SoC01 Namna ya kuondoa Usaliti ndani ya ndoa

SoC01 Namna ya kuondoa Usaliti ndani ya ndoa

Stories of Change - 2021 Competition

Jokajeusi

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2018
Posts
6,323
Reaction score
10,813
Moja ya mambo yanayovunja ndoa za siku hizi ni ongezeko la wanandoa kutokuwa waaminifu. Usaliti unaumiza, Usaliti unaua, Usaliti ni moja ya majanga yasiyosemwa ndani ya jamii yetu yaliyomo kwenye ndoa.

Ndoa ni muunganiko wa mwanaume na mwanamke, walioamua Kwa hiyari yao wakiwa na akili timamu kuishi pamoja Kama mume na Mke. Katika nchi yetu, zipo ndoa za Aina nyingi kulingana na zinapofungiwa Kama vile ndoa za Kidini, kimila na ndoa ya kiserikali ambapo hujulikana pia Kama ndoa ya bomani.
Pia kuna Aina za ndoa kulingana na idadi ya Mke/Wake wanaoolewa Kama vile; ndoa ya mume na Mke mmoja, na ndoa ya Mume na wake wengi.

Ndoa husaidia mambo kadhaa Kama ifuatavyo;
i) Kuunganisha undugu; ndoa huweza kukutanisha familia, koo, Makabila au mataifa yasiyo na mahusiano ya kiundugu na kuyafanya kuwa ndugu.
Sio ajabu Rais wa Kwanza, Hayatti Nyerere aliondoa ukabila Kupitia kuchanganya jamii ili ziweze kuingiliana na kuoana na kuoleana.

ii) Ndoa Imara husaidia jamii kuwa na maadili
iii) Ndoa hutupatia watoto watakaokuzwa vizuri.
iv) Ndoa ni sehemu ya ustaarabu Kwa watu, na kuepusha uasherati, uzinzi na athari ya mambo hayo.
v) Ndoa husaidia watu(wanandoa) kusaidiana kwenye maisha.
vi) Ndoa humpatia mtu hadhi na heshima ndani ya jamii.
vii) Ndoa ndio taasisi pekee inayompatia mtu mwenza wa maisha na kibali cha kummiliki mtu mwingine. Mwanamke atakuwa na kibali na haki ya kummiliki mwanaume Kwa kumuita mume wake, halikadhalika na mwanaume.

Ndoa licha ya kuwa na faida lukuki lakini huweza kugeuka shubiri endapo mmoja hatakuwa mwaminifu. Upo msemo usemao ndoa ndoano, ingawaje sipendi kuupa nguvu msemo huo lakini siwezi kujifanya sioni kwa yale yaendeleayo kwenye jamii hasa za mijini.

Usaliti ni kuvunja maagano, makubaliano baina ya watu wawili. Hiyo huweza kusababishwa na kutokuwa mwaminifu au tamaa mbaya iliyopitiliza.
Hata katika ndoa Usaliti upo. Mwanandoa mmoja au wote wanaweza wakajikuta wakiwa katika tamaa mbaya au kutokuwa waaminifu na hivyo kuvunja makabuliano na maagano waliyoweka na wenzi wao.

Usaliti unaua, Usaliti unaweza kuleta majeraha. Matukio kadhaa ya mauaji ndani ya jamii zetu yanaripotiwa kila uchwao. Sio tuu kwenye nchi yetu hata nchi Jirani na Nchi za mbali. Usaliti ndani ya ndoa umeua na kujeruhi wengi, na wenye nyoyo za kufuata sheria wamejikuta wakibaki na maumivu makali yasiyosahaulika mioyoni mwao.

