Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Madictator sio poa, funika kombe !Nizamu za kinafkii...kwa watu wasio na waledi kazini
HiI sifa zote anazo Dr Mihogo pamoja na yule dalali from mawese City.wengi hupitia nyakati ngumu endapo wakiongozwa na viongozi ama mabosi madikteta.
Zifuatazo ni mbinu unazoweza kutumia ili usidhurike au dikteta asikuone unampinga.
1. Usifanye jambo ambalo pongezi zitaenda kwako badala ya kwake,hata kama umefanya wewe jambo zuri linasibishe kwamba yeye ndio sababu japo kwa mawazo.
2.hakikisha unajifanya kumuomba ushauri wa jambo hata kama unayo njia nzuri ya kutatua jambo hilo.
Mfano unaweza kumuambia "mkuu ishu hii nimepata wazo nifanye hivi,ila kabla ya kufanya nimeona unishauri je ni sahihi nikifanya ?"
Hapo yeye atapenda ulivyomuomba ushauri,na atakuruhusu kufanya jambo hilo ambalo wewe ndio mwenye wazo na haitakudhuru,
epuka kufanya maamuzi bila yeye kujua so unamjulisha kwa mtindo kama huu wa kujifanya kumuomba ushauri.
3. Hakikisha hauwapondi na kuwakandia watu wengine ili usifiwe na dikteta kwa sababu dikteta haishi milele,hivyo unajiwekea ulinzi endapo akifa usiwe na maadui.
4.hakikisha ukipata nafasi ya kuwa na yeye munaongea usiwaponde na kuwachongea watu wengine kwani huwenda hao unaowachongea ni mashushushu wake wakubwa.
Ukiwa nae jikite na yeye usiwaseme wengine kabisa.
5. .hata kama akikutumbua ama kukufanyia uadui,hakikisha unazidisha heshima na ikiwezekana umtetee akisemwa vibaya hata akiwa hayupo hapo, kwa sababu kuna mashushushu watamuambia kwamba jamaa kakutetea sana.
Na hapo mtawala au bosi dikteta atakuona unafaa kwa sababu atajiona unamkubali sana licha ya kukuzingua bado unamtetea.
6. Hakikisha unanukuu kauli zake kama reference ukiwa unazungumza jambo,hiyo itamfanya ajione kwamba kauli zake zinamata na utakuwa salama kwake.
7. Hakikisha unajijengea uwezo wa kutetea kauli zake mbovu anazozitoa hata kwa kubadili kidogo maana ya maneno yake,kwa sababu madikteta wengi hawajui kujitetea ila wanatamani wawe na uwezo huo.
8.ukitoa msaada wowote ule hakikisha unajifanya kautoa yeye hata kama umetoka kwako,na hapo usimuambie kwamba kesho natoa msaada sehemu fulani kwa kujifanya umetoka kwako.
Yaani anatakiwa ashtuke tu kwamba heeh huyu jamaa msaada huu nimeutoa lini,na hatochukia kwa sababu anapenda kusifiwa daima.
9. Usije ukamsema ukiwa na watu wengine kamwe kwa sababu kiongozi ama bosi dikteta anakuwa na mashushushu kibao sana,huwenda hata hao uliokaa nao wamo.
Hakikisha hata ukiwa na mkeo haumsemi bosi wako hata kidogo,.
10. ikiwa amekupa agizo baya lenye kuumiza watu hakikisha unamfuata akiwa peke yake na kumshauri mbadala wa agizo hilo.
Usije kujifanya unataka kumshauri bosi mbele za watu,utaharibu kabisaaaa.
Tena wakati unamfuata ajue kabisa kwamba huyu mtu hawezi kwenda kutangaza kwamba yeye ndo kanishauri kubadili huu msimamo.
Ili kumuweza awaze hivyo basi unatakiwa ufuate vizuri shwria namba 4.
Unaweza kuongeza za kwako hapo chini.
Kuna maisha baada ya umwamba.utii ukizidi huzaa uoga na uoga ukizidi huzaa unafiki (according to mwalimu nyerere)
Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
😂😂😃😂😂😂Huna watoto ww!! Muulize Nkamia
Kwaiyo unataka watanzania wote tutoke barabarani tuongee kuhusu mikutano ya siasa kwa Wana siasa wepi hawa ambao wanatuambia Lowasa fisadi kesho Wana msafisha hawa kina halima mdee kina msingwa kina Lusinde kina ziti kabwe acha bro ebu tuongee vitu seriously siasa acha wenye kazi zao watanzania kwa Sasa si wajinga kivile ndio maana wanaamua waachie CCM tu wafanye wanavyojuaNi rahisi kuongea kuliko kutenda. Juzi umemsikia Profesa Shivji, kuwa wasomi wengi wanaogopa kuikosoa serikali tofauti na miaka ya 1970/80.
Watanzania ni waoga mnoo,japo kwenye mdomo wapo vizuri na lakini kuwe na usalama. Ni watanzania wachache sana wenye uthubutu wa kumkabili dikteta.
Kwa mfano mpaka sasa tunajua katiba inaruhusu mikutano ya hadhara na maandamano ya vyama vya siasa,na siyo kwa kuomba kibali ni kutoa taarifa tu according to Jaji mkuu Mstaafu Barnabas Samata,lakini Wameambiwa wasubiri uchaguzi na kweli wanasubiri uchaguzi.
Hivyo basi mtoa uzi yuko 100%correct. Labda wewe uko Kenya. Huko sawa makamu wa Rais anapambana na Rais wake,wakikutana kwenye shughuli za kitaifa wanakuwa wamoja. Siyo Tanzania. Mama anajitahidi lakini tukubali ameathiriwa sana kwa kufanya kazi na Magu.
Na yeye anaona na pengine anaamini,njia pekee ya kujihakikishia madaraka ni kuiga baadhi ya style za Magu.
Upo sahihi kama unajiamini huwezi nyenyekea mtu hata awe mama salima utamjibu ukweli tu maisha si ndio haya haya bwana kwani wale wasio na ajira hawaishi na kama unajituma utakosaje kuishiNizamu za kinafkii...kwa watu wasio na waledi kazini
Hahha hatari mkuu.Hpo
Kwaiyo unataka watanzania wote tutoke barabarani tuongee kuhusu mikutano ya siasa kwa Wana siasa wepi hawa ambao wanatuambia Lowasa fisadi kesho Wana msafisha hawa kina halima mdee kina msingwa kina Lusinde kina ziti kabwe acha bro ebu tuongee vitu seriously siasa acha wenye kazi zao watanzania kwa Sasa si wajinga kivile ndio maana wanaamua waachie CCM tu wafanye wanavyojua
Ndio wakishinda kesi mahakamani wanapiga vigeregere mahakama imetenda haki, akishinda sabaya kesi wanalaumu mahakama inanajisiwa shubamit ndio wanataka eti tutoke tuseme Katiba mpya yani Rema yupo ughaibuni uko anataka mtoto wa mwana kibiriti ngoma atoke aandamane aseme katiba mpya wakati mda huu hayupoHahha hatari mkuu.
Hawa wanasiasa akina mbowe ambao wakishinda ubunge wanaenda bungeni,wakishinda wenzao uchaguzi ni batili hahahah
Kabisa kaka.Umeongea fact kabisa,
Hapa Cha muhimu ni kujiajiri ili uwe boss Mwnyw.
Ila Sasa changamoto hata uku kwenye kujiajili,Wanasiasa na viongozi wa serikali madikteta wapo na wanaingilia Sana harakati zetu za kila siku.
Mf: maDC,MaRC,wazee wa chama, maafisa wa TRA, MANISPAA,BANDARI,POLISI n.k
Na Lazima wote ujifunze Kuishi nao vizuri ili Mambo yako yaende
Ukikaza shingo sana,
Wanatia fitna unapotea kwenye game
Uzi mzuri Sana huu[emoji4][emoji106]
Sent using Jamii Forums mobile app