Namna ya kufanya ili nirejeshewe pesa ninazomdai mtu Shilingi milioni 105

Namna ya kufanya ili nirejeshewe pesa ninazomdai mtu Shilingi milioni 105

Nimemkumbuka dada mmoja alikuaga anaishi ubungo maeneo ya riverside. Alikuaga na biashara ya juice anaiuza kwa lita tano. Alikua anasambaza kwa wateja wa majumbani. Juice za chungwa, miwa, mixed fruits, tende, nanasi. Alikuaga anapata fedha sana. Kwa siku kukunja laki mbili kawaida. Alikuaga hadi na pikipiki mbili za delivery na kibajaji cha kusupply juice.

Sasa hiyo siku alikunja laki tatu akampa kijana anaemuamini sana aende akaweke benki. Ilikua ni kawaida mno kumpa huyo kijana. Hiyo siku kijana akatokomea. Sasa yule dada zikapita siku kadhaa hola. Akajua kijana kashachimba. Akaamua kuendelea zake na biashara. Ikapita mwezi akaja kumuona huyo kijana mitaa ya kimara. Kwenda kuongea nae kijana akamtemea shit sana mbele za watu. Yule dada ikampain akasema sawa bwana.

All this time hakuwa vizuri kwa sabbu hela ya jasho inauma. Lakin yule dada akaenda mpaka kwa ndugu za kijana akawaambia nao kama vile wakamsikiliza kijana wao. Basi akasema kwahyo mmenikataa? Akaachana nao. Akaamua kusali novena.(sijui hii sana) akasali novena sikumbuki kwa siku ngapi. Alivyomaliza tu, akaja kusikia kijana kapata ajali amelala hospitali hajiwezi..uti wa mgongo hola. Ndugu wakamfata kumuomba msamaha. Yule sister akawaambia mi nilishasamehe mbona. Mi nilikua kwenye maombi yangu mwenyewe. Yule kijana alikujaga kufariki. Nimeikumbuka tu hii story.
 
Wewe kwa jinsi ulivyoandika hata ukienda mahakamani utashindwa kwasababu unaonyesha huna imani na mahakama. Pia kwa mganga inaonyesha huna uzoefu. Mimi nakushauri achana na hilo jambo weka akili yako yote kwenye unachokifanya kwa sasa. Kama uliweza kufanya biashara hadi kumpa mtu mzigo wa 105m jna maana una akili nyingi za biashara na ni mjanja wa Kkoo. Kuna mdada hapo Kkoo alitapeliwa na wachina 119m cash almanusra apate uchizi ila akajipanga na kuanza upya from the scratch na sasa hivi yuko poa. Sio wewe tu umekutana na hiyo hali. Mimi pia ni mhanga wa hayo mambo ila tofauti yangu mimi na watu wengi ni kuwa watu walionidhulumu pesa walikufa.. kuna mwingine alisingizia uongo na kunibambikia kesi sasa hivi anaumwa presha vibaya mno.. mimi mwenyewe huwa sijui sababu ni nini kwasababu huwa nasamehe mapema tu.
 
Mali kauli unampa mtu hadi 100+M ? Duh hata akiwa muaminifu vipi inabidi ushtuke, hapo kama hiyo njia ya upande mwingine kama unaona inafaa sawa, ila uwe makini usije ukamalizwa pesa bure tu. But why asiwe muaminifu hata kulipa kidogo kidogo maana kama alifanya biashara it means alipata na faida juu, not ok
 
Msomee ubani mashtakha sheihk!!! 🤲🤲🤲😆
 
Watu hawaelewi kwamba walipeana mali kauli, wao wanalazimisha mahakamani wakati no document mezani, court cant make decision kwa lolote. No paper signed between both.......walipeana kishikaji ile oya mzigo huu kakomae.

unakuta labda hawa ni ndugu na vitu kama hivyo, sema haya ni maisha tu ukimuachia mungu utapata zaidi ya hizo 105 mkuu.

Siku zote tenda wema nenda zako, ushajifunza kitu wewe sali na mungu wako atakujibu na jaribu kufunga kwa sala na kuomba kwa kujinyima ndani ya siku 30 utaona miujiza.
Be always humble to GOD, SPIRIT TO GOD IS GREATER. Mungu atakujibu muda wowote, hii ni dunia na ni mapito tu yeye ajue hivyo......
 
Niliacha kuamini watu kwenye mambo ya pesa zamani sana na bora nikunyime ili kuepusha dhoruba kama hizi ambazo zinaweza kuwa hatari zaidi, nikikupa pesa ujue nimekusaidia, una deal na mwehu boss, ushauri wangu achana na huyo mtu andika loss kwenye vitabu vyako and move on, wataalam watakulia pesa zako na kukupotezea muda, rudi piga kazi utapata nyingine usiwe na wasiwasi
 
Mali kauli unampa mtu hadi 100+M ? Duh hata akiwa muaminifu vipi inabidi ushtuke, hapo kama hiyo njia ya upande mwingine kama unaona inafaa sawa, ila uwe makini usije ukamalizwa pesa bure tu. But why asiwe muaminifu hata kulipa kidogo kidogo maana kama alifanya biashara it means alipata na faida juu, not ok
Watu wanakibunda na mzunguko unakuta ni wa paaap paaap yaani anachukua mzigo wa milioni 25 trip nne tu ashafikisha mali kauli simple tu. Kwenye kulipa ndiyo anakuja kufanya umafia hewani hewani.
 
Njoo dm na majina yake matatu hatamaliza ubani wa jero majibu utayapata sitaki malipo me atanilipa Mungu ila usije na iman ya kujaribu utafanikiwa au lah.
 
Back
Top Bottom