Namna Watanzania wanavyotapeliwa na Waganga wa Kienyeji nchini Kongo

Namna Watanzania wanavyotapeliwa na Waganga wa Kienyeji nchini Kongo

Haya mambo yakuchokozwa na kutukanwa na baadhi ya members humu halafu mimi nikimjibu nakula BAN sidhani kama imekaa sawa.Haiwezekani mtu anatoka huko anakokujua yeye anaanza kuniporomoshea matusi mazito halafu nimuangalie tu!.

Bado sijafikia kiwango hicho cha Utakatifu,kama ni nginja acha iwe nginja.

Wengine hatujaumbwa kuwa watukanaji,mimi nipo kuwaburudisha na kuwaelimisha hadhira yangu na umma wa watanzania wengi wanaojitambua,sasa anatokea mtu anaanza kukuporomoshea matusi ya nguoni kisa tu alikuja Inbox akaomba jambo fulani ukamnyima,ukimjibu kidogo tu anapelekea na wewe kufungiwa,hii siyo sawa moderators,wengine mnatuonea bila sababu ya msingi.

Kama nyuzi zangu zinakupa kero na huzipendi kwanini usipite ukatazame nyuzi zinazokufurahisha?,Kila mtu hapa anasoma anachoona kwake kina manufaa na anachokipenda,kama unaona hutaki usumbufu una-Block au Una - Ignore unaendelea na mishe zako,waachieni watu wanaotaka kujifunza na kuburudika wasome nyuzi zangu.

Hadhira yangu kwa muda wa siku zisizopungua 5 imeshindwa kupata simulizi nzuri na yenye mafunzo kwasababu tu ya watu fulani wajinga ambao hawataki kuniheshimu na kuanza kuniporomoshea matusi mazito,mimi kuwajibu imekuwa nongwa,hili halikubaliki hata kidogo moderators!.

Kuna muda tunachokozwa na kupandishwa hasira na wajinga kadhaa humu JF,sasa ajabu ni kwamba,mtu anapokutukana mara ya kwanza unamripoti hakuna hatua anayochukuliwa,mara ya pili pia ni vivyo hivyo,akikutukana mara ya tatu uzalendo unakushinda unamjibu,ukisha mjibu tu hapo ndipo Moderators wanakuja kuwaadhibu,wanashindwa kumuadhibu toka awali ulipomripoti wao wanakuja kumuadhibu ulipomjibu ambapo wanawaadhibu wote wanashindwa kumuadhibu mtoa matusi au muanzilishi wa matusi,hili halikubariki na nitaendelea kulipigia kelele.

Nimewahi kutoa mapendekezo kwenye uzi wangu mmoja uko kwenye Jukwaa la COMPLAINTS, APPRECIATION AND ADVICE(TO JF) nikasema tuwekeeni Blocking Button yenye nguvu na siyo hiyo Ignore iliyopo sasa,kwasababu kama nikishaona mtu ananitukana nitampiga Block ili aende akawatukane wazazi wake huko kwasababu wao ndiyo walimfundisha ujinga huo.

Aisee nimesikitishwa sana kupigwa BAN kwakosa ambalo limesabishwa na moja ya wapumbavu hapa JF.Wengine tunakiuka taratibu kwasababu ya kuchokozwa na siyo kwamba taratibu hatuzijui!.


Mimi ni mwema na nitaendelea kuwa mwema ila nikitukanwa lazima nijibu mapigo,kama ni kufungiwa nitafungiwa sana na nipo tayari kwa hilo!.

NIMESHINDWA KUSIMULIA STORI KWA SABABU YA WAJINGA KADHAA HAPA JF,HILI HALIKUBALIKI HATA KIDOGO NA NAUMIA SANA.

Huu ni ujumbe wenu Moderators najua uzi huu mnaupitia.


Ni hayo tu.
Ndio uache na wewe kuwatukana watu pale mnapo tofautiana mitazamo Zaid San kwenye siasa ,mm Ni mwana ccm ila Kuna siku ulinishbulia na matusi bila sababu yoyote kiss mitazamo ya kisiasa Ni vyema uheshimu itikadi za watu uone Kama Nani atakutukana

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
SEHEMU YA PILI

Tuliendelea kukaa pale Micasa lounge hadi mida ya saa 4 usiku ndipo jamaa ali-request tena Bolt tukarudi zetu maskani.Mimi niliendelea kama kawaida kupambana na maisha yangu haya Bodaboda huku jukumu langu kila siku likiwa ni lilelile la kumpeleka Jamaa kazini kwake na kumfuata.

Baada ya wiki moja jamaa aliniambia yeye alikuwa ameomba likizo ya muda mfupi(Takribani wiki 3)na amekubaliwa hivyo akanitaka tufanye haraka twende na tuwahi kugeuka;Sasa kwakuwa jamaa utaratibu wote wa kuelekea Congo alikuwa nao,aliniomba majina yangu ili anitengenezee cheti cha chanjo ya Korona pamoja na cheti cha chanjo ya Homa ya manjano,vyeti vyote hivi jamaa alivitengeneza yeye mimi nikapewa tu bure!.

Kamugisha "Hivi huwa unapasipoti kweli?"

