safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Wengi hupitia nyakati ngumu endapo wakiongozwa na viongozi ama mabosi madikteta.
Zifuatazo ni mbinu unazoweza kutumia ili usidhurike au dikteta asikuone unampinga.
1. Usifanye jambo ambalo pongezi zitaenda kwako badala ya kwake, hata kama umefanya wewe jambo zuri linasibishe kwamba yeye ndio sababu japo kwa mawazo.
2. Hakikisha unajifanya kumuomba ushauri wa jambo hata kama unayo njia nzuri ya kutatua jambo hilo.
Mfano unaweza kumuambia "mkuu ishu hii nimepata wazo nifanye hivi, ila kabla ya kufanya nimeona unishauri je ni sahihi nikifanya ?"
Hapo yeye atapenda ulivyomuomba ushauri,na atakuruhusu kufanya jambo hilo ambalo wewe ndio mwenye wazo na haitakudhuru,
Epuka kufanya maamuzi bila yeye kujua so unamjulisha kwa mtindo kama huu wa kujifanya kumuomba ushauri.
3. Hakikisha hauwapondi na kuwakandia watu wengine ili usifiwe na dikteta kwa sababu dikteta haishi milele,hivyo unajiwekea ulinzi endapo akifa usiwe na maadui.
4.hakikisha ukipata nafasi ya kuwa na yeye munaongea usiwaponde na kuwachongea watu wengine kwani huwenda hao unaowachongea ni mashushushu wake wakubwa.
Ukiwa nae jikite na yeye usiwaseme wengine kabisa.
5. .hata kama akikutumbua ama kukufanyia uadui,hakikisha unazidisha heshima na ikiwezekana umtetee akisemwa vibaya hata akiwa hayupo hapo, kwa sababu kuna mashushushu watamuambia kwamba jamaa kakutetea sana.
Na hapo mtawala au bosi dikteta atakuona unafaa kwa sababu atajiona unamkubali sana licha ya kukuzingua bado unamtetea.
6. Hakikisha unanukuu kauli zake kama reference ukiwa unazungumza jambo,hiyo itamfanya ajione kwamba kauli zake zinamata na utakuwa salama kwake.
7. Hakikisha unajijengea uwezo wa kutetea kauli zake mbovu anazozitoa hata kwa kubadili kidogo maana ya maneno yake,kwa sababu madikteta wengi hawajui kujitetea ila wanatamani wawe na uwezo huo.
8.ukitoa msaada wowote ule hakikisha unajifanya kautoa yeye hata kama umetoka kwako,na hapo usimuambie kwamba kesho natoa msaada sehemu fulani kwa kujifanya umetoka kwako.
Yaani anatakiwa ashtuke tu kwamba heeh huyu jamaa msaada huu nimeutoa lini,na hatochukia kwa sababu anapenda kusifiwa daima.
9. Usije ukamsema ukiwa na watu wengine kamwe kwa sababu kiongozi ama bosi dikteta anakuwa na mashushushu kibao sana,huwenda hata hao uliokaa nao wamo.
Hakikisha hata ukiwa na mkeo haumsemi bosi wako hata kidogo,.
10. ikiwa amekupa agizo baya lenye kuumiza watu hakikisha unamfuata akiwa peke yake na kumshauri mbadala wa agizo hilo.
Usije kujifanya unataka kumshauri bosi mbele za watu,utaharibu kabisaaaa.
Tena wakati unamfuata ajue kabisa kwamba huyu mtu hawezi kwenda kutangaza kwamba yeye ndo kanishauri kubadili huu msimamo.
Ili kumuweza awaze hivyo basi unatakiwa ufuate vizuri shwria namba 4.
Unaweza kuongeza za kwako hapo chini.