Sababu kuu za Usaliti ndani ya ndoa huweza kuwa kati ya zifuatazo;

i) Watu kushindwa kujizuia na tamaa mbaya hasa tamaa ya ngono.
ii) Utandawazi unaotokana na ukuaji WA Sayansi na Teknolojia ambapo umefanya dunia kuwa Kama kijiji, na mchanganyiko wa kiutamaduni kuongezeka. Hali iliyopelekea baadhi ya tamaduni mbaya kutoka nchi zilizoendelea kuathiri jamii zetu mpaka kwenye ndoa.
iii). Hali ngumu ya maisha ambapo watu hutumia miili yao Kama chanzo cha mapato, wanawake wanadanga, wanaume wanalelewa na kujigeuza mario.

iv). Propaganda na drama zinazoendeshwa na watu mashuhuri na vyombo vya habari kuhusiana na masuala ya Mahusiano ya kimapenzi na ndoa pia vimechangia Usaliti kuzidi kuongeka.

v) Kutokuwa na usimamizi mzuri wa sheria kwenye serikali, mila na dini zinazodhibiti Usaliti ndani ya ndoa pia husababisha Usaliti kuwapo, kwani inaonekana sio jinai wala kosa bali ni utashi WA mtu mwenyewe.
Miongoni mwa sababu zingine.

Usaliti ndani ya ndoa umepeleka watu jela, umepeleka watu makaburini.
Usaliti umesababisha Ongezeko kubwa la watoto wa mitaani kwani familia nyingi zimevunjika kutokana na Usaliti.

Usaliti ndani ya ndoa pia umesababisha watu kupata magonjwa ya zinaa. Wengi wamejikuta wamedumbukia kwenye shimo lenye magonjwa mabaya na yakutisha ya zinaa Kama vile UKIMWI na kuiua familia.
Usaliti! Usaliti! Usaliti!

Usaliti ndani ya ndoa umesababisha chuki baina ya watu kuongezeka. Umesababisha jamii Fulani kushutumiwa na kupewa majina yenye sifa mbaya ya Umalaya. Mtu mmoja anaweza akasalitiwa na Mke/mume wake alafu akalijumuisha kabila zima la mwenzi wake aliyemsaliti kuwa wanatabia za kimalaya Jambo ambalo sio kweli.

Usaliti ndani ya ndoa umeathiri baadhi ya watu kiuchumi, Wanawake Kwa wanaume wapo waliofukuzwa kazi kisa utendaji mbovu ambao mizizi yake ikifuatiliwa utakuta ni Usaliti ndani ya ndoa.

Usaliti ndani ya ndoa, umechangia Kwa kiasi kikubwa watoto kuzaliwa wasio ndani ya ndani. Wapo wanawake walioolewa wanaozaa watoto na wanaume wengine mbali na waume zao waliowaoa. Halikadhalika na wanaume kuzaa nje ya ndoa wangali ndani ya ndoa.

Usaliti unaathari nyingi, hata nilisema nieleze athari zote hapa, naweza kujikuta naandika kitabu kizima kinachoelezea athari pekee yake.

Usaliti lazima udhibitwe, lazima ukabiliwe. Lakini swali linakuja, tuyaukabili vipi Usaliti ndani ya ndoa? Sababu za kuudhibiti tunazo, athari zake kila mmoja anazijua. Sasa embu tuone Kwa kifupi namna ya kuondoa Usaliti ndani ya ndoa Kama sio kuupunguza kabisa;

1. Serikali ikaze sheria Kwa wasaliti ndani ya ndoa na adhabu Kali itolewe.
Ingawaje suala la ndoa linaonekana ni suala binafsi na kila mtu ana Uhuru wa kufanya vile atakavyo lakini katika hili kutokana linaathiri jamii Kwa sehemu kubwa, serikali inanafasi kubwa ya kudhibiti na kupunguza Kama sio kuondoa kabisa Usaliti ndani ya ndoa, Kwa kuweka sheria Kali Kwa watakaosaliti ndoa zao.
Hii itawafanya watu hasa wanaoshindwa kujizuia kuwa na hofu ya kusaliti ndoa zao.
Serikali iweke adhabu Kwa wasaliti ndani ya ndoa Kama inataka matokeo hasi ya Usaliti yapungue.