Mimi "Sina kaka"

Kamugisha "Jitahidi basi upate pasipoti maana hiyo ni muhimu sana"

Kiukweli nilidhani uenda jamaa angenipatia hela nikakate hiyo pasipoti ila nilivyoona amekausha ikabidi niende mwenyewe kuitafuta katika ofisi za wilaya ya Ubungo pale Luguruni.Mimi nilikuwa sitaki kabisa kuelekea huko Congo kwasababu niliona siku zote hizo nitakazokuwa huko ina maana sitoingiza chochote.Nia na madhumuni ya kwenda Congo ilikuwa kumuunga mkono jamaa ili asije akajisikia vibaya kwasababu tayari nishamkubalia tangu siku ile tumeenda pale Micasa,malengo yangu yalikuwa si kujipatia mali kwa njia ya waganga ila kama kweli yangekuwepo nigeyapokea kwa mikono miwili,pia nilikuwa nina kumuhe muhe cha kukanyaga Congo kwa mara ya kwanza kwasababu nimekuwa nikiisikia tu.

Kweli!,nilienda nikaipambania pasipoti ya muda nikawa nimeipata,nilipoipata tu nikamjulisha mshikaji kwamba nishaipata.

Kamugisha "Ok sawa,sasa nadhani leo ngoja nikakate tiketi ya gari halafu kesho tuondoke!"

Mimi "Sawa kaka hakuna tatizo"

Jamaa alienda akakata tiketi ya gari ijulikanayo kama MAJINJAH EXPRESS,Baada ya jamaa kuniambia tutapanda gari la MAJINJA nikafahamu kabisa tutakuwa tunapitia Sumbawanga,mimi nilikuwa najua uenda tulikuwa tunapitia Kigoma kumbe ni Sumbawanga,sasa sikutaka kabisa kumwambia kwamba huko Sumbawanga nishafika hadi huko Namanyere kwenye ishu za mihangaiko,nilijikausha kana kwamba ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza.

Asubuhi na mapema jamaa alinikuta mimi nishafika stendi ya Magufuli nikiwa nishaingia nimekaa ndani ya gari.Lile gari la Majinjah sitolisahau kwasababu lilikuwa ni tofauti na lile la mara ya kwanza wakati mimi naelekea Sumbawanga,Gari lile lilikuwa kana kwamba halioshwi kwasababu lilikuwa likinuka harufu fulani za mikojo,ukiacha hewa nzito yenye kiharufu fulani lakini pia kuwaona wadudu kama Mende na Kunguni lilikuwa jambo la kawaida.

Gari liling'oa nanga mida ya saa 12 asubuhi na ilipofika mida ya saa 2 usiku tulikuwa Mkoani Mbeya,kwakuwa jamaa alikuwa amekata tiketi ya moja kwa moja kutoka Dar to Sumbawanga tulivyofika pale Mbeya abiria wa Mbeya walitelemka kisha tukaendelea na safari.Tuliingia Tunduma mida ya Saa 4 Usiku,tulipofika Tunduma ile gari taa za mbele zikawa haziwaki vizuri,kuna mahali tulifika jamaa wakawa wamepaki gari kisha wakawa wanawasiliana na wenzao ili ikiwezekana waone namna nzuri ya kutufaulisha,jamaa waliwaambia hamna gari hivyo ni eidha atafutwe fundi wa umeme aje kutengeneza au ndiyo tuondoke hivyo hivyo kibishi.

Dereva na Konda walihangaika sana siku hiyo kuhusu fundi kwasababu mafundi wengi wa huko walikuwa wakipigiwa simu wanasema wamelala na wasingeweza kutoka usiku huo mpaka kesho ndiyo wangetusaidia.Hapa ndipo nikawadharau sana ndugu zangu watanzania,yaani muda wa saa 4 usiku unapigiwa simu uje upewe pesa nzuri wewe unasema umelala,tena walikuwa wanaongea kwa nyodo na dharau sana!,kibaya zaidi waliwapigia simu mafundi wawili kwa nyakati mbili tofauti lakini hakuna aliyekuja,nakumbuka Dereva alikuwa anawaambia watafuatwa popote walipo na Bodaboda na wakimaliza watarudishwa lakini jamaa wakagoma kabisa kukiachia kitanda.

Sasa dereva alipoona hakuna namna aliamua kuwasha chombo na kuondoka hivyo hivyo taa zikiwa haziwaki,sema uzuri ni kwamba yawezekana ile njia alikuwa ameiozoea,taa zilizokuwa zinawaka zilikuwa ni zile ndogo za parking,lakini taa kubwa ziligoma kabisa kuwaka,tulitembea mdogo mdogo na namshukuru Mungu tukafanikiwa kufika Sumbawanga mida ya saa 9 Usiku.

Tulipofika Sumbawanga tulitafuta Guest nzuri iliyokuwa jirani na Stendi kisha tukachukua vyumba kila mtu akaingia kulala,hata hivyo mimi sikulala kwasababu ni kama kulikuwa kumekucha tu!,nilijilaza nikawa nikama naiota ile safari namna ilivyokuwa ndefu na misukosuko ya hapa na pale.
Kulivyopambazuka jamaa alikuja kunigongea akaniambia nijiandae ili tuwahi kuondoka,Kwakuwa mimi tayari nilikuwa nimeshaoga na kujiandaa nilimwambia nilikuwa tayari.


Basi tuliondoka zetu kuelekea stendi ili tuelekee mahali ambapo jamaa yeye alikuwa ameelekezwa au kupewa ramani na mwenyeji wake.

