Mkuu; kwanza ukumbuke na kuzingatia kwamba Rais ni mtu/binadamu kama ww na mm. Pili zingatia kwamba kwa nafasi yake kama Rais, anawajibika au anahudumia waTz zaidi ya milioni 60. Kwa mantiki hiyo ukiwa unataka kuonana naye uso kwa uso lazima uwe umejiandaa vema na kuzingatia Taratibu zilizopo i.e. Utapewa Appointment inayoonesha mahali na muda. Lakini cha muhimu zaidi ujiulize Je, Wasaidizi wake wameshindwa kukusikiliza? Yani Mtendaji Kata, DED, DC, Mkuu wa Mkoa, Katibu Mkuu na Waziri wanaohusika na Hoja yako wameshindwa kukusikiliza?(Kumbuka hao ndo wanamwakilisha Rais katika nafasi zao). Je, naye Mbunge wako ameshindwa? Ila kama unataka eti kuonana naye tu ili umsalimie, umpe na kaumbeya kidogo au upige naye picha ....dah! Hilo ni gumu kidogo japokuwa inawezekana.
Kama una kero nyeti au kitu so touching kwamba ni yeye tu "in person" inafaa akisikie kwa masikio yake, nenda kwa Mkuu wa Mkoa wako atakupa mwongozo au Ikulu Nyumbani kwake. Ila ONYO usiende na jambo ambalo limeruka ngazi/hatua za ufumbuzi kama nilivyobainisha hapo juu.