2. Viongozi wa Kidini na kimila wazipe nguvu sheria na adhabu Kwa Wasaliti wa ndoa;
Bahati nzuri sheria za kimila na Kidini zipo kabisa wala sio kwamba zinatungwa upya, sheria na adhabu katika dini na Mila zetu zipo zinazohusu wasaliti ndani ya ndoa. Tatizo kubwa hazifuatwi.
Viongozi wa Kidini na kimila pamoja na serikali zikishirikiana Kwa pamoja kuondoa Usaliti ndani ya ndoa, na uasherati wa reja reja ninauhakika Usaliti utapungua Kama sio kuondoka kabisa.

3. Taasisi, mashirika, na makampuni pamoja na serikali ziweke sheria kwa Wafanyakazi wao kuwa atakayesaliti ndoa, atafukuzwa kazi pasipo jicho la huruma.
Mbali na sheria zingine, iwepo sheria Kwa kila Kampuni, shirika, taasisi na serikali Kwa Wafanyakazi kuwa Moja ya adhabu ya wasaliti ndani ya ndoa ni kufukuzwa kazi.
Unajua kazi ni baraka, lakini wakati mwingine ni laana hasa pale mtu anapojipatia riziki inayomfanya afanye Uovu ndani ya jamii.

Imezoeleka kuwa, wanaume wengi wasipokuwa na kazi zinazowaingizia kipato wanakuwa sio Wasaliti Kwa wenzi wao, lakini wakishapata kazi zenye kuwa kipato huanza kuzisaliti familia zao.
Namna bora ya kudhibiti Jambo hili ni kuweka sheria na adhabu ya kuwafukuza kazi wasaliti ndani ya ndoa.

4. Elimu ya maadili kuhusu mahusiano itolewe.
Elimu ya Mahusiano itolewe kuanzia kwenye familia, dini, na shuleni na vyuoni.
4.1. Elimu kutoka Kwa wazazi.
Wazazi wawafundishe watoto maadili ya kimahusiano, wawafundishe miiko ndani ya Mahusiano, wawafundishe watoto namna ya kufanya chaguzi Bora hasa kwenye kuchagua wenza wa maisha, wawafundishe uvumilivu na ustahimilivu kwenye mahusiano na maisha Kwa ujumla. Wazazi Kwa sehemu kubwa hujenga msingi mzuri Kwa watoto wao kuhusu ndoa.
Pia wazazi wawafundishe watoto wao kujitunza kimwili, waolewe wakiwa bikra na Vijana waoe wakiwa hawajamjua mwanamke.

4.2. Elimu kutoka kwenye Dini.
Elimu ya Dini inayomchango mkubwa kwenye ndoa ndani ya jamii yetu. Viongozi wa dini waliothibitishwa na serikali, waliosomea na kupewa Leseni na kibali cha kuhudumu kwenye taasisi za Kidini hao ndio watoe elimu ya Mahusiano ya kindoa na familia.
Dini itoe umuhimu wa wenza kuwa waaminifu na wenye kujizuia kiimani na Kiroho.

4.3. Serikali iingize Mada ya Mahusiano ya ndoa katika mitaala ya shule na itoe msisitizo.
Nafahamu kuna topic ya Uchumba na ndoa kwenye Somo la uraia kwenye elimu ya sekondari.
Serikali inapaswa itilia mkazo mada hiyo, tena mada hiyo iwekwe katika kila darasa la mwisho la elimu, mfano, sekondari; mada hiyo iwekwe kidato cha nne na cha sita.
Kwa chuoni iwekwe Kwa wanafunzi WA mwaka wa mwisho, iwe watatu, wanne au watano kulingana na kozi Mwanafunzi anayoichukua.

Elimu ya Mahusiano na ndoa itolewe kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Matamasha, semina na washaa zinazokemea Usaliti, kuelimisha jamii zitolewe.

5. Watu mashuhuri wanaohamasisha Usaliti, wadhibitiwe.
Serikali na vyombo vyenye mamlaka ikiwepo dini, wamiliki wa vyombo vya habari na wazazi wanayonafasi ya kulifanya hili likafanikiwa Kwa kiasi kikubwa.
Watu mashuhuri Kama Wasanii wa muziki, waigizaji, walimbwende, wanamasumbwi, Wachezaji mpira, Watangazaji na watu wote mashuhuri wenye maudhui ya kuhamasisha Usaliti ndani ya ndoa, kuathiri maadili ya kimahusiano, wadhibitiwe.

