Mademoiselle
JF-Expert Member
- Jul 11, 2022
- 704
- 2,842
Nimemkumbuka dada mmoja alikuaga anaishi ubungo maeneo ya riverside. Alikuaga na biashara ya juice anaiuza kwa lita tano. Alikua anasambaza kwa wateja wa majumbani. Juice za chungwa, miwa, mixed fruits, tende, nanasi. Alikuaga anapata fedha sana. Kwa siku kukunja laki mbili kawaida. Alikuaga hadi na pikipiki mbili za delivery na kibajaji cha kusupply juice.
Sasa hiyo siku alikunja laki tatu akampa kijana anaemuamini sana aende akaweke benki. Ilikua ni kawaida mno kumpa huyo kijana. Hiyo siku kijana akatokomea. Sasa yule dada zikapita siku kadhaa hola. Akajua kijana kashachimba. Akaamua kuendelea zake na biashara. Ikapita mwezi akaja kumuona huyo kijana mitaa ya kimara. Kwenda kuongea nae kijana akamtemea shit sana mbele za watu. Yule dada ikampain akasema sawa bwana.
All this time hakuwa vizuri kwa sabbu hela ya jasho inauma. Lakin yule dada akaenda mpaka kwa ndugu za kijana akawaambia nao kama vile wakamsikiliza kijana wao. Basi akasema kwahyo mmenikataa? Akaachana nao. Akaamua kusali novena.(sijui hii sana) akasali novena sikumbuki kwa siku ngapi. Alivyomaliza tu, akaja kusikia kijana kapata ajali amelala hospitali hajiwezi..uti wa mgongo hola. Ndugu wakamfata kumuomba msamaha. Yule sister akawaambia mi nilishasamehe mbona. Mi nilikua kwenye maombi yangu mwenyewe. Yule kijana alikujaga kufariki. Nimeikumbuka tu hii story.