Nampeleka Mahakamani Mwanamke niliyezaa naye kwa kushindwa kumhudumia mwanaye. Hoja nitakazopeleka Mahakamani ni hizi

Nampeleka Mahakamani Mwanamke niliyezaa naye kwa kushindwa kumhudumia mwanaye. Hoja nitakazopeleka Mahakamani ni hizi

Na mahakama ikibisha waambie kabisa siku mko chumbani mnatafuta huyo mtoto ushahidi wa video unao vile jinsi alikua anakung'ang'ania ili usi wash-out ni yeye mwenyewe ndo aling'ang'ania mpira uingie wavuni wakati we ulitaka kugongesha besela
 
NAMPELEKA MAHAKAMANI MWANAMKE NILIYEZAA NAYE KWA KUSHINDWA KUMHUDUMIA MWANAYE. HOJA NITAKAZOPELEKA MAHAKAMANI NI HIZI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Lazima naye ahudumie. Sikumtuma abebe mimba na anizalie mtoto. Wakati tunafanya alivyokuwa anajichetua, kujibinjua, kubiringita, kujipogoa na kunengua achimenengule kama Akudo band alikuwa akichekelea. Hakujua ikiingia mimba kuna majukumu ya kulea?

Anyway! Hizi ndio Hoja ambazo nimeziandaa kwa ajili ya kungurumisha kesi Mahakamani. Na lazima nipate pesa za matumizi ya mtoto kutoka kwa huyu Mwanamke niliyezaa naye;

1. Uroda tulipata Nusu kwa Nusu tena yeye ndiye alihitaji nyongeza.
Ndugu Mhe. Hakimu. Upatikanaji wa mtoto huyu ni matokeo ya uchu na tamaa zetu mbaya ambazo hata hivyo zilitufurahisha kwani tulistarehe. Na wote tulienjoy Hasahasa huyu Mwanamke yeye alihitaji nyongeza. Na aliipata.
Kama tulivyoshirikiana kupata uroda siku ileile nusu kwa nusu. Basi tushirikiane pia nusu kwa nusu kuwajibika na matokeo ya Uroda ule ambao ndio huyu mtoto wetu.

2. Jenetikali tumempa mtoto Nusu kwa Nusu vinasaba vyetu.
Tena Hakimu kama utakuwa unamacho yanayoona vizuri hutoshindwa kuona kuwa huyu mtoto kachukua sura kutoka kwa Mamaake zaidi. Sisemi kwamba hiyo itamfanya awe na Wajibu zaidi wa kumhudumia mtoto. Ila najaribu kueleza kuwa hata Mwanamke anatakiwa kutoa huduma kwa mtoto wake nusu kwa nusu kwa mwanaye kama alivyochangia chromosome 23 na Mimi chromosome 23 ambayo ndio imemfanya mtoto huyu awe na 46 chromosome.
Kila mtu atunze chromosome zake 23 alizompa huyu mtoto.

3. Haki Sawa .
Mheshimiwa. Hakimu. Kwenye haki Sawa huyu ni mtoto wetu sote. Hivyo ni wajibu wetu kutoa huduma Sawa kiwajibu na kwa Mujibu wa sheria. Kwa mfano kama matumizi na huduma ya mtoto ni 300,000/= kwa mwezi basi kila mzazi atoe 150,000/= kwa sababu ndio Haki.
Mtoto ni mali yetu sote.
Kama kuna atakayetaka kutoa zaidi kwa hiyari/mapenzi yake kwa mtoto hiyo isihusianishwe na sheria na isitajwe hapa Mahakamani kwa sababu ni hiyari na mapenzi ya mtu.

4. Hii itamfanya Mwanamke huyu atafute kazi ya kufanya ili awe na faida kwa taifa.
Mwanamke kumhudumia mtoto wake italisaidia taifa kuondoa utegemezi.
Ndugu Hakimu, nashukuru kwa sababu kwenye kesi hii wewe ni mfano wa wanawake wanaofanya kazi. Na kulitumikia taifa. Ninauhakika hata wewe unahudumia watoto wako. Na hii inapunguza utegemezi ndani ya nchi.

5. Itapunguza kuzaa bila mpango na itadhibiti idadi kubwa ya Watu wasio na tija.
Wanawake wengi wanaozaa watoto wengi ni kwa sababu hawawajibiki kuwatunza na kuwahudumia. Ni aidha wawapelekee Mama na baba zao(Bibi na babu). Au watakuwa wanasumbua wanaume waliozaa nao wawahudumie .
Mwanamke anayehudumia watoto wake ni ngumu kuzaa idadi ya watoto wengi asioweza kuwalea.
Hii itafanya watoto watakaozaliwa wawe na tija.