Kamugisha "Nauli hadi Kirando ni shi ngapi?"

Konda "Ni elfu 10 boss"

Kamugisha "Ok nikatie tiketi mbili yangu naya jamaa hapa"

Baada ya kupewa tiketi tuliingia kwenye gari aina ya Tata lililokuwa la wastani kama Eicher,kisha lilipojaza tukaondoka zetu,gari iliondoka hapo stendi ya Sumbawanga mida ya saa 1:30 na tukafika hapo Kirando mida ya 4 asubuhi.

Tulipofika pale Kirando jamaa aliniambia tuelekee eneo la bandari kulipokuwa na maboti ili tuone namna ya kupata usafiri wa kuelekea Congo ambapo alikuwa amepewa ramani na mwenyeji wake.Tulivyofika pale bandarini ilibidi tuulize utaratibu namna ulivyokuwa.

Kamugisha "Habari ya saa hizi mkuu"

Jamaa mmoja "Safi,habari ya kwako"

Kamugisha "Salama kabisa"

Aliendelea "Naomba kuuliza utaratibu wa boti hapa umekaa aje ?"

Jamaa "Boti za kwenda wapi?"

Kamugisha "Kuelekea Congo mkuu"

Jamaa "Congo ni kubwa,Congo sehemu gani?"

Kamugisha "Kuelekea Moba kaka"

Jamaa "Sasa hapa lazima muwe na vibali"

Kamugisha "Vibali tunavyo"

Jamaa "Ok sawa,sasa kuna jamaa mmoja anaitwa Seif,huyo ndiye anaye husika na mambo ya usafiri na maboti yote haya unayoyaona"

Kamugisha "Huyo Seif yuko wapi?"

Jamaa "Alikuwa hapa muda si mrefh sijui atakuwa ameenda wapi ila nyie kaeni pale mumsubiri anakuja"

Tulisogea hadi mahali fulani ambapo kulikuwa na kituo cha mafuta ambacho kilikuwa hakitumiki tukakaa ili tumsubiri bwana Seif.

Inaendelea.
Kirando,,,,na kipili nmekaa sana huko,,

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
 
SEHEMU YA NNE




Tulipanda kwenye zile bodaboda na safari ya kuelekea makaburini ili kazi ya kuanza kuaga mizimu ya mababu zetu wa kitanzania ichukue nafasi.Tulipofika jirani na lile eneo la makaburi,Jentre aliwaambia Bodaboda wasimame tushuke kisha watusubiri tukakamilishe jambo letu halafu tuondoke.

Tulipofika pale makaburini Jentre alituambia kila mtu atafute kaburi ambalo lilikuwa bado halijasakafiwa na ambalo bado lilikuwa halina siku nyingi tangu shughuli ya mazishi ifanyike.Baada ya kuwa kila mtu amepata kaburi lake,ndipo Jentre akatupa ishara ya kwamba tuvue nguo na tubaki kama tulivyozaliwa.

Jentre "Kamata hii"

Aliendelea "Naomba uniambie ndugu zako walikwisha kufa"

Mimi "Babu,Baba wakubwa kadhaa,Bibi mzaa mama,mama wadogo pamoja na wajomba ikiwemo watoto na ndugu kadhaa"

Jentre "Sasa chukua hicho kijiti nilichokupatia kisha utahesabu kutoka miguuni mwa hili kaburi hatua kumi,kisha utachukua hicho kijiti utachimba hapohapo ulipofikia kuhesabu hatua zako hizo kumi"


Aliendelea "Hakikisha shimo utakalo chimba liwe saizi ya kiganja cha mkono wako"


Baada ya kutamka maneno hayo aliondoka kwangu akaelekea kwa Kamugisha ambaye alikuwa mbali kidogo na mimi,sasa mkononi Jentre alinipatia Pemba nyeupe pamoja na kijiti kidogo chenye makadirio kama Centimeter 15.Sasa kwenye Kaburi lolote lile huwa kuna ile sehemu ambayo misalaba huwekwa na kuandikwa majina,hapo mara zote huwa tunaita kichwani na kule ambako hakuna kibao cha majina wala msalaba huwa tunaita miguuni,sasa jamaa akawa ameniambia nichukue kile kijiti cha senitimita 15 alichokuwa amenipatia nikipime kuanzia sehemu ya miguu ya lile kaburi kwa hatua ya vijiti kumi,yaani Sentimita 150 kisha hapo katikati zitakapofikia hizo hatua za vijiti ndipo nichimbe kishimo kidogo ambacho nikizamisha kiganja cha mkono wangu kiishilie chote.

Hivyo ndivyo nilivyofanya na baada ya kumaliza niliendelea kuchuchumaa pale chini nikimsubiri aje anipe maelekezo ya kufanya;Alipomalizana na Kamugisha alinirudia ndipo akaanza kuniambia nitamke maneno kadhaa atakayonielekeza yeye.

Jentre "Naomba unifuatishe maneno haya,Babu zangu,Bibi zangu,wajomba zangu,ndugu zangu wote mliofikwa na mauti,kijana wenu ninarudi kwenu naombeni baraka zenu,nimekuja kuwaaga mimi nasafiri kuelekea Congo,hivyo ninaomba baraka zenu ili nivuke salama na nikafanikishe mambo yangu"

Baada ya kuyatamka maneno hayo na mimi niliyarudia kama alivyokuwa ameniambia,nilipomaliza kuyatamka maneno hayo kuna alichukua ile pemba nyeupe aliyokuwa nayo mkononi akanipatia akaniambia niitupe kwenye kile kishimo nilichokuwa pamoja na kile kijiti kisha nifukie.

