Basi tulilolitumia ambalo lilikwama njiani tukasaidiwa na RTO (Regional Traffic Officers)
Picha linaanza kwanza basi lilichelewa kuondoka, badala ya Saa Nane Kamili, tuliondoka Nane na Nusu Mchana.
Pili namba ya gari iliyoandikwa kwenye tiketi tulizokata ni tofauti na basi tulilolikuta kituoni na kutakiwa kusafiri nao.
Majira ya Saa Mbili Kasoro Usiku, gari ikazimika tukiwa Korogwe mkoani Tanga
Baada ya kukaa pale kwa takribani saa mbili yaani dakika 180 bila kupata muafaka, wawakilishi wa Kampuni ya BM wakawasiliana na bosi wao ambaye aligoma kulet basi lingine, badala yake akataka atafute Coaster mbili ndio zije zitubebe.
Baada ya muda dereva naye akapotea katika mzingira tata, ilipofika 3 hours tangu tulipokwamba, ikabidi tuwasiliane na DTO wa Korogwe, Mshangama Nyangasa ambaye tunashukuru aliagiza vijana wake Askari mafundi waje kutoa msaada.
Ndani ya dakika 15 tu basi likawaka na tukatakiwa kuendelea na safari, wakati wale staff wa BM walipambana kwa saa tatu bila mafanikio huku bosi wao akileta porojo nyingi.
Nitumie nafasi hii kupitia JamiiForums kumpongeza DTO wa Korogwe na Askari wake kwa kutupa msaada, lakini niwaambie tu BM wajitafakari kwa kilichotokea.