandarini nakumbuka simu zilipigwa sana siku hiyo kutoka kwa wakubwa,baada ya kuhesabiwa idadi yetu tulikabidhiwa kwa jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano wakitaka kufahamu ni kitu gani kilitokea.

Kamanda wa Jeshi "Poleni sana ndugu zetu,Mungu amewasaidia na mmenusurika,msiwe na hofu hapa ni sehemu salama na mtahudumiwa hadi pale mtakapopata usafiri mwingine au hadi dhoruba zitakapotulia"

Aliendelea "Sisi kama Jeshi lenu tumeshakamilisha kazi yetu,tunawakabidhi sasa kwa Jeshi la polisi nao waendelee na utaratibu wao,ila muwe na amani kabisa hapa mtaishi kama mpo kwenu vile"

Sasa kumbe kesho yake mkuu wa Mkoa alimwambia mkuu wa wilaya aje atuone na kutupatia Pole,kiukweli Polisi na Jeshi la wananchi(JWTZ) Kwa upande wa kule wanajali sana wananchi wa Tanzania kuliko nilivyokuwa nikidhani,nadhani ni kwasababu ya mipakani na mavurugu vurugu ya waasi wa Kongo.

Mtanzania upande ule wa Sumbawanga hadi Kigoma wanathaminiwa sana majeshi yao.

Basi,baada ya kuwa kila kitu kimekamilika,tulitafutiwa boti nyingine ambayo ilikuwa ikielekea Congo siku iliyokuwa ikifuatiwa na tukaombewa nafasi na kiongozi wa pale bandari ya kipili,boti ile ilikuwa inaelekea Congo sehemu moja inaitwa Fungo,sasa tukifika hapo kuna mizigo ishushwe kisha ndiyo turudishwe Moba.Ile safari kiukweli kutokea Kirando hadi Moba ilituchukua siku 5 kwasababu kadhaa wa kadhaa.

Sasa tukafanikiwa kufika Moba,tulipokamilisha taratibu zote za uhamiaji upande wa Congo tukaondoka zetu kuelekea mji mmoja ambao haukuwa mbali na hapo Moba unaitwa Kirungu.Sasa hapo Moba ni Jimbo au Mkoa na makao makuu yake ndiyo hapo Kirungu.

Naendelea...................
Hapo kirando 2007 , JWTZ waliwahi zuia watu kutembea mwisho saa mbili usiku kipindi ambacho vurugu za wakongo zilikuwa zimezidi hapo .

Kwahiyo sasa hivi kambi ya jeshi iliyopo hapo karibu na shule ya msingi Kirando imeondolewa mpaka Kipili ? Nijuze UMUGHAKA napamiss hapo
 
Kambi bado ipo ila pale Kipili kuna Bandari ya Jeshi la wananchi
 
Haya mambo yakuchokozwa na kutukanwa na baadhi ya members humu halafu mimi nikimjibu nakula BAN sidhani kama imekaa sawa.Haiwezekani mtu anatoka huko anakokujua yeye anaanza kuniporomoshea matusi mazito halafu nimuangalie tu!.

Bado sijafikia kiwango hicho cha Utakatifu,kama ni nginja acha iwe nginja.

Wengine hatujaumbwa kuwa watukanaji,mimi nipo kuwaburudisha na kuwaelimisha hadhira yangu na umma wa watanzania wengi wanaojitambua,sasa anatokea mtu anaanza kukuporomoshea matusi ya nguoni kisa tu alikuja Inbox akaomba jambo fulani ukamnyima,ukimjibu kidogo tu anapelekea na wewe kufungiwa,hii siyo sawa moderators,wengine mnatuonea bila sababu ya msingi.

Kama nyuzi zangu zinakupa kero na huzipendi kwanini usipite ukatazame nyuzi zinazokufurahisha?,Kila mtu hapa anasoma anachoona kwake kina manufaa na anachokipenda,kama unaona hutaki usumbufu una-Block au Una - Ignore unaendelea na mishe zako,waachieni watu wanaotaka kujifunza na kuburudika wasome nyuzi zangu.

Hadhira yangu kwa muda wa siku zisizopungua 5 imeshindwa kupata simulizi nzuri na yenye mafunzo kwasababu tu ya watu fulani wajinga ambao hawataki kuniheshimu na kuanza kuniporomoshea matusi mazito,mimi kuwajibu imekuwa nongwa,hili halikubaliki hata kidogo moderators!.

Kuna muda tunachokozwa na kupandishwa hasira na wajinga kadhaa humu JF,sasa ajabu ni kwamba,mtu anapokutukana mara ya kwanza unamripoti hakuna hatua anayochukuliwa,mara ya pili pia ni vivyo hivyo,akikutukana mara ya tatu uzalendo unakushinda unamjibu,ukisha mjibu tu hapo ndipo Moderators wanakuja kuwaadhibu,wanashindwa kumuadhibu toka awali ulipomripoti wao wanakuja kumuadhibu ulipomjibu ambapo wanawaadhibu wote wanashindwa kumuadhibu mtoa matusi au muanzilishi wa matusi,hili halikubariki na nitaendelea kulipigia kelele.

Nimewahi kutoa mapendekezo kwenye uzi wangu mmoja uko kwenye Jukwaa la COMPLAINTS, APPRECIATION AND ADVICE(TO JF) nikasema tuwekeeni Blocking Button yenye nguvu na siyo hiyo Ignore iliyopo sasa,kwasababu kama nikishaona mtu ananitukana nitampiga Block ili aende akawatukane wazazi wake huko kwasababu wao ndiyo walimfundisha ujinga huo.

Aisee nimesikitishwa sana kupigwa BAN kwakosa ambalo limesabishwa na moja ya wapumbavu hapa JF.Wengine tunakiuka taratibu kwasababu ya kuchokozwa na siyo kwamba taratibu hatuzijui!.

Mimi ni mwema na nitaendelea kuwa mwema ila nikitukanwa lazima nijibu mapigo,kama ni kufungiwa nitafungiwa sana na nipo tayari kwa hilo!.

NIMESHINDWA KUSIMULIA STORI KWA SABABU YA WAJINGA KADHAA HAPA JF,HILI HALIKUBALIKI HATA KIDOGO NA NAUMIA SANA.

Huu ni ujumbe wenu Moderators najua uzi huu mnaupitia.

Ni hayo tu.
Pole mkuu UMUGHAKA story hii inaonekana ni nzuri kuliko zote ulizowahi kuleta. HAO WANAOKUJIBU ACHANA NAO USI-COMMENT KITU WEWE WEKA UZI JUU YA UZI WAPUUZE NA SISI TUNAWAPUUZA, TUSONGE MBELE. Jitahidi sana usiwajibu wala usisome comments wewe chapa mwendo tu.
 
Back
Top Bottom