Namna ya kufanya ili nirejeshewe pesa ninazomdai mtu Shilingi milioni 105

Namna ya kufanya ili nirejeshewe pesa ninazomdai mtu Shilingi milioni 105

Kwanza yeye mwenyewe unamuonaje anajiweza kwasasa?

Uwezo wa kunilipa anao.. ndio maana kila ninapo enda anatanguliza pesa ipi wanipotezee.. kama hapo police ndio kabisa nikienda tu wanasema wewe bwana kesi yako ya madai nendeni mahakamani wenyewe
 
Kuna mdau alikuwa ni mteja wangu, hapa Kariakoo. Nilikua nampa mali kauli ili akauze, mara ya mwisho kabisa uyo mteja alinitapeli. Hakunilipa pesa yangu. Nikafuatilia kwa njia ya sheria na kutumia police wa pale Central ya posta Tukafanikiwa kumkamata lakini kama mnavyojua police hawahusiki na madeni na jamaa alikuwa na connection, hata ndani hakulala. Kilichotokea tu ni kwamba police walishauri niende mahakamani au tuandikishane pale pale. Tukaandikishana mkataba kwamba atakua ananilipa kwa awamu. Mpaka sasa hajalipa hata sumni na amekuwa mbishi sana. Ni kama aliwapa pesa wale police maana kila Nikimkumbusha deni langu anakataa anasema yeye amesha nilipa. Nikimuuliza umenilipaje anasema alikua ananipa pesa cash kitu ambacho ni uongo.

Sasa wadau naombeni solution huyu mtu nimfanye nini? Kwanza kabisa amechangia katika kuanguka kwa biashara yangu.

Mwanzo nilifikiria kwenda mahakaman lakini najua nitapoteza pesa nyingi na wanasheria wengi ni wahuni. Pia mahakimu hawaaminiki wanaweza kula rushwa na nikapoteza haki yangu.

Wazo la pili nafikiria niende kwa mtaalam anisaidie kurejesha deni langu. Nimeshapata connection ya watalaam wanaoweza mambo hayo watu wa uhakika. Walionipa connection wao walifanikisha kurejesha pesa/mali zao.

Naombeni ushauri madhara ya kutumia mtaalam kurejesha deni na faida zake.
Kama mliandikishana nenda mahakamani achan na kuloga watu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mbona nasikia kudaiwa ni kesi na inamfunga mtu vizuri wala sio kama zamani eti "deni halimfungi mtu" check na wanasheria ukipoteza 5M ukaokoa 100 kuna shida gani
 
Huyo jamaa inaonekana ameisha jipanga ata huko kwa mtaalamu
Uwezo wa kunilipa anao.. ndio maana kila ninapo enda anatanguliza pesa ipi wanipotezee.. kama hapo police ndio kabisa nikienda tu wanasema wewe bwana kesi yako ya madai nendeni mahakamani wenyewe
 
Mbona nasikia kudaiwa ni kesi na inamfunga mtu vizuri wala sio kama zamani eti "deni halimfungi mtu" check na wanasheria ukipoteza 5M ukaokoa 100 kuna shida gani

Ndugu yangu wanasheria sikuizi ni wafanya biashara.. wanaangalia zaidi mapato yao kuliko uchungu wa kukusaidia.. pia unaweza ukawa na mwanasheria mzuri hakimu akahongwa.. hatakama una ushahidi unaweza ukapindishwa.. system yetu ipo vibaya sana na mtu akitoa pesa kidogo sheria inapindishwa mpaka nimekata tamaa..

Lakini pia ukienda kimahakama inabidi ukubali kupoteza 10 years.. kesi inaweza kwenda miaka 4-5, akakata rufaa ambayo nayo inaweza chukua miaka, 2-3 anaweza akaendelea na huo mchezo ukajikuta 10 yrs zimeisha hvi hvi..
 
Mkuu mbona unakuwa negative Sana kila unavyoshauriwa kwenda kisheria
 
Mponde tu system ya mahakama una 100 percent utarudisha hela yako.
Ila kipindi hiki, kuliko kwa mganga. Bora unamoa mtu ata elfu kumi. Anaenda anamtia hata makofi, fanya tu vibweka mzee. Ukipata nguvu nenda mahakamani. Tia makonzi mbwa huyo. Tuma watu.
 
Mteke muweke ndani, mwambie hiyo million 105 ndio mahari yake, atakula atalala, mpaka kufa kwake, ndio ushamuoa.
Amfanyie umafia tu , undava undava , mtu akikusumbua ni kumtengenezea squad ya vijana wa kazi ,kumteka then wanampeleka gereji kumpa kivinyo + kumla tigo , mnamshikilia mpaka atoe huo mtonyo na mkimuachilia mnampa onyo ,akithubutu kutoa siri video zinaleak kumuaibisha.
Wangese mahayawani kama hao ni kudeal nao kinyama tu ,hakuna huruma
 
Muachie Mungu. Move on, kuna mmoja nae alikuja kwangu kuchukua Mali kauli kwa jina la kampuni yao. Akanizima kampuni wakaniambia hio ni mzigo wake binafsi. Nilimdai muda mrefu nikaona tunasumbuana nikamwambia Mungu atanilipa. Haukupita mwezi kigari alichonunua(nahisi hela zangu zimechangia) kiligongwa kikaisha na Hana insurance. Juzi kapata ajali ya bodaboda kavunjika mguu. Malipo hapa hapa duniani.
 
Milioni 105 kwenye jua hili unapata wapi jeuri ya kumkopesha mtu, kha watu mna imani sana, hapo hata sijui naanzaje kukushauri....
 
acha kuwa na mawazo mabaya kuhusu mahakama, hao mahakimu wenye kula rushwa ni asilimia ndogo sana, wengi wanatenda haki tu usiwe na wasiwasi na usifuate tu maneno ya mtaani.

Tafuta wakili akusaidie hiyo kesi unashinda mchana kweupe kabisa.. hakikisha ile document mliyoandikishana polisi unayo na uitunze vizuri. Utampa wakili copy afungulie kesi na baada ya kesi kwisha unakamata mali zake unauza unapata pesa yako na hasara aliyokutia.

Usiogope kwenda mahakamani nenda na utapata haki yako usiwe na shaka. huko kwenye ushirikina ni kupoteza muda tu achana na mambo ya kijinga.
 
Back
Top Bottom