Jentre "Haya lizunguke hilo kaburi mara kumi ukirudi kinyumenyume"

Nilifanya kama alivyoniambia na baada ya kumaliza aliniambia nisimame niende nikavae nguo kisha nimsubiri akamlizane na Kamugisha kisha tuondoke zetu.Baada ya lile zoezi kuwa limekamilika kwa wote wawili,jamaa alitushika mikono kwa pamoja kisha akaanza kuongea maneno aliyokuwa akiyafahamu yeye kwa lugha ya Lingala na French.

Tulipomaliza huo mchakato tuliondoka zetu kurudi hotelini na jamaa yeye aliondoka kwenda kwake.

Asubuhi kulivyopambazuka Seif alimpigia simu Kamugisha na kumwambia inabidi tufanye harakati za kuvuka kwasababu ile Boti ambayo tulipaswa kuondoka nayo ilikuwa inaondoka baada ya kukamilisha zoezi la upakiaji wa mizigo.Tuliondoka tukaelekea zilipo ofisi za uhamiaji na kuacha documenti zetu pale tukaambiwa tutaletewa kwenye boti ambayo tulikuwa tukisafiri nayo.

Ilipofika muda wa saa nane mchana,Seif alitubeba kwenye mtumbwi wake uliokuwa umefungwa injini,kwenye mtumbwi huo tulikuwa abiria wengi.

Seif "Nawapeleka kwenye kile kisiwa pale,jamaa wanaenda kupakia mizigo mingine kwenye bandari ya Kipili,wakimaliza watawachukulia pale muondoke zenu!"

Kamugisha "Hakuna tatizo"


Kulikuwa kuna kisiwa kikubwa sana kinaitwa Mandakerege ambacho ndicho bwana Seif alituacha hapo akatuambia wale jamaa wa ile Boti wangemaliza kupakia mizigo pale bandari ya Kirando walikuwa wanaelekea bandari ya Kipili iliyokuwa kushoto mwa kirando wakapakie mzigo mwingine kisha ndiyo tusepe zetu Congo.

Kwakuwa tuliambiwa ziwani tungekaa siku zaidi ya moja kulingana na hali ya hewa,tulichukua soda za kopo pamoja na maandazi ya kutosha kama dharura endapo kungetokea jambo lolote.Kiukweli ndugu zangu kwakuwa ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika ziwa Tanganyika na kuliona,asikwambie mtu si ziwa la kawaida hata kidogo,kwa wale waliofanikiwa kuliona hata kulipita watakubaliana nami!.

Ingawa wajuvi wa mambo ya majini wanasema ziwa lile lina unafuu mkubwa kuliko ziwa Victoria lakini mimi kwakuwa maziwa yote mawili nimeshayashuhudia kwa macho,kwa upande wangu ziwa Tanganyika ni hatari kuliko ziwa Victoria,nina maana yangu kusema hivyo.

Basi bhana,tulikaa pale Mandakerege hadi mida ya saa 11 jioni,baada ya ile boti kumaliza kupakia shehena ya mzigo pale Kipili ilikuja kutuchukua pale.Kiukweli sikuwahi kuona Boti limebeba shehena ya mzigo kama lile,nilipoliona kwanza nikaingiwa na hofu nikajikuta tu nauliza wenzangu!.

Mimi "Sasa lilivyojaza mzigo hivyo tutakaa wapi?,au kwachini kuna nafasi ya abiria kukaa?"

Jamaa mmoja "Ndiyo mara kwanza nini kusafiri"

Mimi "Yes,hii ndiyo mara ya kwanza"

Jamaa "Abiria wote wanakaa juu ya huo mzigo"

Baada ya jamaa kuniambia vile nilitaka kabisa kugoma kupanda lile boti,roho yangu ilijaa sana hofu na kiukweli nilivyokuwa nikidhani ndivyo ilivyokuwa.Basi nilipiga moyo konde na nikajikaza kisabuni kijana wa Kikurya kisha baada ya kuitwa majina nikazama kwenye chombo.Ile boti ilikuwa imekula mzigo hadi ule mstari wa ujazo ukawa umepitwa na maji,ilikuwa ukiinama kidogo unayashika maji na mkono.Kiukweli mimi ni jasiri lakini hofu kuu ilitanda ndani ya moyo wangu,nilikuwa nikimuangalia Kamugisha yeye hakuwa na hofu yeyote kana kwamba alikuwa akiifurahia ile safari.

Jamaa wa Boti "Jamani nadhani muanze kunipatia nauli"

Kila mmoja alimpatia nauli ambayo ilikuwa shilingi elfu 30 kwa mtu mmoja.Baada ya kukamilisha mambo yao Boti iling'oa nanga mida ya saa 12 jioni kuelekea upande wa Congo.