Vyombo vya habari zisiwape promo, zisitoe habari zao, serikali iwafutie vibali vya kufanya kazi za Sanaa au kazi hizo zinazowapa umashuhuri.
Tunaojua kuwa Wasanii ni kioo cha jamii, kizazi kichanga huiga mambo mengi kutoka Kwa watu mashuhuri.
Serikali, vyombo vya dini na wazazi iwapige Pini, pasipo huruma.

Ingawaje watetezi wa haki za binadamu watatetea Uhuru wao lakini ni bora kudhibiti Uhuru unaoathiri jamii yetu.

6. Vijana na wasichana wachape kazi kujiingizia kipato.
Kazi ni moja ya nguzo muhimu katika ndoa Imara. Kazi ndio inayofanya familia iwe na furaha kupitia kipato kinachopatikana.

Dhana potofu ya mwanamke hapaswi kufanya kazi iondolewe kwenye jamii. Kwani tangu zamani jamii zetu wanawake walikuwa wakifanya kazi za uzalishaji.
Utegemezi pia ni chanzo kikubwa cha Usaliti pale inapotokea mwanaume anashindwa kumudu kuhudumia familia yake.

Mke huweza Kumsaliti mume wake Kwa sababu ya kukutafutia riziki kupitia mwili wake yaani kufanya ukahaba.
Hivyo ni afadhali Mke naye akawa na kazi au shughuli ya kumuingizia kipato.

Vijana pia wanapaswa kuchapa kazi pasipo kuchagua ili waweze kujimudu na kuendesha familia zao.
Wanandoa wakishirikiana kuzalisha Mali ni rahisi kumudu mahitaji ya nyumba Yao.

7. Vyombo vya habari vinayo nafasi kubwa;
Kwanza waajiriwa WA vyombo vya habari wawe na vigezo maalumu Kama vile elimu kuanzia shahada, au stashahada sio mbaya. Ili wawe na upeo wa kufanya kazi kisomi na kiupeo mkubwa. Maadili ya kazi za uandishi na utangazaji na maudhui yarushwayo yafuatwe na yalenge kujenga jamii ndoa ikiwemo.

Sio waajiriwa wa vyombo vya habari wawe na elimu ndogo, upeo Finyu na waliookotwa barabarani huko, au wahuni tuu wanaohamasisha upuuzi na mambo yanayovunja jamii.

Media zinanafasi kubwa ya kudhibiti mmomonyoko wa maadili kwenye ndoa.

Kwa sasa media nyingi, hutoa habari zinazohamasisha uasherati na ngono zembe. Media huwapa promo watu mashuhuri wenye kufanya matendo yenye kubomoa maadili ya jamii.

Media zapaswa zifuate maadili ya kazi zao.

Kwa kuhitimisha, Ndoa ni msingi wanmaendeleo ya kijamii, Kisiasa na kiuchumi ndani ya jamii yetu. Kuiheshimu ndoa mi kuiheshimu maendeleo ya nchi.
Ndoa Imara hutoa jamii Imara, hutoa viongozi Imara na Uchumi Imara.
Ndoa zikiwa na Usaliti husababisha jamii kujawa na watu wasaliti, husababisha mpaka viongozi kuwa wasaliti wa wananchi wenzao. Watu waache Usaliti ndani ya ndoa ili jamii iweze kuwa na furaha, iweze kuendelea kijamii, Kisiasa na kiuchumi.

Baada ya kujadili Kwa kifupi mniruhusu niishie hapa.
 
Upvote 10
Mkuu umeelezea faida, madhara na jinsi ya kuyaepuka.
Lakini sijaona sababu za hao wanandoa kuchepuka.

Bikra je?? Haijaongelewa kabisa kwenye huu uzi 😁.
Na kwanini wewe unachepuka,?? labda kutokana na uzoefu wako tutajifunza mengi pia.

Asante.
 
Mkuu umeelezea faida, madhara na jinsi ya kuyaepuka.
Lakini sijaona sababu za hao wanandoa kuchepuka.

