Asante sana
asigwa kwa mada nzuri ila mara nyingi kwenye hizo affirmation una shauriwa kufanya kinyume chake kwa mfano badala ya ku sema mimi siyo mwoga unatakiwa kusema mimi ni jasiri au tafuta neno lingine lakini usirudie kutamka mwoga, punyeto pombe nk .. Kwani subconscios mind itakuwa inaskia muoga.. Muoga.. Muoga. (kwa kuwa hilo ndilo dominant hii subconscious mind haina uwezo wa kupambanua inachukuaga mambo yote kama ni real ndiyo maana ukiwa unaota unakimbiza na mashetani yenyewe inachukulia ni kweli utakuta mapigo ya moyo yanaenda mbio,jasho linakutoka nk )
Wanashauri pia unapoacha tabia flani tafuta tabia nyingine kinyume chake ya kuireplace badala ya pombe amia kwenye maziwa, fresh fruit juice, au hata soda.
Subconscious mind siku zote ni taswira (imagnation) na conscious ina controol (will) au nia. Wanasema when imagnation is stronger than will imagnation always win. Hivyo unashauriwa ubalanceshe kati ya image yako na will visiwe vinaendana kinyume. Ndiyo maana mpigaji wapunyeto hawezi fanya bila ya kuvuta taswira picha za ngono..
Hivyo nina maanisha kama unataka kuacha uraibu wowote inatakiwa ile nia ya kuacha iendane na picha mbaya ya lile jambo unalotaka kuacha au picha nzuri ya vile ambavyo unafikiri ukiacha utakuwa.. Waswahili wanasema ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya.. Hivi mtu anayeita bangi au ugoro dawa au pombe juice kali. anaweza kuacha kweli? ni wazi hawezi kuacha. Hivyo njia nzuri niku itafutia jina baya na jina baya utalipata kwenye madhara ya hicho kitu unachotaka kuacha. Mtu mmoja akaita sigara cancer stick au kijiti cha kansa.. Hivi ni kwanini watu wanajua kabisa kwamba ni kivuta sigara nitapata kansa au nikinywa pombe namaliza pesa na chelewa kulala, au naharibu mwili lakini bado unaendelea kuvuta au kunywa pombe.. Ni kwa kuwa vitu vingi tunavyofanya ni kwasababu ya kupata starehe au kuepuka maumivu.. Hivyo mara nyingi watu waliobobea kwenye jambo flani inafikaga kipindi inakuwa anafanya jambo flani siyo kwasabu ya kupata tena starehe bali ni kwaajili ya kuepuka maumivu.. Sasa ikishafikia hatua hiyo unahitaji...Rudi kwenye wil na imagnation naishia hapa kwanza kwa sasa