Mhe. Hakimu, kesi hii kama angekuwa mke wangu au mwanamke ninayeishi naye ingekuwa tofauti kidogo katika hoja zangu nilizotoa. Kwa sababu tungekuwa kitu kimoja yaani familia. Na mimi kama mwanaume ambaye ni mume ningebeba jukumu la Baba na Mume. Lakini kwa sasa sisi hatuishi pamoja hivyo nimebaki na jukumu la Baba na yeye kabaki na jukumu la Mama. Na sisi sio kitu kimoja, sisi sio familia. Ndio maana hii kesi ipo mahakamani.
Naomba hiyo pesa ya matumizi na huduma iingizwe kwenye akaunti yangu ya Benki au namba ya simu anayotumia kuwasiliana na Mimi.
Asante sana.

Sabato Njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Lea mtoto acha upumbavu mtoto wakiume unampeleka mwanamke mahakamani kwaajir ya nini..
Kweli tunakoelekea kuna wanaume wanatoka kwenye reli alafu wao wanajiona wapo sawa tu

Sent from my motorola one macro using JamiiForums mobile app
 
Kwakuwa ni maoni yako, nayaheshimu.
Ila mwanaume Mkristo anayewaza majukumu ya 50/50 ni mpumbavu na ni mbaya kuliko asiyemuamini Kristo.

Mwanaume Mkristo lazima aitunze na kuilinda familia yake, asimtegemee mwanamke pesa yake kabisa ila amtegemee Mungu kama msaada wake mkuu pamoja na maarifa aliyokuwa nayo. Afanye kazi kwa bidii na kutegemea Mungu ataibariki kazi ya mikono yake.

Mwanaume Mkristo ni mwanajeshi anayemfuata Yesu, akishindwa kumpenda mwanamke wake, ameshindwa kuonyesha upendo wa Yesu kwa mwanamke huyo. Upendo wa Yesu ni utoaji na sio kupokea kila kitu zaidi ya utii kutoka kwa mwanamke. Mwanaume ni natural giver na kutokana na utoaji huo, mwanamke ataonyesha upendo wake kupitia utii.
Ni huu ukristo unaobariki mashoga ndiyo hautambui 50 50? Au kuna mwingine

Mtoa mada yuko Ok sana wanaume tukifungua kesi za kutosha kuhusu hii 50 50 nadhani itakufa kifo cha asili kwa sababu 50 50 ni mzigo kwa wanawake wenyewe kama wanaume tukiizingati

Ukisema 50 50 maana yake tayari unanipunguzia mimi mwanaume majukumu
Kinachotakiwa ni kusimamia kile mnachotaka
Siyo 50 50 kwenye mambo rahisi tu

Mimi nilikuwa na wazo mtoto akizaliwa kwa kuwa ni wetu sote tushirikiane, na baba apeleke huduma mpaka mtoto afikishe miaka saba
Baada ya hapo baba amchukue mtoto na mama ndiyo awe anapeleka huduma kwa baba na kama kuna mahitaji ya shule tupokezane kila mwaka kuanzia ada na mahitaji mengine
 
Sasa mbona sijaona mahali uliposema mligawana majukumu ya kumpikia, kumfulia, kumuogesha, kumuuguza akiumwa na malezi yote kiujumla, ukiachilia mbali kubeba ujauzito, kumzaa na kumnyonyesha ambayo hayo huwa hamyahesabii kwa kisingizio kwamba ni majukumu ya kimaumbile
 
Ni huu ukristo unaobariki mashoga ndiyo hautambui 50 50? Au kuna mwingine

Mtoa mada yuko Ok sana wanaume tukifungua kesi za kutosha kuhusu hii 50 50 nadhani itakufa kifo cha asili kwa sababu 50 50 ni mzigo kwa wanawake wenyewe kama wanaume tukiizingati

Ukisema 50 50 maana yake tayari unanipunguzia mimi mwanaume majukumu
Kinachotakiwa ni kusimamia kile mnachotaka
Siyo 50 50 kwenye mambo rahisi tu

Mimi nilikuwa na wazo mtoto akizaliwa kwa kuwa ni wetu sote tushirikiane, na baba apeleke huduma mpaka mtoto afikishe miaka saba
Baada ya hapo baba amchukue mtoto na mama ndiyo awe anapeleka huduma kwa baba na kama kuna mahitaji ya shule tupokezane kila mwaka kuanzia ada na mahitaji mengine
Hivi hapo uliposema 50 50 itampunguzia majukumu mwanaume, umejumlisha na majukumu kama kupika, kuosha vyombo, kufua, kusafisha nyumba pamoja na kulea hao watoto au hayo siyo majukumu
 
Shenz ushaanza kuleta udini hapa. Usitaje bure jina la bwana Mungu wako. Shenziiii [emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji41]
Wapi nimelitaja jina la Bwana Mungu wangu?
Mungu wangu ana jina alilomwambia Musa katika sura ya kijiti, Mungu ni cheo chake ila jina lake sijalitaja kabisa.
 
Kwani ilikuaje maana mara nyingi mama ndo anabakigi na mtoto imekaaje kwako ikawa vaisvesa au mtoto ana umri gani
 
Back
Top Bottom