Namna ya kuuaga umasikini

pureman2

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Posts
1,494
Reaction score
2,540
Leo nimeamua kuanzisha thread itakayodumu nyakati zote na majira yote . Pia uzi huu unamgusa Kila mmoja wetu.

Tunalo tatizo la umasikini katika jamii yetu. Unazaliwa masikini, unakua kimasikini, unaanzisha familia masikini, unakufa masikini, na wanao wanaendeza vicious cycle of poverty"

Ili kuondokana na dhahama hii ni vizuri kuwa na maarifa sahii na mbinu za kuvunja mnyororo huu wa umasikini.

Hivyo, naomba tushirikishane wakuu mbinu, mitizamo, hamasa, na maarifa ya kuushinda umasikini.

Mimi naanza : zifuatazo ni mbinu zinazoweza kuvunja mnyororo wa umasikini.

Kama huna uchumi wa kati usizae.

Ukitimiza miaka 25 hama eneo ulilozaliwa.

Ushinde ulevi wa sex.

Usiache kujielimisha na kujiongezea ujuzi.

Karibuni, tupia hints zako.
 
Africans likes poverty, in order to prove that. just wait for their comments.

2-kwa wengi watakaoelewa nilichoandika
watabadirisha walichotakata kuandika baada ya kusoma hiyo sentence hapo juu ili kuendana na mchangiaji wa kwanza kwenye uzi huu.

Pia wengine watakaoelewa wataandika ili mradi kupinganga na kifungu cha maneno namba 2 hapo juu.

Wengi Ambao hawajaelewa nilichoandika kwa kutumia English ndo watatoa mawazo yao ya kweli ambayo mara nyingi huwa ni negative. Wengi wakimaliza kusoma hii comment hawatochangia sababu ya UOGA na KUTOKUJIAMINI.


Chanzo kingine cha umasikini Africa ni UOGA, KUTOKUJIAMINI. kukosa misimamo imara juu ya mawazo/fikra/maamuzi yao. Bila kutokomeza hayo tutabaki na umasikini...
 
Binafsi tujibidiishe kutafuta maarifa maana naamini mtu akiwa maskini kichwani Basi atakuwa maskini mpk huku kwenye real life labda itokee bahati ya mkenge tu..
 
Badala ya kulalamika huna ajira uja smart phone yako ya laki 5 kisha nunua ya laki au kiswaswadu. pesa inayobaki anzisha biashara ndogo.
 
Aaaaaaah ulevi huu wa sex mgumu Sana - japo inabidi tujikane
 
Nakubaliana na wewe jambo Moja hapo kutafutia mafanikio nyumbani ukianza kunyanyuka kidogo kuna changamoto zake hasa ndugu na jamaa kujiona na wao ni wamiliki wa biashara yako au kazi mwisho wa siku usipokuwa makini juhudi zako zitakwama
au ndugu kukugeuza chuma ulete au mlipa fadhila
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…