SoC02 Namna ya kufanya kazi na maadui sehemu ya kazi

SoC02 Namna ya kufanya kazi na maadui sehemu ya kazi

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 10, 2019
Posts
18
Reaction score
7
Umewahi kupata wazo kuwa mtu kazini kwako hana nia njema na wewe?

Je, wakati mwingine unahisi kuna watu fulani unaofanya nao kazi ni wabaya wako?

Inawezekana isiwe uadui wa moja kwa moja lakini kuna ile hali ya kutokuamni wenzako.

Unajisikia haupo salama unapomsikiliza mtu lakini hujui ni wakati upi uamni kile anachokisema.

Huwezi kuwa na Amani unapofanya kazi kwa mazingira ya namna hii.Utafanyeje?
Napendekeza utumie mbinu hizi hapa chini;-

1-Wabaini marafiki zako,mwenzi wako,watu wakomavu kazini ambao kila unapokuwa na changamoto unaweza kuwafuata na ukazungumza nao kupata mawazo.
2-Angalia namna unavyoweza kuishi maisha ya faragha yasiyoingiliana sana na watu bila sababu.
3-Tumia muda wako wa ziada kazini kufanya vitu unavyovipenda kama Mziki,Kusoma vitabu au kusikiliza Hotuba mbalimbali yaani fanya kile kinachokukuza.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom