Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Kama wazazi, tunapenda kuona watoto wetu wakijifunza mambo mapya. Si ajabu kumuona mama akimuuliza mtoto maswali huku akijua mtoto atatoa jibu la kufurahisha.
Zifuatazo ni baadhi ya mbinu ambazo zinaweza kukusaidia kukuza mtoto anayependa kusoma.
Panga kusoma na mtoto wako iwe ratiba ya kila siku. Endapo mtasoma pamoja, mtoto wako ataona kuwa kusoma kuna umuhimu na ataungojea muda huu kwa hamu hata kama umepanga kusoma kwa nusu saa tu.
Mnapotaka kusoma, shirikiana na mtoto wako kuchagua vitabu. Maamuzi kama haya ni muhimu kwa mtoto wako na yatamuongezea shauku ya kusoma na kujifunza.
Msomee mtoto kwa sauti huku ukimwonesha unapopasoma. Unaweza pia ukapokezana kusoma na mwanao. Hii itamsaidia kujifunza maneno mapya kirahisi na kuyakumbuka.
Muoneshe mtoto picha mkiwa mnasoma. Hii itamsaidia kuelewa maneno mapya na magumu. Mnaweza kuangalia picha kabla ya kusoma hadithi na kukisia inahusu nini. Hii huleta tofauti katika simulizi na huweza kuchochea ubunifu wa mtoto.
Filamu na simulizi za redioni ni namna nyingine za kuleta tofauti katika kusimulia hadithi. Watoto hutofautiana na sio kila mtoto anapenda kusoma sana kwa hiyo kuangalia/kusikiliza simulizi wanazopenda huenda kukawapa hamasa ya kusoma hadithi hizo.
#Malezi