Kadiri tulivyokuwa tukiyakata maji ndivyo hali ya hewa nayo ilianza kubadirika na kusababisha mawimbi makubwa yaliyokuwa yakiyumbisha ile boti kwa kiasi kikubwa;Upande wangu kiukweli nilikuwa napata taabu sana kwa hofu hadi upumuaji ukawa ni changamoto,sikuwahi kushuhudia hali kama ile tangu nimezaliwa.

Muendeshaji wa ile Boti alipoona hali imeanza kuwa mbaya aliipelekea kando ya kile kisiwa cha Mandakerege kwa upande wa nyuma kwasababu tulikuwa tushaviacha vijiji kadhaa nyuma,alipofika hapo alianza kuwasiliana na watu wa upande wa Congo kuwauliza kama kwa upande ule hali ya hewa inaweza kuwa nzuri tuondoke mdogo mdogo,sasa nadhani wale jamaa wa Moba walimwambia aende mdogo mdogo hali ya hewa si nzuri kwasababu kulikuwa kuna kitu wanakiita wao "KUSI".

Sasa hiyo KUSI ilikuwa ni aina ya upepo mbaya sana ambao ulikuwa unapiga kutokea Kusini kuelekea Kaskazini na Mashariki,Upepo huu ni mbaya zaidi kwa mujibu wao na wajuvi walikuwa wanasema ni heri ukutwe na Upepo utokao KASKAZ kuliko kukutwa na hiyo kitu iitwayo KUSI,ilikuwa ni hatari sana.

Basi baada ya jamaa muendesha chombo kujiridhisha aliamua kuondoa chombo mdogo mdogo,kadiri tulivyokuwa tunaviacha visiwa vya Tanzania giza totoro na upepo mkali vilikuwa vikitusumbua kwa sana tu.

Tuliyakata maji kwa shida sana usiku huo kwa kuwa kulikuwa na mawimbi makali mno,ilipofika mida ya saa 6 usiku tukafika sehemu ambayo wao wanaiita GEZI,hiyo GEZI ni katikati ya TANZANIA na CONGO na ndipo kwenye mkondo mkali mno wa maji,huwa mkivuka salama eneo hilo mnapaswa kumshukuru Mungu kwa kuwavusha salama na kama wewe ni muabudu mizimu basi inapaswa uishukuru Mizimu ya kwenu.

Haikuchukua muda hali ikabadirika sana na kupitia mawimbi yale makali yaliyokuwa yakiipiga boti ile,nahodha wa chombo aliamua kuzima injini kwasababu hali ilikuwa mbaya,sasa kumbe kuzima injini jamaa ni kama alifanya makosa makubwa mno,Kuna Wimbi lilikuja likatuchota likatuzungusha ile boti ikaangalia ilipotokea,kiukweli kila mtu alikuwa anamuomba Mungu kwa namna alivyokuwa anajua yeye,jamaa muendesha chombo alipoona boti imegeuzwa na mawimbi alikiwasha chombo tukawa tunarudi tena Tanzania,sasa kumbe yale mawimbi yalitikisa ubao ukawa unapitisha maji kwa chini kwa kasi ya ajabu.Wale wasaidizi wake wakaanza kupiga kelele kwa nguvu sana.

Wasaidizi "Mwambieni Ustaadhi maji yanaingia ndaniiiiii "

Waliendelea "Mwambie ustadhi maji yanaingia ndaniiiiiiii !!"

Kwakuwa wao walikuwa mbele kabisa walitaka tupaze sauti kumwambia muendesha chombo aliyekuwa akiitwa Ustadhi,ya kwamba ajaribu kuwa makini kwasababu maji yanaingia ndani.Watu waliokuwa nyuma kwenye injini walijaribu kumwambia jamaa na yeye akawaambia wawashe majenereta ya kuvuta maji na kuyatoa nje.

Wasaidizi " Maji ni mengi mno na mashine zinazidiwa"

Baada ya kuona hali inakuwa mbaya,kuna jamaa ambao walikuwa na mizigo yao kwenye ile boti walianza kuvua nguo wakabaki na kaptura pekee kisha wakaanza kupiga kelele ya kwamba wanaume wote tuingie chini tukasaidie kutoa maji kwa nguvu zote kupitia ndoo zilizokuwa huko kwasababu ile mashine iliilemewa.


Inaendelea......................
Mkuuu usinichukulie POA hiyo lake Tanganyika mm nimeenda huko kupitia kalambo upande wa samazi ,Ni Kweli unavyo Seema ziwa Lile Lina Tisha ukiona kwa macho ya kibinadamu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
SEHEMU YA TATU



Baada ya muda kupita bwana Seif alirejea akiwa ameambata na watu huku wengine wakiwa na mafurushi ya mizigo.

Kamugisha alimfuata akaanza kuzungumza nae na ndipo alimwambia asubiri kwanza kwakuwa kuna watu alikuwa anawafanyia taratibu za kusafiri;Alipomalizana na watu wake hao takribani yapata saa 8 mchana mchana,alitufuata tulipo kisha akawa anahitaji tumapatie maelekezo ni wapi tulikuwa tunaelekea .

Kamugisha " Tunaelekea Congo mkuu"

Seif "Congo sehemu gani?"

Kamugisha "Moba"

Seif "Ok usafiri wa Kuelekea Moba hadi kesho kutwa,kuna ile boti pale ndiyo mtakayoondoka nayo!"

