Namna ya kuonana na Rais

Namna ya kuonana na Rais

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
17,171
Reaction score
34,394
Habari wanabodi,

Naomba kufahamishwa au kujuzwa je, nikitaka kuonana na mama Samia yani face to face nifanyeje? Wazo hili limenijia kwa mfano unataka kuongea naye je, unamngoja akiwa kwenye msafara unamuomba? Unamngoja afike ikulu ndogo mkoa anaotembelea unamfata?

Akiwa safarini unampigia makelele "mama nina shida ya kuonana na wewe" je, inaruhusiwa kwa mwananchi wa kawaida kumuona raisi wa nchi akaongea naye ana kwa ana? Je, hua anajibu dm huko tweeter au instagram?

Yaani ikitokea unataka kuonana na raisi ukiwa mwananchi wa kawaida unatakiwa kufata hatua zipi?
 
habari wanabodi,

naomba kufahamishwa au kujuzwa je nikitaka kuonana na mama samia yani face to face nifanyeje?? wazo hili limenijia kwa mfano unataka kuongea naye je unamngoja akiwa kwenye msafara unamuomba?? unamngoja afike ikulu ndogo mkoa anaotembelea unamfata?? akiwa safarini unampigia makelele "mama nina shida ya kuonana na wewe" je inaruhusiwa kwa mwananchi wa kawaida kumuona raisi wa nchi akaongea naye ana kwa ana?? je hua anajibu dm huko tweeter au instagram??

yaani ikitokea unataka kuonana na raisi ukiwamwananchi wa kawaida unatakiwa kufata hatua zipi??
Mkuu; kwanza ukumbuke na kuzingatia kwamba Rais ni mtu/binadamu kama ww na mm. Pili zingatia kwamba kwa nafasi yake kama Rais, anawajibika au anahudumia waTz zaidi ya milioni 60. Kwa mantiki hiyo ukiwa unataka kuonana naye uso kwa uso lazima uwe umejiandaa vema na kuzingatia Taratibu zilizopo i.e. Utapewa Appointment inayoonesha mahali na muda. Lakini cha muhimu zaidi ujiulize Je, Wasaidizi wake wameshindwa kukusikiliza? Yani Mtendaji Kata, DED, DC, Mkuu wa Mkoa, Katibu Mkuu na Waziri wanaohusika na Hoja yako wameshindwa kukusikiliza?(Kumbuka hao ndo wanamwakilisha Rais katika nafasi zao). Je, naye Mbunge wako ameshindwa? Ila kama unataka eti kuonana naye tu ili umsalimie, umpe na kaumbeya kidogo au upige naye picha ....dah! Hilo ni gumu kidogo japokuwa inawezekana.
Kama una kero nyeti au kitu so touching kwamba ni yeye tu "in person" inafaa akisikie kwa masikio yake, nenda kwa Mkuu wa Mkoa wako atakupa mwongozo au Ikulu Nyumbani kwake. Ila ONYO usiende na jambo ambalo limeruka ngazi/hatua za ufumbuzi kama nilivyobainisha hapo juu.
 
swali hili hili nimewah kumuuliza diwani wangu namna ya kuonana na mbunge hahahha aliniambia nipp kwenye kikao nitakutafta, uzuri n mtu ambae tunafahamiana nikaja kumtafta tena nikamkunbushia swali langu alichofanya ni kunijibu the same thing yupo kwenye kikao sasa ninajiuliza huyo ni mbunge tu napigwa dana dana na ni haki yangu kama mwananchi kujua ili kama hatua nizifuate ikitokea nna shida hio sasa diwani kanigomea rc ni nani anisaidie yan naona kabisa kufuata utaratibu kwa kutaka kuonana na raisi ni mtihani hence huku chini hawana huo ushirikiano na ndio hali halisi
 
Hayo ndo wanasemaga majibu ya mkato na mara nyingi hutolewa na mtu asiyejua jawabu sahihi. Madiwani (sio wote) wapo kisiasa zaidi na wanachojua ni kumhoji DED, Kupitisha Maazimio au Kumwazimia Mtumishi wa Halmashauri baas;tofauti na hapo atakubabaisha sana. Mbunge anayo fursa ya kumwona Rais moja kwa moja lakini naye atazingatia utaratibu uliopo.
Kumbuka RC ni mteule wa Rais. Ana Mamlaka makubwa sana kufanya maamuzi akishauriwa na mtaalam wake -Katibu Tawala Mkoa, zamani akiitwa RAS (Regional Administrative Secretary). Ndo mana nimekuambia hizo ngazi zote hawatashindwa kukusikiliza mpaka ufike huko juu ngazi ya mwisho kiasi hicho. Tuseme ikatokea umefika kwa Mh.Rais na hoja yako, basi ujue 100% hao wote niliowataja hapo juu na wengineo watakuwa na wakati mgumu sana.
 
Hayo ndo wanasemaga majibu ya mkato na mara nyingi hutolewa na mtu asiyejua jawabu sahihi. Madiwani (sio wote) wapo kisiasa zaidi na wanachojua ni kumhoji DED, Kupitisha Maazimio au Kumwazimia Mtumishi wa Halmashauri baas;tofauti na hapo atakubabaisha sana. Mbunge anayo fursa ya kumwona Rais moja kwa moja lakini naye atazingatia utaratibu uliopo.
Kumbuka RC ni mteule wa Rais. Ana Mamlaka makubwa sana kufanya maamuzi akishauriwa na mtaalam wake -Katibu Tawala Mkoa, zamani akiitwa RAS (Regional Administrative Secretary). Ndo mana nimekuambia hizo ngazi zote hawatashindwa kukusikiliza mpaka ufike huko juu ngazi ya mwisho kiasi hicho. Tuseme ikatokea umefika kwa Mh.Rais basi ujue 100% hao wote niliowataja hapo juu watakuwa na wakati mgumu sana.
kwanza niulize tena unaweza onana na raisi ukampa shida yako binafsi akusaidie?? ukumbuke huku chini hujapata msaada wa hio shida inawezekana??
 
Back
Top Bottom