Mwalimu Saidi
New Member
- Jul 17, 2021
- 1
- 0
Ni ukweli usopingika Tanzania kwa sasa tuna wimbi kubwa la vijana wasio na ajira kutokana na mfumo wa elimu kutokuwa rafiki sana kwa vijana kujiajiri, hivyo kupelekea vijana wengi kukata tamaa na kupoteza kabisa malengo yao walojipangia katika maisha.
Laikini ukweli ni kwamba kuna njia nyingi sisi kama vijana tunaweza kuzitumia kutimiza ndoto zetu pasipo tegemea kuajiriwa.
NJIA ZIFUATAZO ZINAWEZA KUWA SULUHISHO LA AJIRA KWA VIJANA.
1.Kutafutana vijana ambao wote wana maono yanayofanana(common goals), ili kuweza kuungana na kufanya jambo kubwa kwa pamoja. Hapa unaweza jiuliza nitapataje watu wenye maono yanayofanana? Ni rahisi tu, unaweza tafuta watu ulosoma nao ambao nao wanapita changamoto kama yako na kuwapa maono yako,mfano mmesomea ualimu na jira zimekuwa ngumu. Mnaweza tafutana mkaamua sasa tuwekeze nguvu katika kilimo badala ya kusubiri ajira. Mkiwa 10 mkaamua mfano tulime mpunga ,kila mtu achangie laki moja mtakuwa na mtaji wa milion moja. Kukodi shamba ni elfu 50 heka, heka kumi ni laki 5. Heka inaweza kutoa zaidi ya gunia ya 30 pale Mbeya, mara 10=gunia 300 kila gunia uza hata kwa elfu 80 mara 300=24,000,000/= Ni mtaji mkubwa sana huu,hata kuajiriwa hutakumbuka tena.
2.Kuwekeza katika biashara ya mtandao,unaweza kubadili maisha kwa kujifunza namna ya kuendesha biashara mtandaoni. Kuna njia nyingi za kujiajiri kupitia mitandao ambazo hazihitaji uwe na mtaji mkubwa bali namna nani ya kutumia mtandao. Mfano unaweza anzisha tovuti((website) ukaibrand ni nini upost na ukaingiza pesa nyingi tu na ni kazi ambao haikubani bali inahitaji ubunifu tu. Pia kuna biashara ya kubadili fedha za kigeni mtandaoni maarufu kama forex( foreign exchange) hii inahitaji usome namna ya kubadili viwango vya pesa kulingana na kupanda au kushuka kwa dola nchi mbali mbali,nayo ni fursa kubwa inayowatoa baadhi ya vijana katika mataifa mbali mbali Afrika. Afrika ya kusini na Nigeria imekuwa ni ishu kubwa kwa vijana kwa sasa. Pitia hapa kwa ushadi(https://www.bis.org/publ/bppdf/bispap73x.pdf). Vile vile unaweza anzisha biashara ndoto kama uuzaji nguo za mitumba,vyombo au mafuta na sababu ukatumia mitandao kama sehemu ya kufikia wateja kwa ukaribu zaidi.
3 Njia ya tatu ni serikali kuanzisha mtaala utakawajenga vijana wenye uwezo wa kujiajiri kwa kuwekeza zaidi kwenye masomo ya vitendo kuliko nadharia. Mfano kilimo kianzie shule ya msingi kama zamani, TEHAMA iwekewe nguvu zaidi kwa kuwekeza kwa wataalamu watoa mafunzo mashuleni na sio mwalimu wa sanaa afundishe TEHAMA. Kuweka program maalum ya kuwapromote watu wenye ubunifu ,hii itachochea zaidi kasi ya ukuaji wa vijana wenye kujiamin na kujikita zaidi kwenye kujiajiri.

Upvote
1