Aliendelea "Congo mnaenda kufanyaje ndugu zangu"

Kamugisha "Kwenye mambo ya biashara tu kaka"

Seif "Kuweni wakweli,unajua watanzania sijui tukoje,mara kibao wanapita wanashindwa kusema ukweli ili kama ni msaada wapewe wao wanajifanya wajanja wakifika huko mambo yakiwagomea wanarudi na manung'uniko"

Kamugisha "Hahaha hahaha kaka bhana"

Seif "Nakwambia ukweli ndugu zangu,nyie kama mnaenda kwa waganga semeni niwaambie waganga wazuri msije mkatapeliwa!"

Jamaa alikuwa anaongea kwa ujasiri sana na pia mbele za watu,kitu ambacho mimi na mshikaji hatukukipenda hata kidogo,jamaa alimuomba kama inawezekana tutafute sehemu ambayo tutakuwa sisi watu watatu tuzungumze!.Seif alituchukua hadi maeneo ya nyumbani kwake ambako pembeni kulikuwa na Grosary ya kwake tukakaa hapo.

Sasa tukiwa pale kuna mtu alimpigia simu akamwambia amletee samaki wakubwa 3,haukupita muda boda boda mmoja alikuja na samaki wakubwa akiwa amewaning'niza mbele ya taa.

Seif "Ngojeni kwanza wawakaangie samaki hawa mle kisha ndiyo tuongee,mimi hapa kwangu huwa siwezi kuongewa na watu bila kula kwanza"


Baada ya muda wale samaki waliletwa wakiwa wamekaangwa,tulianza kuwatafuna huku tukiendelea kupiga stori za hapa na pale.Tulipomaliza kula wale samaki jamaa ndipo akaanzisha stori na alihitaji kufahamu tunaelekea Congo kufanya kitu gani!.

Kamugisha "Yes kaka unajua mficha uchi kifo umuumbua,sisi tunaelekea Congo kwa ajili ya matibabu"

Seif "Eeeh huo ndiyo uanaume,niambieni sasa mnaenda kwenye matibabu ya aina gani,Je mnaumwa ?"

Aliendelea "Msije mkaona nawauliza sana maswali,nyinyi ni watanzania wenzangu na kule mimi napafahamu vizuri sana na hata waganga wengi wazuri nawajua na ndiyo maana nataka nijue tatizo lenu kisha nitawaambia mtu sahihi atakaye wafaa!"

Seif "Hivyo msione aibu niambieni"

Kamugisha "Kaka sisi tulikuwa tunaelekea kwenye ishu za mali!"

Seif "Kwahiyo mlikuwa mnataka pesa,si ndiyo!"

Kamugisha "Ndiyo,brother!"

Seif "Sasa hayo ndiyo maneno,hapo nitajua sasa namna ya kuwasaidia!"

Aliendelea "Ngoja nimpigie bwana mmoja,aje muongee nae yaani kwa huyu niaminini tatizo lenu limepata tiba sahihi!"


Jamaa alinyanyua simu yake akapiga,ilipopokelewa wakaanza kuongea kwa lugha ya huko(Kiha au Kifipa).

Seif "Kuna jamaa nimemuita anakuja,huyu yeye ni mtaalamu wa maradhi ya kawaida na kuna kipindi mke wangu alikuwa akiumwa alinisaidia sana,huyu yeye ni mkongomani ila ameshazamia Tanzania muda mrefu na kaoa mwanamke wa Kiha,atawasaidia sana!"

Tulikaa tukiendelea kumsubiri huyo jamaa aliyeitwa aje tuzungumze ili tujue wapi pa kuanzia;Seif alikuwa ni muongeaji sana na kiukweli jamaa alibarikiwa kipaji cha kuongea.

Haukupita muda huyo jamaa alifika akiwa anavuta tumbaku,baada ya kufika bwana Seif alianza kumueleza kila kitu tulichokuwa tumezungumza nae.Baada ya kuelezwa jambo letu,jamaa alituambia wabongo wengi huwa wanafeli kwasababu ya ujuaji wa kijinga.

Jamaa "Unajua watanzania wengi huwa hawajui chochote,na hata hao mnaowaona wanasimulia huwa ni uongo tu,ukweli wa huku tunaujua sisi"

Aliendelea "Mmeaga?"

Kamugisha "Mimi sijamuaga mtu,sijui kwa upande wako mwanangu!"

Mimi "Mimi pia sijamuaga mtu"

Jamaa "Kuaga simaanishi hivyo mnavyofikiria nyie,kuaga maana yake mmeongea na mizimu ya wazee wenu?"

Baada ya kutuambia hiyo kauli tulibaki tunaangaliana na kamugisha kwasababu lilikuwa ni jambo jipya ambalo tulilisikia kwa jamaa.

Kamugisha "Sasa hao mizimu tungewaaga vipi?"

Jamaa "Hamuwezi kwenda huko bila kuaga mizimu,au mnadhani mnaweza kufanikisha mambo yenu bila kuaga mizimu?"

Aliendelea "Sasa sijui nyie mnasemaje,muage kwanza kabla ya kuondoka au muondoke bila kuaga!"

Kamugisha "Kwakuwa nia na lengo ni pesa,nadhani kuaga ni bora zaidi!"