Bikra je?? Haijaongelewa kabisa kwenye huu uzi 😁.
Na kwanini wewe unachepuka,?? labda kutokana na uzoefu wako tutajifunza mengi pia.

Asante.

😃😃😃

Mkuu sababu kubwa ni Tamaa mbaya na kushindwa kuithibiti, pia na kutokuwa mwaminifu
 
Suluhisho lako halijakaa sawa. Labda ungesuggest ndoa za mikataba. Mwezi, miezi, mwaka. Hii ingesaidia Kama mmoja akimchoka mwenzie anasubiri mkataba uishe wanamwagana.
 
Suluhisho lako halijakaa sawa. Labda ungesuggest ndoa za mikataba. Mwezi, miezi, mwaka. Hii ingesaidia Kama mmoja akimchoka mwenzie anasubiri mkataba uishe wanamwagana.

Ndoa za mikataba haiwezi kuwa Suluhu kwenye jamii yetu kwani ni jamii masikini.

Ndoa za mikataba ni nzuri kwenye jamii zilizoendelea.

Nashukuru Kwa kuongeza idea nyingine
 
Ndoa za mikataba haiwezi kuwa Suluhu kwenye jamii yetu kwani ni jamii masikini.

Ndoa za mikataba ni nzuri kwenye jamii zilizoendelea.

Nashukuru Kwa kuongeza idea nyingine
Tukianza tutazoea, ndoa nyingi ni jela watu hawana raha wanajilazimisha.
 
Tukianza tutazoea, ndoa nyingi ni jela watu hawana raha wanajilazimisha.


Umenena iliyo kweli.

Watu wengi hawana Raha kwenye ndoa Kwa sababu hawajafundishwa tangu wakiwa watoto kufanya uchaguzi sahihi.

Kinachowaumiza sio ndoa bali ni uchaguzi mbaya wa wenza.

Uchaguzi mbaya upo pia hata katika Kazi, watu wengi hawazifurahii kazi zao Kwa sababu walizichagua Kwa kufuata mkumbo au mazingira yaliwalazimisha. Sasa wanapoanza kazi hujikuta wakisononeka
 
Umenena iliyo kweli.

Watu hawana Raha kwenye ndoa Kwa sababu hawajafundishwa tangu wakiwa watoto kufanya uchaguzi sahihi.

Kinachowaumiza sio ndoa bali ni uchaguzi mbaya wa wenza.

Uchaguzi mbaya upo hata katika Kazi, watu wengi hawazifurahii kazi zao Kwa sababu walizichagua Kwa kufuata mkumbo au mazingira yaliwalazimisha. Sasa wanapoanza kazi hujikuta wakisononeka
Uchaguzi mbaya kwa mwenza unamaanisha Nini? Huwezi jua tabia halisi za mwenzako kama hujaishi nae, kipindi cha uchumba sio rahisi kufahamu tabia maana wengi wanazificha.
Na pia wengine hubadilika tabia baada ya ndoa. Na ukisema serikali ianze kudeal na mambo ya ndoa basi itakuwa balaa, yaani iache kufatilia mambo ya msingi ideal na tabia za watu.
Ndoa haikupaswa kuwepo...ni jela tuliyojiwekea sisi wenyewe.
 
nadhani hii itakuwa toleo jipya la makala kwa wanandoa ,umewasaidia kwa hali ya juu,
 
Uchaguzi mbaya kwa mwenza unamaanisha Nini? Huwezi jua tabia halisi za mwenzako kama hujaishi nae, kipindi cha uchumba sio rahisi kufahamu tabia maana wengi wanazificha.
Na pia wengine hubadilika tabia baada ya ndoa. Na ukisema serikali ianze kudeal na mambo ya ndoa basi itakuwa balaa, yaani iache kufatilia mambo ya msingi ideal na tabia za watu.
Ndoa haikupaswa kuwepo...ni jela tuliyojiwekea sisi wenyewe.

Mkuu pengine bado huijui ndoa ni nini na mchango wake kwenye jamii, taifa na dunia.

Ndoa ni Jambo la msingi kuliko kitu chochote unachodhani.
Serikali lazima iwe inajihusisha na ndoa indirect or direct ways.

Unapozungumzia serikali unazungumzia ngazi ya juu kabisa ya Familia/ndoa.

Ndoa huunda familia, familia huunda ukoo, ukoo huunda kabila/jamii, kabila huunda taifa, taifa huunda dunia.

Familia/ndoa ni Kama Cell Kwa kiumbe(Taifa)
Kiumbe hufanya kila awezacho kuzifanya seli zake ziishi, zidumu na kuwa nguvu.
Seli zikipata madhara mwili/kiumbe hupata madhara.

Seli ni Kama Familia/ndoa.

Ndoa zikiugua na kudhurika automatic Taifa linaathirika Kama sio kufa kabisa.

Kila Jambo linalofanywa na serikali ni Kwa ajili ya ndoa za watu,
Watu waweze kuishi vizuri na salama kwenye familia zao.

Ukishasema serikali jua umeshataja muunganiko wa familia/ndoa za watu.

Kuhusu machaguo sahihi na yasiyo sahihi.

Mtu hubadilika kutegemea na background yake na mazingira yanayomzunguka.
Kama mazingira hayamsapoti mtu kubadilika na background yake haipo vibaya kamwe hawezi kuwa mtu mbaya.

Serikali, dini na viongozi wa Mila wanachangia Kwa kiasi kikubwa anguko la maadili katika ndoa na jamii.
 
Mkuu pengine bado huijui ndoa ni nini na mchango wake kwenye jamii, taifa na dunia.

Ndoa ni Jambo la msingi kuliko kitu chochote unachodhani.
Serikali lazima iwe inajihusisha na ndoa indirect or direct ways.

Unapozungumzia serikali unazungumzia ngazi ya juu kabisa ya Familia/ndoa.

Ndoa huunda familia, familia huunda ukoo, ukoo huunda kabila/jamii, kabila huunda taifa, taifa huunda dunia.

Familia/ndoa ni Kama Cell Kwa kiumbe(Taifa)
Kiumbe hufanya kila awezacho kuzifanya seli zake ziishi, zidumu na kuwa nguvu.
Seli zikipata madhara mwili/kiumbe hupata madhara.

Seli ni Kama Familia/ndoa.

Ndoa zikiugua na kudhurika automatic Taifa linaathirika Kama sio kufa kabisa.

Kila Jambo linalofanywa na serikali ni Kwa ajili ya ndoa za watu,
Watu waweze kuishi vizuri na salama kwenye familia zao.

Ukishasema serikali jua umeshataja muunganiko wa familia/ndoa za watu.

Kuhusu machaguo sahihi na yasiyo sahihi.

Mtu hubadilika kutegemea na background yake na mazingira yanayomzunguka.
Kama mazingira hayamsapoti mtu kubadilika na background yake haipo vibaya kamwe hawezi kuwa mtu mbaya.

Serikali, dini na viongozi wa Mila wanachangia Kwa kiasi kikubwa anguko la maadili katika ndoa na jamii.
Aisee leo Jokajeusi unatema madini tupu.
Hongera, hapa umenena vyema familia ni muhimu hasa katika makuzi ya vizazi.
 
Umeandika Mambo mazuri tatizo ni haya manyanguru.... yanayodanganya watu kwamba maisha ni rahisi huharibu ndoa nyingi sana
 
😃😃😃

Mkuu sababu kubwa ni Tamaa mbaya na kushindwa kuithibiti, pia na kutokuwa mwaminifu
Kuithibiti na kuidhibiti ni maneno mawili yenye maana tofauti muheshimiwa! Vilevile chunga hapo kwenye muaminifu na mwaminifu.Muandiko na mwandiko.Muandishi na mwandishi.
 
Umeandika Mambo mazuri tatizo ni haya manyanguru.... yanayodanganya watu kwamba maisha ni rahisi huharibu ndoa nyingi sana

Naam Mkuu,
Nipigie Kura hapo juu mwisho kabisa wa Uzi
 
Back
Top Bottom