Jamaa "Pale Moba Pol kuna jamaa yangu huyu ni mtaalamu sana kwa kazi yenu hiyo mnayoitaka,na yeye huwa hachukui pesa mpaka afanye kazi kwanza,sasa kama mko tayari tuvuke wote niwapeleke kwake kisha nikisha wafikisha mimi nitarudi nitawaacha ila mtanipa ka hela kadogo tu"

Kamugisha "Hayo sasa ndiyo mambo,tunaomba utusaidie!"

Kamugisha "Ujatuambia lakini jina lako kaka"

Jamaa "Mimi naitwa Jentre"

Kamugisha "Ok, sasa tunafanyaje?"

Jentre "Kuaga maana yake ni kuiaga mizimu ya ndugu zenu waliokufa,wawe mababu,mababa,wamama,au watoto;ili mradi wawe wamekufa hao ndiyo tunaita mizimu!"

Aliendelea "Kwakuwa hamkuaga huko mtokako,tutatafuta makaburi hapa jirani mkaage huko,kwanza nipeni hela nikachukue pemba nyeupe na udi kwa ajili ya kuagia!"


Kamugisha alichomoa noti ya shilingi elfu 5 akawa amempatia bwana Jentre ili akanunue mahitaji yaliyokuwa yanahitajika kwa ajili ya kuagia mizimu.

Jentre "Hili zoezi litafanyika usiku siyo muda huu lakini"

Seif "Ok kama ndivyo nadhani hawa mabwana waende wakatafute Guest House waweke mizigo yao kisha watarudi hapa ili ikifika jioni iwe rahisi"


Basi,bwana Seif alituchukua pale kwake akatupeleka kwenye Guest moja ambayo haikuwa mbali sana tukawa tumechukua vyumba kwa ajili ya kuweka mizigo,baada ya hapo tulirudi kwa bwana Seif kupumzika huku tukipiga stori za hapa na pale kupoteza muda.

Ilipofika jioni Seif alimuelekeza jamaa makaburi yaliyokuwa jirani na makazi ya watu,hata hivyo jamaa alimwambia pale itakuwa si pazuri kwasababu ni sehemu ambayo watu walikuwa wanapita masaa 24 na sisi tulipaswa kuvua nguo na kubaki uchi!.

Seif alimuelekeza makaburi ambayo yalikuwa mbali kidogo na mji ule mdogo na yalikuwa makaburi yaliyokuwa yanamilikiwa na kanisa la Roman Katholic,alimuita yule bodaboda aliyeleta wale samaki akamuambia aje na mwenzie ili watupeleke kwenye hayo makaburi ili kazi ya kuaga mizimu ichukue nafasi.


Inaendelea.................
Misheni kwa masister huko makaburi,,,huko kuna wachawi wa kila aina

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
 
SEHEMU YA TANO



Hali ilizidi kuwa mbaya sana kwasababu maji yaliendelea kujaa kwa wingi,Baada ya yule Ustadhi aliyekuwa akiendesha kile chombo kuona mambo yanazidi kwenda mlama,alijaribu kuwasiliana na watu wa nchi kavu kule bandari ya Kirando kuona kama tutapata msaada,Mungu alisaidia mpaka wakati huo mawasiliano kwa hiyo sehemu ya katikati ya ziwa yenye mkondo mkali mawasiliano yalikuwa yakipatikana.

Alimpigia yule Seif usiku huo na bahati nzuri akapatikana,sasa ishu ikawa na kutufikia kwasababu tulikuwa mbali mno,sasa kumbe Seif alimwambia Ustadhi tuanze kutupa mizigo ziwani.

Utaratibu huwa ni kwamba,mnapopata matatizo ya msukosuko mkiwa ziwani huwa hakuna namna,mnaambiwa muanze kutupa mizigo kwenye maji,hapa huwa kuna imani za aina mbili.

1.Huamini mkitupa mizigo ziwani basi hali ya hewa itakuwa shwari.

2.Ni kupunguza uzito kwenye boti angalau kuweka uwiano sawa ili mpone.

Ustadhi "Anzeni kutupa mizigooooooo!"

Aliendelea "Tupeni mizigoooooo hiyoooo!"

Kila mtu aliyekuwa kwenye ile boti alianza kushika mzigo anaohumudu na kuurusha kwenye maji,mimi wakati huo kwakweli sikujua nifanyeje kwasababu hali yangu ilikuwa mbaya sana na nilidhani uenda siku hiyo ndiyo ilikuwa mwisho wa maisha yangu hapa duniani.Nilikuwa nawaza itakuwaje kwasababu niliondoka bila mtu yeyote kufahamu naenda wapi.

Pamoja na kutupa mizigo kwenye maji,bado hali ikazidi kuwa mbaya sana,Yule ustadhi niliona amechua boya akavaa akachukua na kamba akakamata dumu akaifunga kwenye dumu akawa tayari kwa lolote.

Wasaidizi wake nao nikaona kila mmoja amejiandaa kisaikolojia;Sisi ambao tulikuwa abiria kila mtu alikuwa akilia na kusali kivyake,wakati wenzangu kila mtu alikumbatia dumu lake,mimi kuna dumu lilikuwa na mafuta ambalo lilikuwa kando yangu,nikalichukua nikamwaga yale mafuta ziwani kisha nikafunga mfuniko nikaliweka chini ya miguu yangu.

Ustadhi na wasaidizi wake kumbe wao wote walikuwa wamejifunga kamba kiunoni kisha wakazifunga kwenye yale madumu, baadae nilipokuja kuuliza nikaambiwa madumu huwa yanakawaida ya kuponyoka mkononi ukiwa kwenye maji,hivyo ukifunga kama itakusaidia katika purukushani za mawimbi ya maji lisikimbie kwenda mbali ukafa maji.

Nakumbuka ilibidi nimuombe Mungu anisamehe dhambi zangu kwakuwa nilikuwa nimekosea sana.

Mimi "Eeeh Mungu nimekutenda dhambi,naomba unisamehe,Ikikupendeza nikalala mauti naomba unikumbuke katika ufalme wako utakaokuja"

Hayo ndiyo maombi nilimuomba Mungu wangu kwa wakati huo,kiukweli nilikuwa nimeshakata tamaa na nilijua sitoiona tena nchi kavu.

Sasa kumbe Seif aliwapigia simu kikosi cha uokoaji cha JWTZ ambao wapo jirani na Kirando kwenye mji wa Kipili,baada ya kikosi kazi cha Uokoaji cha JWTZ kupewa taarifa ile waliwasha Boti zao aina ya Fiber ambazo zinakimbia hatari,sasa kwakuwa Seif aliwaambia tupo Gezini jamaa waliondoka hadi Kirando kumchukua Seif waje nae maeneo ambayo tulikuwepo,walipofika Kirando Seif aliwapa mashine 2 za kuvuta maji kwenye boti kisha wao wakaondoka kutufuatilia tulipokuwa na Seif yeye akawasha boti yake akawa anakuja na watu wengine kwa ajili ya ukoaji.

Zile Boti za Jeshi zilifika eneo tulilokuwepo mida ya 8 usiku,walivyofika wakaanza kutuokoa kutoka kwenye ile Boti iliyokuwa inazama taratibu kwa kuzidiwa na maji,baada kuhakikisha watu wote tumeokolewa,walichukua zile mashine za kuvuta maji wakazihamishia kwenye ile boti kisha wanajeshi wengine wakabaki pale na ile fiber yao wakawa wanasaidia.Sisi tuliondolewa pale na kurudishwa hadi Kipili zilipo Kambi ya jeshi pamoja na kituo cha polisi.

Pamoja na zile Fiber kukimbia kwa spidi kali lakini tulitumia masaa 3 hadi kufika Kipili,kumbuka walifika kutuokoa ilikuwa saa 8 usiku,sasa kuondoka hapo Gezini hadi kufika Kipili ilikuwa saa 11 Afajiri.

Aisee sitokaa nisahau lile dhoruba na hata Wanajeshi walituambia Mungu alikuwa upande wetu siku hiyo kwasababu walidai huwa ni nadra kufika sehemu ya tukio wakakuta watu bado wapo hai,walisema ajali nyingi za hapo Gezini huwa wanafika kuokoa wanakuta watu walishakufa kitambo.

Bado hadi leo namshukuru Mungu sana kwasababu naamini bado anamakusudi na mimi,sema mimi ndiye muda mwingine najizima data na kuendelea kufanya maovu.

Baada ya kufika Bandarini nakumbuka simu zilipigwa sana siku hiyo kutoka kwa wakubwa,baada ya kuhesabiwa idadi yetu tulikabidhiwa kwa jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano wakitaka kufahamu ni kitu gani kilitokea.

Kamanda wa Jeshi "Poleni sana ndugu zetu,Mungu amewasaidia na mmenusurika,msiwe na hofu hapa ni sehemu salama na mtahudumiwa hadi pale mtakapopata usafiri mwingine au hadi dhoruba zitakapotulia"

Aliendelea "Sisi kama Jeshi lenu tumeshakamilisha kazi yetu,tunawakabidhi sasa kwa Jeshi la polisi nao waendelee na utaratibu wao,ila muwe na amani kabisa hapa mtaishi kama mpo kwenu vile"

Sasa kumbe kesho yake mkuu wa Mkoa alimwambia mkuu wa wilaya aje atuone na kutupatia Pole,kiukweli Polisi na Jeshi la wananchi(JWTZ) Kwa upande wa kule wanajali sana wananchi wa Tanzania kuliko nilivyokuwa nikidhani,nadhani ni kwasababu ya mipakani na mavurugu vurugu ya waasi wa Kongo.

Mtanzania upande ule wa Sumbawanga hadi Kigoma wanathaminiwa sana majeshi yao.


Basi,baada ya kuwa kila kitu kimekamilika,tulitafutiwa boti nyingine ambayo ilikuwa ikielekea Congo siku iliyokuwa ikifuatiwa na tukaombewa nafasi na kiongozi wa pale bandari ya kipili,boti ile ilikuwa inaelekea Congo sehemu moja inaitwa Fungo,sasa tukifika hapo kuna mizigo ishushwe kisha ndiyo turudishwe Moba.Ile safari kiukweli kutokea Kirando hadi Moba ilituchukua siku 5 kwasababu kadhaa wa kadhaa.

Sasa tukafanikiwa kufika Moba,tulipokamilisha taratibu zote za uhamiaji upande wa Congo tukaondoka zetu kuelekea mji mmoja ambao haukuwa mbali na hapo Moba unaitwa Kirungu.Sasa hapo Moba ni Jimbo au Mkoa na makao makuu yake ndiyo hapo Kirungu.

Naendelea...................
Kipili hapo ndio nyumbn aise

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom